LadyAJ
JF-Expert Member
- Oct 21, 2015
- 7,173
- 9,631
Tutake radhi watoto tuliokulia uswahilini, kule ndo kwetu Yale ndo maisha yetu hata kama utaponda ni yaliyojaa mabaya! Wengi wetu humu hatujakulia kwenye mageti na suala la tabia mbaya ni la mtoto mwenyewe na ushirika wa mzazi katika malezi yake!Hii imenikuta kwa mtoto wangu , Mpaka amaefikisha miaka miwili na nusu alikuwa hajui kuongea vizuri nikashindwa kumpeleka shule.
Baadae ikabidi nimtoe nyumbani kwangu nimpeleke kwa shangazi yangu kwake ana wajukuu wengi japo napo ni gate kali ila watoto wapo wengi.
Alipokaa pale kwa muda wa mwezi mmoja na nusu tu nikaanza kuona changes hata nikiongea naye kwenye simu anaongea kitu kinachoeleweka. nilimuacha kwa miezi mitano kisha nikamchukua sasa hivi nikirudii kazini huwa ananisimulia kila kitu hata kama dada wa kazi alimchapa anasema tumrudishie.
Naunga mkono hoja ila sishauri kuruhusu watoto wakacheze na hawa wenzao wa uswahilini kwa sababu wanatabia za hovyo sana sijui huwa wanafundishwa na wazazi wao au huwa wanaiga tu bila kujua kuwa hili ni baya.
Bahati nzuri babangu hakuwaga na uwezo wa kunilea geti Kali kipindi hiko ila kakake alikua na uwezo sana full geti maisha ya gari na viyoyozi vya kizamani,ila Leo hii ukiwaona watoto wake walivyoharibika kwa tabia mbaya walizofunzwa kwa kufungiwa magetini huwezi mtukana mtoto wa uswazi kama mimi ambaye nakifurahia kitaa kwa kunijuza mema na mabaya