Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,100
- 859,269
- Thread starter
- #901
WASHINGTON — NASA imebadili kidogo mpango wa safari yake ya kurejea Mwezini inayoitwa Artemis III.
Safari hiyo iliyipangwa kuzinduliwa mwaka 2027, lakini sasa Chombo hakitatua moja kwa moja Mwezini kama ilivyopangwa awali.
Badala yake, chombo cha angani cha Orion kitazunguka karibu na Dunia kwanza.
Chombo hicho kitarushwa kutoka Florida kwa kutumia roketi kubwa ya Space Launch System.
Kikiwa angani, Orion kitaungana na vyombo vingine vidogo vya kutua Mwezini ambavyo vinatengenezwa na kampuni za SpaceX na Blue Origin.
Wanaanga watakaa ndani ya vyombo hivyo, kukagua jinsi vinavyofanya kazi, kuangalia hewa na mawasiliano. Safari nzima itachukua kama wiki mbili, halafu chombo kitarudi kutua kwa usalama kwenye Bahari ya Pasifiki.
NASA imesema mabadiliko haya ni kwa ajili ya usalama. Wanaona ni bora kupima kila kitu karibu na Dunia kwanza kabla wanaanga hawajasafiri mbali zaidi.
Hii itawasaidia wahandisi kugundua na kutatua matatizo mapema.
Kwa safari hii NASA imechagua wanaanga wanne akiwemo Kamanda Randy Bresnik kutoka Marekani na Luca Parmitano kutoka Ulaya, pamoja na Frank Rubio na Andre Douglas ambao pia ni wa NASA.
Baada ya majaribio haya kukamilika, safari inayofuata ya Artemis IV ndiyo itajaribu kutua rasmi kwenye ncha ya kusini ya Mwezi.