Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

๐—ž๐—ถ๐—ด๐—ผ๐—บ๐—ฎ, ๐—ง๐—ฎ๐—ป๐˜‡๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ฎ - Ukarabati na maboresho ya uwanja wa Ndege wa Kigoma umefikia asilimia 60 ya utekelezaji hadi kufikia Juni 2026.

Mradi unaotekelezwa na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group kwa gharama ya shilingi bilioni 51.4 unajumuisha ujenzi wa jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuhudumia watu 500 kwa wakati mmoja.

Njia ya kurukia ndege yenye urefu wa kilomita 1.8 tayari imekamilika, huku ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege, ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, na jengo la mitambo ya umeme kwa ajili ya Taa za uwanjani ukiendelea.

Pia kumefanyika upanuzi wa eneo la maegesho ya magari pamoja na ujenzi wa uzio kuzunguka uwanja mzima.

Mradi unatarajiwa kukamilika rasmi Julai 2026 na huduma zianze kutolewa kikamilifu kuanzia Novemba mwaka huu.

Maboresho haya yanalenga kuufanya uwanja wa Kigoma kuwa kitovu cha usafiri wa anga katika ukanda wa magharibi, kukuza biashara na nchi jirani kama Burundi na DRC, pamoja na kuimarisha sekta ya utalii.
 
๐—ก๐—ฎ๐—ถ๐—ฟ๐—ผ๐—ฏ๐—ถ, ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฎ โ€“ Kenya Airways imerudisha huduma ndege yake kubwa ya Boeing 777-300ER na kuwapa abiria nafasi ya kuipanda kwa nauli iliyopunguzwa hadi asilimia 50 katika safari za ndani kati ya Nairobi na Mombasa. Hatua hiyo inakuja wakati shirika hilo likijipanga kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza siku ya Jumatano Juni 24, wakati ndege hiyo iliporudi rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa muda George Kamal alisema Boeing 777-300ER ni ishara ya uthabiti na maendeleo ya Kenya Airways.

Amedokeza kuwa ndege hiyo imewekwa kwa makusudi kwenye njia ya Nairobi-Mombasa ili Wakenya wapate kuipata kabla haijarejea safari za kimataifa.

Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50, Kenya Airways imetoa punguzo la nauli hadi asilimia 50 kama shukrani kwa wateja walioungana nayo kwa miongo mitano.

Ndege hiyo inatarajiwa kuanza safari zake za kimataifa tena Julai 17, 2026, kwa safari yake ya kwanza kuelekea London, hatua ambayo shirika linasema itaimarisha muunganisho kati ya Kenya na maeneo muhimu duniani.
1782698998679.jpg
 
๐—›๐—ฒ๐—น๐—ถ๐—ธ๐—ผ๐—ฝ๐˜๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—ฆ๐—ฎ๐˜‚๐—ฑ๐—ถ ๐—”๐—ฟ๐—ฎ๐—บ๐—ฐ๐—ผ aina ya ๐—Ÿ๐—ฒ๐—ผ๐—ป๐—ฎ๐—ฟ๐—ฑ๐—ผ ๐—”๐—ช139 inayofanya kazi chini ya kampuni tanzu ya Aloula Aviation, imeanguka karibu na bohari ya mafuta ya Ras Tanura nchini Saudi Arabia na kusababisha vifo vya watu wote 14 waliokuwa ndani yake.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili asubuhi, Juni 28, 2026, majira ya saa 12:00 asubuhi kwa saa za huko wakati helikopta hiyo yenye namba za usajili HZ-AL65 ikirejea kutoka kwenye mtambo wa mafuta uliopo baharini.

Data za mtandao wa Flightradar zinaonyesha kuwa ndege hiyo ilipoteza mwelekeo kwa kasi kubwa sana wakati ikikaribia Uwanja wa Ndege wa Ras Tanura.

Wizara ya Nishati ya Saudi Arabia imethibitisha kuwa wahanga wote 14 wa ajali hiyo walikuwa raia wa nchi hiyo.

Tukio hili limetokea siku mbili tu baada ya kampuni hiyo kuanza tena kusafirisha mafuta ghafi kutoka bohari hiyo kufuatia kufungwa kwa miezi minne kutokana na migogoro ya kikanda.

Mamlaka za anga na serikali zimeanzisha uchunguzi rasmi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo, huku kukiwa hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa tukio hilo lilitokana na shambulio au uhasama wa kiusalama.
1782733559184.jpg
 
Mradi wa kutengeneza ndege za abiria za Mitsubishi SpaceJet (awali ikiitwa MRJ) ulifutwa rasmi tarehe 7 Februari 2023 na kampuni ya Mitsubishi Heavy Industries baada ya miaka 15 ya maendeleo na hasara ya takriban dola bilioni 9.

Anguko la mradi huu wa ndege ya abiria ya kwanza kutoka Japan lilisababishwa na changamoto kubwa za kisheria nchini Marekani, ambako sheria za vyama vya marubani (scope clauses) zilizuia ndege hiyo kufanya kazi kwa sababu ya uzito wake mkubwa.

Aidha, kampuni hiyo ilikosa uzoefu wa kupata vyeti vya usalama vya kimataifa kutoka mamlaka za anga kama FAA, hali iliyopelekea mabadiliko ya mara kwa mara ya muundo na ucheleweshaji wa miaka mingi unaofikia mara sita.

Ucheleweshaji huo ulifanya teknolojia ya ndege hiyo kupitwa na wakati ikilinganishwa na mahitaji mapya ya soko yanayojali mazingira.

Mgogoro wa kiutamaduni kati ya wahandisi wa Japan na wataalamu wa kimataifa ulipunguza kasi ya uzalishaji, na hatimaye janga la COVID-19 lililoharibu soko la usafiri wa anga na kutoa pigo la mwisho lililolazimisha mradi huo kufutwa kabisa na mifano ya ndege hizo kuharibiwa.
1782792980409.jpg
 
๐— ๐—ผ๐˜€๐—ฐ๐—ผ๐˜„, ๐—จ๐—ฟ๐˜‚๐˜€๐—ถ - Shirika la ndege la S7 Airlines la nchini Urusi limeweka sheria ya muda inayopiga marufuku maafisa wasaidizi wa marubani (First Officers) kutua ndege katika viwanja vingi vya ndege nchini Urusi.
Sheria hiyo isiyo ya kawaida ilianza Juni 1 na itadumu hadi Oktoba 1, 2026.

Uamuzi huo umefuatia ongezeko la matukio kadhaa ya ndege kutua kwa nguvu (hard landing) na kuharibu baadhi ya miundo ya ndege.

Kwa mujibu wa sheria mpya, marubani wasaidizi wanaruhusiwa kutua ndege katika vituo vinne tu ambavyo ni Moscow Domodedovo, Novosibirsk, Vladivostok na Irkutsk.
Katika viwanja vingine vyote, nahodha wa ndege ndiye anatakiwa kushughulikia utuaji.

S7 Airlines imesema hatua hiyo inalenga kulinda ndege zake zilizosalia dhidi ya kucheleweshwa kwa matengenezo na uhaba wa vipuri.

Hata hivyo, safari za mafunzo zilizopo na waalimu zimeruhusiwa na hazitahusishwa na marufuku hiyo.
1782808544543.jpg
 
Ndege ya kifahari aina ya Boeing 747-8 ilinunuliwa na mwanamfalme wa Saudi Arabia, Sultan bin Abdulaziz, kwa gharama ya takriban dola milioni 280 (karibu bilioni 735) kwa ajili ya safari zake binafsi.

Hata hivyo, mwanamfalme huyo alifariki dunia mwaka 2011, miezi michache tu kabla ya ndege hiyo kukabidhiwa kwake.

Baada ya kifo chake, hakuna mtu mwingine wa familia ya kifalme aliyetaka kuitumia, hivyo ilipelekwa nchini Uswisi ambako ilikaa karakana kwa miaka kumi ikisubiri mteja mpya na kuwekewa samani za ndani.

Licha ya jitihada za kuitafutia mnunuzi mpya kwa bei ya hasara ya dola milioni 95, hakuna aliyejitokeza kuinunua kutokana na gharama kubwa za uendeshaji.

Mnamo mwaka 2022, ndege hiyo ilisafirishwa kuelekea jangwa la Arizona nchini Marekani ikiwa imepaa kwa jumla ya saa 42 tu tangu itengenezwe.

Ndege hiyo ilivunjwa vipande vipande na kuuzwa kama vipuri, ikawa ndiyo ndege mpya zaidi ya aina hiyo kuwahi kuharibiwa bila kuingia kwenye huduma.
1782822809240.jpg
 
๐—ž๐˜‚๐—ฎ๐—น๐—ฎ ๐—Ÿ๐˜‚๐—บ๐—ฝ๐˜‚๐—ฟ, ๐— ๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐˜†๐˜€๐—ถ๐—ฎ โ€“ Jua lilikuwa bado halijapanda sana asubuhi ya tarehe 23 Agosti 2001, lakini katika kona ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur kulikuwa na shughuli nyingi zikiendelea.

Moja ya shughuli hizo ni ndege kubwa aina ya Boeing 747-300 ya shirika la ndege la Saudi Arabian, yenye usajili HZ-AIO, ambapo ilikuwa imekamilisha matengenezo na majaribio ya injini.

Ndege hiyo ilikuwa imepangwa kubeba abiria 319 kwenye safari ya kuelekea Jeddah, Saudi Arabia.

Mafundi 06 walipanda ndani. Hapakuwa na abiria, hapakuwa na wahudumu wa ndege. Kazi yao ilikuwa rahisi tu, kuiongoza ndege hiyo kutoka karakana hadi lango la abiria.

Walianza kuisogeza polepole kwa kutumia injini mbili tu, namba 2 na namba 3. Kila kitu kilionekana sawa, hadi walipofika kwenye kona ya kuelekea njia nyingine.

Ndipo kosa dogo lakini la gharama kubwa lilipotokea. Katika haraka zao za siku hiyo walikuwa wamesahau kuwasha pampu za dharura za mfumo wa haidroliki.

Bila pampu hizo, mfumo mzima wa haidroliki unapoteza nguvu. Breki hazikushika na usukani wa gurudumu la mbele ulikataa.
Ndege hiyo kubwa badala ya kupinda, iliendelea mbele moja kwa moja kama ilivyoamrishwa na injini hizo mbili zilizowashwa na mafundi hao.

Mafundi ndani walijaribu kila njia, wakakanyaga breki, wakageuza usukani, lakini 747 ile haikusikia kitu.

Sekunde chache baadaye, ndege ilitoka nje ya njia ya lami na kwa kishindo kikali pua yake ilizama ndani ya mfereji mkubwa wa zege wa maji ya mvua.

Kelele zilisikika uwanja mzima.
Sehemu ya mbele ya chumba cha marubani ilipasuka na kubonyezeka vibaya.

Lakini bahati nzuri, mafundi wote sita walitoka hai, wakiwa na mshtuko tu, hawakuumia vibaya.

Ndege yenyewe, iliyokuwa na miaka 16, haikuwa na bahati.
Wahandisi wa ndege walipoangalia uharibifu huo walitikisa vichwa.

Gharama ya kuitengeneza ilikuwa kubwa kuliko thamani yake. Kwa hivyo, Boeing 747-300 hiyo iliandikwa rasmi โ€œimeharibika kabisa, haifaiโ€ na safari yake ya mwisho ikaishia kwenye mfereji wa Kuala Lumpur.
1782837593250.jpg
 
๐—›๐—จ๐—ก๐—ง๐—ฆ๐—ฉ๐—œ๐—Ÿ๐—Ÿ๐—˜, ๐—”๐—Ÿ๐—”๐—•๐—”๐— ๐—” โ€” Ndege ya shirika la United Express imekuwa gumzo mtandaoni baada ya ndege yake aina ya Embraer ERJ-145 kutoka Huntsville kuelekea Washington Dulles siku ya juzi, kuruka ikiwa na abiria mmoja tu. Ndege hiyo ilikuwa inaendeshwa na CommutAir.

Kutokuwepo kwa uzito wa kutosha ndani kulisababisha shida ya uzani (urari) hivyo Kitovu cha mvutano wa ndege (Centre of gravity) kikaelekea nje ya viwango salama.
Kuoata suluhusho, Wahudumu wa ardhini walipakia mifuko ya mchanga kwenye mizigo kama uzito wa ziada ili ndege iweze kupaa kwa usalama.

Licha ya hasara ya mafuta na gharama za uendeshaji, United walichagua kuendelea na safari. Sababu ilikuwa kupeleka ndege na wafanyakazi kwenye kituo kinachofuata kwa ratiba za safari zijazo.

Abiria huyo wa pekee alipata huduma ya daraja la kwanza. Alipokelewa kwa bashasha na matangazo yake yalikuwa maalum, na baada ya kutua salama alialikwa hata ndani ya chumba cha marubani.

Wataalamu wanasema kutumia uzito wa ziada kama mchanga ni utaratibu wa kawaida na salama kabisa katika anga. Hakuna kitu cha kuogopa.
1782912479616.jpg
 
Rais Donald Trump amefanya safari yake ya kwanza leo Julai mosi, 2026, kwa kutumia ndege mpya ya Rais ya Air Force One kusafiri kwenda jimbo la North Dakota.

Ndege hiyo aina ya Boeing 747-8, yenye thamani ya dola milioni 400, ilitolewa kama zawadi kwa serikali ya Marekani kutoka kwa serikali ya Qatar.

Safari hii imefanyika kwa lengo la kwenda kuzindua Maktaba ya Rais ya Theodore Roosevelt ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 250 ya uhuru wa Marekani.

Ndege hii inatumika kama suluhisho la mpito kupunguza mzigo kwa ndege za zamani wakati nchi hiyo ikisubiri ndege zingine mpya kutoka kampuni ya Boeing zinazotarajiwa kukamilika mwaka 2028.

Jeshi la Anga la Marekani lilitumia takriban miezi 10 na chini ya dola milioni 400 kuifanyia ndege hiyo marekebisho makubwa ya kiusalama, ikiwemo kuweka mifumo ya mawasiliano ya siri ya kijeshi na mifumo ya ulinzi dhidi ya mashambulizi.

Muonekano wake wa nje una rangi nyekundu, nyeupe na bluu ya bahari, huku ndani ikiwa imehifadhi mapambo ya kifahari ya kifalme kutoka Qatar ikiwemo samani za dhahabu na viti vya ngozi.

Trump ameeleza kuwa baada ya muhula wake wa uongozi kwisha, ndege hiyo haitakuwa mali yake binafsi bali itapelekwa kwenye maktaba yake ya rais.

Hata hivyo, hatua ya kupokea ndege hiyo kama zawadi kutoka taifa la kigeni imeleta mjadala mkubwa wa kisiasa nchini Marekani.

Wakosoaji kutoka chama cha Democratic wamehoji kuhusu maadili na usalama wa kiidara wa kutumia ndege iliyotoka nchi nyingine.

Kwa upande mwingine, Ikulu ya Marekani na Jeshi la Anga wametetea uamuzi huo wakisisitiza kuwa ndege hiyo imekaguliwa kikamilifu na imesaidia kuokoa mamia ya mamilioni ya dola za walipa kodi.
1782915606062.jpg
 
 
 
Rubani wa helikopta ya Polisi wa New York (NYPD) na waongoza ndege wa uwanja wa LaGuardia walishangazwa na kughafilika baada ya kuona wapandaji wawili juu ya mnara wa Empire State Building, jengo refu zaidi Manhattan, NewYork.

Katika mazungumzo ya sauti yaliyonaswa kutoka mnara wa mawasiliano ya anga, mdhibiti wa usafiri wa anga alisikika akiuliza kwa mshangao, "Kuna vurugu gani gani zinaendelea huko?" huku akitazama mnara huo mashuhuri wa Manhattan.

Rubani wa helikopta ya polisi aliyekuwa akizunguka eneo hilo alijibu kwa kejeli akisema, "Kuna maajabu, watu wawili wamepanda hadi juu kabisa ya mnara wa Empire State Building," huku akiripoti kuwa walikuwa wamebeba bendera na kupepea ujumbe juu ya kilele hicho.

Rubani huyo aliendelea kuwatazama kwa ukaribu kupitia kamera za angani na kushuhudia tukio zima la kihistoria, akithibitisha kwa waongoza ndege kuwa mwanamume alikuwa amepiga magoti na kumvisha pete mwenzake, akisema,

"Wana bendera huko juu waliyokuwa wanapepea, na jamaa ndio kwanza amemposa mwenzake."
1782971411132.jpg
 
Back
Top Bottom