Mwanangu anatapika kila anapokula chakula, nini tatizo na dawa yake?

impelle

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
832
1,100
Poleni na kazi.
Mwanangu ana mwaka na miezi miwili, huyu mtoto ni wa kiume, tangu aanze kula chakula cha kawaida kwa watoto wadogo ( tunatumia celeriac, pia huwa wanamuandalia vingine kwa kusaga).

Tatizo ni kuwa kwanza sio mpenzi wa kula, ingawa anapenda kunyonya na akinyonya hatapiki, pili ikitokea akilishwa vijiko viwili vitatu anatapika, kwa hivyo unakuta analishwa kwa muda mrefu huku wakicheza naye nk, maana wakimlisha serious basi anatapika.

Akishatapika basi tena anacheka anafurahi anaendelea na kucheza, tumewahi kufanya vipimo mbalimbali na tulihisi ni uvivu wa mtoto kula au hiyo hali itakoma hata hivyo tunaona inaendelea.

Naomba kutumia hili jukwaa kuomba ushauri juu ya hii hali huenda kuna mmoja wetu aliwahi kukutana nayo, hii ni hali ya kawaida au ni nini? Inatibiwaje?

Kama mtu anamjua daktari mzuri sana wa watoto wadogo ( chini ya miaka 5) hapa jijini mwanza au kwingineko anaweza kunambia jina au hata mawasiliano yake inbox ili niweze kutatua hili tatizo. Natanguliza shukrani. Ahsante sana
 
kawaidaa,

Usimlishe maugali, mpe vitu laini... pondaponda hata viaz mviringo

Maugali jau, mimi mwenyewe nikila maugali nahisi kutapika sema tu Roho mtakatifu yu ndani mwangu, ananiongoza japo nina komwe.
 
Back
Top Bottom