Madai, kesi, na hukumu ya kuruhusu wafungwa kupinga kura ni kielelezo kingine cha maono mafupi ya wanasheria na mawakili wa Tanzania

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,949
Kwenye sheria na mahakamani wanao msemo wa mahakama siyo mama yako. Dhana hii inaelekeza kuwa mahakama itakupa tu kile ulichoomba na kuthibitisha stahiki ya wewe kupewa.

Hivi karibuni imetolewa hukumu na mahakama yetu kufuatiwa kuombwa na mawakili kadhaa kuwa wafungwa wanayo stahiki ya kupiga kura. Walioomba wamepewa walichoomba baada ya kuirizisha mahakama.

Kwa mjibu wa katiba yetu, kila mtu anayostahiki ya kupiga na kupigiwa kura bila kujali muktadha msingi ambao ndipo kesi iliposimama. Kwamba mtu kuwa jela hakumnyimi stahiki yake.

Swali kama siyo ukosefu wa weledi na maono mafupi ya mawakili na wanasheria wetu waliofungua kesi hiyo kwa nini hawakuomba pia wafungwa apewe stahiki yao ya kupigiwa kura?

Kuna maslahi gani nyuma ya hii kesi na hukumu iliyotolewa?
 
Back
Top Bottom