Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,519
- 870,046
- Thread starter
- #1,381
Abiria mmoja wa kiume amefariki dunia ndani ya ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka Nairobi, Kenya, kwenda Lagos, Nigeria, siku ya Jumanne, Oktoba 6, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la ndege la Kenya Airways iliyotolewa Jumatano, Oktoba 7, abiria huyo alikutwa akiwa hajitambui majira ya saa 3:20 usiku kwa saa za Nigeria, ikiwa ni takribani dakika 20 kabla ya ndege kutua Lagos. Taarifa zinasema awali abiria huyo alikuwa ameonyesha hali ya kutotulia akiwa ndani ya ndege.
Wahudumu wa ndege walitoa huduma ya kwanza na kutekeleza taratibu za dharura za kitabibu wakati ndege ikiendelea na safari.
Ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed (MMIA), Lagos, saa 3:41 usiku, ambapo wahudumu wa afya waliokuwa wakisubiri walipanda ndani ya ndege na kuthibitisha kifo cha abiria huyo.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nigeria (NCAA) imesema polisi wamechukua jukumu la uchunguzi ili kubaini mazingira halisi yaliyopelekea kifo hicho.
Kenya Airways haijataja jina, uraia wala historia ya kiafya ya marehemu, ikieleza kuwa inazingatia taratibu za faragha za abiria.
Shirika hilo limetoa pole kwa familia ya marehemu na kusema linaendelea kushirikiana na mamlaka za Nigeria pamoja na wadau wa usafiri wa anga katika uchunguzi na taratibu zinazohitajika.