Zanzibar: Matumizi ya Dawa za Mitishamba chanzo cha Watu 12,000 kupofuka Macho

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Matumizi holela ya dawa za mitishamba zisizokuwa na uhakika ni miongoni mwa sababu zilizopelekea watu 12,000 Zanzibar kupata matatizo ya ugonjwa wa macho yakiwemo uoni hafifu bila ya wenyewe kujitambua.

Akizungumza na Mwananchi Digital mjini Unguja jana mratibu afya msingi matibabu ya macho, Dk Rajab Mohamed Rajab alisema idadi hiyo ya watu ambao wanamatatizo ya macho ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguni (WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.

Ameleza kuwa uwepo wa hali hiyo unatokana na jamii kutojiwekea kabisa utaratibu wa kupima afya ya macho kila baada ya muda kama wanavyofanya vipimo vyengine.

Amesema kuwa zipo sababu mbalimbali ambazo zinapelekea watu kupata matatizo ya macho na kuzitaja kuwa kuanzia umri wa miaka 50 kuna uwezekano wa kupatatizo hilo pamoja na presha ya macho, mionzi ya jua na hata simu kwa watoto wadogo.

Kuhusu watoto wenye umri mdogo mtalamu huyo alisema kila kwenye idadi ya watu 100,000 ndani yake kuna watoto 10,000 wanavaa miwani kutokana na matatizo ya ugojwa wa macho ambao wengine wanasababishwa na urithi pamoja na dawa ambazo wamekua wakitumia wazazi na watoto wenyewe.

Aliitaka jamii kuacha tabia za kukaa na matatizo ya macho pale wanapoona dalili zikiwemo za kutoka machozi mara kwa mara pale wanapopigwa na mwanga na kuacha kabisa kutumia dawa bila ya kufika vituo vya afya.
 
Wazee wa za " Kisuna" wazee wa mujarabu, hospitali hamtakinkujenga, mnauziana mamizizi eti muwe na uwezo wa kuwashughulikia wake wengi kumbe mnaathiri mzunguko wa damu Moyo na pressure ikiwepo ya macho ambayo ni chanzo Cha upofu
 
Hzi data zinapikwa tu ili watu wafanye biashara zao wazee wetu walitumia hyo miti shamba waliishi miaka 100+ sisi tuaotumia hzo za hospital hata miaka 50 tunaitafuta kwa tochi na tukifika tunaumwa kila sehemu yaani hyo haina tofauti na makamba ile tafiti yake kwamba wanaotumia mkaa wanakufa mapema kuliko wanaotumia gas.
 
Back
Top Bottom