Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,079
- 859,208
- Thread starter
- #981
𝗪𝗔𝗦𝗛𝗜𝗡𝗚𝗧𝗢𝗡 - “Niliziona kundi la droni zikiruka pamoja zikipaa kwa ushirikiano wa hali ya juu, zikibadilika-badilika kama umbo la jellyfish.”
Hayo ni maneno ya rubani wa ndege ya kivita ya Marekani F-15 aliyenusurika baada ya ndege yake kutunguliwa nchini Irani.
Ushuhuda wake sasa umezua mjadala mzito ndani ya idara za kiintelijensia za Marekani kuhusu mabadiliko makubwa ya kiteknolojia ya kijeshi.
Ripoti ya majaribio ya tukio hilo inaonyesha rubani huyo alishuhudia ndege zisizo na rubani nyingi zikiruka kwa mtindo usiotarajiwa, ishara ambayo wataalamu wengi wanasema inaweza kuwa uthibitisho wa teknolojia mpya ya "swarm drones" inayojaribiwa na Irani.
Suala hili limegawa maoni ya maafisa wa usalama nchini Marekani.
Upande mmoja unaamini tukio hilo ni dalili ya maendeleo makubwa ya mifumo ya mtandao na ushirikiano wa droni za jeshi la Irani.
Upande mwingine unatoa tahadhari, ukibainisha kuwa rubani huyo alipata majeraha ya kichwa wakati wa ajali hiyo na hii ilikuwa mara yake ya pili kutunguliwa katika mzo huo unaoendelea.
Tukio hili linajiri wakati Irani ikiendelea kupanua miradi yake ya droni, ikiwemo matumizi ya kambi za siri chini ya ardhi.
Wakati huo huo, Marekani na Tehran ziko kwenye mazungumzo ya kujaribu kusitisha vita vya kikanda.
Wataalamu wa ulinzi wanasema kama ushuhuda wa rubani utathibitishwa kuwa kweli, basi jeshi la Marekani na majeshi mengine duniani yatalazimika kubadilisha mikakati ya kukabiliana na vitisho vipya angani.