MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Habari wakuu,

Naomba msaada wa mawazo kuhusu hili.

Mwanangu ana umri wa miaka 3 na miezi 8 ila bado hajaweza kuongea vizuri anaongea baadhi ya maneno kama baba, mama, bibi yaani kwa kuyahesabu hayafiki hata 30.

Nimejaribu kumpeleka Muhimbili kitengo cha speech ila tofauti haionekani sasa mitaani nakutana sana na ushauri kwamba nimpeleke kwa watalaam akaangaliwe kama ana UDATA.

Mama yake anasema ameshachunguza watoto wawili na anaona kuna tofauti kubwa katika ndimi zao kwa chini ila sasa hofu yangu ni kweli hili jambo lipo?
Naomba kama kuna ambaye aliishamfanyia mwanae hiki kitu aniambie pia anipe na risk zake.

Asante.

Jaribu ' Kumlambisha ' sana Pilipili kwa Siku 14 mfululizo mara mbili kwa Siku atawahi kuzungumza mwenyewe.
 
"UDATA" ndiyo nini?
"Hujambemenda" kweli huyo mtoto?!

Kingine mtoto kuchelewa kuongea inachangiwa na ikiwa mtoto alipatwa na homa/maradhi makali pindi akiwa mchanga.

Mpe pole sana jitahidi kumchanganya na watoto wa uswazi kwenye michezo yake.
Hii kitu kubemenda sijui unamaanisha ile kuzaa mtoto mwengine wakati huyu bado akiwa mchanga?kama ndo unavyomaanisha basi sivyo mkuu ninaye huyu huyu mmoja.ila nakushukuru kwa maoni yako
Mwambie mama ake amlambishe mwiko akishapikia
Asante sana mkuu...
je mwanao ananyonya kidole? kama ananyonya kidole huchangia pia kuchelewesha kuongea. Mwanangu kaanza kuchanganya maneno sasa baada ya kutimiza miaka mitano. Nilimpeleka Aga Khan kulikuwa na speech therapist anaitwa Hilda, ni mama mtu mzima alisaidia kumfanya achanganye maneno.
Usifuate sana shaka za wanadamu maana kila mmoja hujifanya mjuaji, watoto hutofautiana katika makuzi. Kuwa na shaka kama akifika miaka 5 na haongei vizuri. Kwa sasa ni kawaida tu.
Yah mkuu mtoto anapenda sana kunyonya vidole,asante kwa ushauri.
 
Habari wakuu,

Naomba msaada wa mawazo kuhusu hili.

Mwanangu ana umri wa miaka 3 na miezi 8 ila bado hajaweza kuongea vizuri anaongea baadhi ya maneno kama baba, mama, bibi yaani kwa kuyahesabu hayafiki hata 30.

Nimejaribu kumpeleka Muhimbili kitengo cha speech ila tofauti haionekani sasa mitaani nakutana sana na ushauri kwamba nimpeleke kwa watalaam akaangaliwe kama ana UDATA.

Mama yake anasema ameshachunguza watoto wawili na anaona kuna tofauti kubwa katika ndimi zao kwa chini ila sasa hofu yangu ni kweli hili jambo lipo?
Naomba kama kuna ambaye aliishamfanyia mwanae hiki kitu aniambie pia anipe na risk zake.

Asante.
Mm binafsi nilichelewa kuzungumza nilipokuwa mdogo na neno langu lilikuwa baba,

Tatizo ni nyama au mishipa inayoshika ulimi kwa chini, ukitazama utaona ulimi haunyanyuki vizuri kama ukijaribu tena kutazama mwambie alete ulimi nje hautaona ncha nyembamba ya ulimi,
Hii inatokana na kwamba manesi hawakupitisha kidole sawa sawa wakati Wa kuzaliwa kwa mtoto au mazoezi hafifu uchangani ya kuinua ulimi.

Tiba
Kutafuta wataalamu hospital au kwa wanajamii wajuzi Wa mambo wamkate hata kidogo, Mimi binafsi nilipona baada kukatwa hicho kilimi na bibi yangu ambaye alikuwa na ufahmu Wa mambo ya kitamaduni katika matibabu, lkn baadae mama yangu aligundua kuwa hapakukatwa vizur kwan sizungumzi neno likasika kwa urahisi kwa MTU hata nikitoa ulimi nje hauonyeshi ncha ya ulimi.

Nb
Watoto wengi Wa kiume huchelewa kuongea hata mm ninaye wangu approaching to 2 hajanyoosha maneno.

Kabla ya hospitali kulikuwa na tiba.
 
Mchanganye na watoto wa kiswahili tu mtaani ataweza.. we unamfungia kilasiku ndani hachangamani na watoto wenginewategemea ataongeaje!!
 
Idadi hiyo ya maneno ni ndogo sana kwa mtoto wa miaka minne lakini hana huo "udata" unaoambiwa. Kwani wewe ukiongea sehemu ya chini ya ulimi inanyanyuka kwa kiasi gani?

Kama ndo hivyo angeshindwa kuongea maneno machache sana labda yenye "L". Ile kwamba anaongea japo maneno machache ni ishara nzuri kuwa si kiziwi kabisa. Endelea kumpeleka kwa madaktari bingwa wa eneo hilo.

Google pia utapata mawili matatu. Pia maadam nyumbani kuna watu wanaomsemesha au anaowasikia wakiongea hata kwenye TV na redio, huhitaji kumpelekapeleka kwenye nyumba za watu ili aongee; kuwa na subira.
 
kubemenda mtoto ni kufanya mapenzi nje ya ndoa kabla mtoto hajatembea au kuanza kuongea
Aisee mkuu ktk hilo kundi nitoe kabisa maana kama ingekuwa kuiona pepo ni kuheshimu ndoa tu basi mimi pepo ingekuwa yangu bila shaka yoyote.ila nashkuru umenifamisha.
 
Back
Top Bottom