Madagascar: Waziri wa Elimu atimuliwa baada ya kununua pipi za Tsh. Trilioni zaidi 4 ili kuwasaidia watoto kunywa mitishamba ya #Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
File image of lollipops

Waziri wa elimu nchini Madagascar amefukuzwa kazi kwa sababu ya mipango yake ya kuagiza peremende au pipi zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 2 sawa na (£1.6m) kwa watoto wa shule.

Rijasoa Andriamanana amesema wanafunzi watapewa pipi tatu kila mmoja watakazokula baada ya kunywa dawa ya mitishamba inayodaiwa kutibu virusi vya corona nchini humo ambayo bado haijathibitishwa.

Mpango huo ulitupiliwa mbali baada ya kupingwa na rais wa Madagascar.

Rais Andry Rajoelina anapigia debe dawa ya mitishamba walioibaini kama yenye uwezo wa kutibu virusi vya corona.

Nchi kadhaa za Afrika zinaendelea kuagiza dawa hiyo ya mitishamba inayoaminiwa kusaidia katika kukabiliana na virusi vya corona lakini Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonya kuwa dawa hiyo bado haijathibitishwa kuwa na uwezo huo.

Taasisi ya Taifa ya Matibabu nchini Madagascar pia nayo imetilia shaka uwezo wa dawa hiyo inayotokana na mmea wa pakanga yaani (Artemisia) ikisema kwamba inaweza kusababisha matatizo ya afya kwa watu.

_112232946_gettyimages-1210464474.jpg
Bwana Rajoelina alisema kama taifa la ulaya lingetengeza dawa, mapokeo yangekuwa ya tofauti
Rais Rajoelina amepuuzia ukosoaji juu ya dawa hiyo ya mitishamba, akisema ni wazi kuwa nchi za magharibi inadharau uwezo wa Afrika.

"Kama ingekuwa ni nchi ya Ulaya ambayo imegundua dawa hii, Je kungekuwa na mashaka kiasi hiki, Sidhani," aliambia chombo cha habari cha Ufaransa cha France 24.

Karibia watu 1,000 wamethibitishwa kupata virusi vya corona nchini humo, pamoja na vifo saba ambavyo vinahusishwa na virusi hivyo.

Hatua za kutotoka nje pia zimewekwa lakini Rais Rajoelina amekosolewa vikali kwa jinsi alivyokabiliana na janga hilo nchini humo.

Mapema wiki hii kulitokea vurugu katika mji uliopo mwashariki mwa nchi hiyo wa Toamasina, ambapo wanajeshi wamepelekwa eneo hilo kuhakikisha raia wanatekeleza hatua za kukabiliana na corona zilizowekwa na wizara ya afya.

Chanzo cha ghasia hizo ni mchuuzi wa barabarani aliyepigwa na vikosi vya usalama. Hata hivyo maafisa wamekanusha madai ya kutekeleza vurugu za aina yoyote ile.

Taarifa nyingine unazoweza kuvutiwa nazo:

Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona?
 
Jamani $2Mil ni sawa na Trilion za shillings, hii shilling sasa itakuwa na value sawa na hela ya Zimbabwe...aisee shule zifunguliwe watu wafanyiwe revision ya hesabu..

Everyday is Saturday.......................... :cool:
 
Afrika

Ila majina ya hawa majamaa nayaelewa sana rajolina ravaromanana
 
File image of lollipops

Waziri wa elimu nchini Madagascar amefukuzwa kazi kwa sababu ya mipango yake ya kuagiza peremende au pipi zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 2 sawa na (£1.6m) kwa watoto wa shule.

Rijasoa Andriamanana amesema wanafunzi watapewa pipi tatu kila mmoja watakazokula baada ya kunywa dawa ya mitishamba inayodaiwa kutibu virusi vya corona nchini humo ambayo bado haijathibitishwa.

Mpango huo ulitupiliwa mbali baada ya kupingwa na rais wa Madagascar.

Rais Andry Rajoelina anapigia debe dawa ya mitishamba walioibaini kama yenye uwezo wa kutibu virusi vya corona.

Nchi kadhaa za Afrika zinaendelea kuagiza dawa hiyo ya mitishamba inayoaminiwa kusaidia katika kukabiliana na virusi vya corona lakini Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonya kuwa dawa hiyo bado haijathibitishwa kuwa na uwezo huo.

Taasisi ya Taifa ya Matibabu nchini Madagascar pia nayo imetilia shaka uwezo wa dawa hiyo inayotokana na mmea wa pakanga yaani (Artemisia) ikisema kwamba inaweza kusababisha matatizo ya afya kwa watu.

_112232946_gettyimages-1210464474.jpg
Bwana Rajoelina alisema kama taifa la ulaya lingetengeza dawa, mapokeo yangekuwa ya tofauti
Rais Rajoelina amepuuzia ukosoaji juu ya dawa hiyo ya mitishamba, akisema ni wazi kuwa nchi za magharibi inadharau uwezo wa Afrika.

"Kama ingekuwa ni nchi ya Ulaya ambayo imegundua dawa hii, Je kungekuwa na mashaka kiasi hiki, Sidhani," aliambia chombo cha habari cha Ufaransa cha France 24.

Karibia watu 1,000 wamethibitishwa kupata virusi vya corona nchini humo, pamoja na vifo saba ambavyo vinahusishwa na virusi hivyo.

Hatua za kutotoka nje pia zimewekwa lakini Rais Rajoelina amekosolewa vikali kwa jinsi alivyokabiliana na janga hilo nchini humo.B

Mapema wiki hii kulitokea vurugu katika mji uliopo mwashariki mwa nchi hiyo wa Toamasina, ambapo wanajeshi wamepelekwa eneo hilo kuhakikisha raia wanatekeleza hatua za kukabiliana na corona zilizowekwa na wizara ya afya.

Chanzo cha ghasia hizo ni mchuuzi wa barabarani aliyepigwa na vikosi vya usalama. Hata hivyo maafisa wamekanusha madai ya kutekeleza vurugu za aina yoyote ile.

Taarifa nyingine unazoweza kuvutiwa nazo:

Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona?
Badilisha kichwa cha habari siyo tiilioni hata mimi nilishtuka, maana magadascar haina uchumi huo na huenda hata wizara yao ya elimu haina hiyo pesa.
 
Back
Top Bottom