Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Ndege ya Virgin Atlantic (Flight VS165) ililazimika kugeuza safari na kurudi uwanja wa ndege wa Shannon nchini Ireland mapema juzi baada ya moja ya injini zake kushindwa kufanya kazi ndege ikiwa juu ya Bahari ya Atlantiki.

Ndege hiyo aina ya Airbus A330-900neo iliondoka uwanja wa Heathrow London tarehe 30 Mei 2026 ikiwa na abiria 246 na wafanyakazi 13, ikielekea Montego Bay, Jamaica.

Masaa Matatu baada ya kuruka, ikiwa urefu wa futi 34,000, rubani aliripoti hitilafu kwenye injini ya kulia aina ya Rolls-Royce Trent 7000.
Kwa kufuata taratibu za dharura, marubani walizima injini hiyo na kuendelea kuruka kwa injini moja tu juu ya bahari.

Ndege hiyo ilishuka hadi futi 20,000 kisha ikaelekezwa uwanja wa ndege wa Shannon ambako timu za dharura zilikuwa tayari zimesimama, zikiwemo gari za wagonjwa, zima moto, polisi, walinzi wa pwani na hata boti ya uokoaji ya RNLI.

Licha ya hali ya kusisimua, ndege hiyo ilitua salama muda wa jioni na watu wote 259 ndani yake walitoka salama.

Tukio hilo linaonyesha jinsi ndege za kisasa za abiria zinavyoweza kuruka salama kwa injini moja, na ujuzi wa marubani katika kudhibiti dharura angani.
1780338696644.jpg
 
Ndege ya kujazia mafuta angani ya Marekani aina ya KC-135R kutoka kikosi cha Alaska Air National Guard 168th Wing ililrudi nyumbani ikiwa na matundu na viraka ya matengenezo ya muda baada ya kupata uharibifu mkubwa wakati wa Operation Epic Fury ya iliyoendeshwa na Israel na Marekani dhidi ya Irani.

Hii ni ndege ya pili ya aina hiyo kurudi ikiwa na madhara kutoka operesheni hiyo, hivyo kuonyesha hatari zinazokabili ndege za kutoa msaada angani.

Bomba lake la kujazia mafuta ilionekana kuondolewa kabla ya safari ndefu ya kuvuka bahari ya Atlantiki.

Ndege hiyo sasa itakaguliwa katika kituo cha Tinker Air Force Base, Oklahoma ili kuamuliwa kama itatengenezwa au kutumika kama vipuri.
1780398570679.jpg
 
Ndege mbili za Airbus A320neo ambazo bado hazijazeeka, zikiwa na umri wa miaka mitatu tu, sasa zinavunjwa kuwa vipuri kwa sababu zisizo za kawaida.

Thamani ya vipuri vyake zote pamoja ni kubwa zaidi kuliko thamani ya ndege nzima ikiwa imekamilika.

Uamuzi huu wa kubomoa ndege hizo unasababishwa na upungufu mkubwa wa injini duniani kote.

Ndege hizo zinatumia injini za Pratt & Whitney GTF ambazo zilikumbwa na janga kubwa la kimataifa baada ya kugundulika kuwa na vumbi la chuma lisilo safi kwenye sehemu muhimu ndani ya injini husika.

Kwa sasa mamia ya ndege zimesimamishwa kwa sababu injini zinasubiri ukarabati ambao unachukua hadi miezi 10.

Hali hiyo imefanya injini na vipuri vinavyofanya kazi kuwa na thamani kubwa sana, huku injini moja tu ikithaminiwa kati ya dola milioni 20 hadi 22.

Mfumo wa usambazaji vipuri kutoka viwandani umesimama, hivyo mashirika ya ndege yanapendelea kununua vipuri vilivyotumika lakini vinafanya kazi badala ya kusubiri miezi mingi kutoka kwa msambazaji kiwandani.

Pia baadhi ya mashirika kama Spirit Airlines yamepata matatizo ya kifedha na kurejesha ndege zilizokodiwa kwa wamiliki.

Wamiliki hao wanagundua ni faida zaidi kuvuna injini na vipuri ambavyo havijatumika sana badala ya kutafuta waendeshaji wapya.

Kwa hiyo kuikata ndege yenye umri wa miaka mitatu imekuwa uamuzi wa kiuchumi unaolenga kutoa vipuri vinavyohitajika sana na kutatua msongamano wa usambazaji.

Hali hii inaonyesha jinsi sekta ya anga inavyolazimika kufanya maamuzi magumu ili ndege nyingine ziendelee kuruka.
1780563309050.jpg
 
Ndege ya Airbus A350-1000ULR (Utra Long Range) ambayo ni ya masafa marefu zaidi duniani imefanikiwa kufanya jaribio lake la kwanza angani kwa kuruka kwa saa 3 na dakika 43 kwenye kimo cha futi 41,000.

Jaribio hilo la kwanza la kuruka la Airbus A350-1000ULR lilifanyika Toulouse, Ufaransa, siku ya jumanne Juni 02, 2026 kutoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Toulouse-Blagnac TLS

Ndege hiyo inatengenezwa mahsusi kwa Shirika la Ndege la Qantas Airways ili kuwezesha safari za moja kwa moja kati ya Sydney na London kwa mara ya kwanza kabisa, umbali wa takriban maili 10,000 za bahari na muda wa kuruka hadi saa 22 bila kutua.

Uwezo wa masafa ya ndege hii wa kuruka umbali wa kilomita 17,964 pasipo kituo umewezekana kwa sababu ya kuingizwa kwa tanki la ziada la mafuta upande wa nyuma katikati ya muundo wa ndege unaoitwa Rear Centre Tank (RCT).

Tanki hilo limeongeza utendaji wa ndege na kupanua masafa yake kwa maili 1,000 zaidi ya Airbus A350-1000 ya kawaida.

Mradi huu unalenga kuibadilisha kabisa dhana ya safari za ndege za masafa marefu na kuunganisha moja kwa moja Australia na Ulaya bila kupita nchi za kati.
1780568803108.jpg
 
Ndege binafsi ya Sean "Diddy" Combs aina ya Gulfstream G550 yenye rangi nyeusi ya matte imeuzwa na kubadilishwa usajili kwa sababu ya kile kilichotajwa kutumikia kifungo cha miezi 50 jela ya shirikisho.

Muasisi huyo wa muziki aliyefungwa kwa mashtaka ya uhalifu wa uasherati alikamilisha rasmi mauzo ya ndege hiyo Oktoba 2025 na kubadilisha umiliki, na hivyo kiwa sehemu ya mauuzo ya mali kubwa baada ya kuhukumiwa.

Kabla haijauzwa, ndege hiyo ilikuwa na usajili namba N1969C chini ya LoveAir LLC sasa imesajiliwa kwa namba mpya ya T7-OKS na inaonekana kuruka katika mjini wa San Marino.

Ndege hiyo binafsi ya Gulfstream G550 ilikuwa ikitumika kumwingizia mamilioni ya dola kupitia ukodishaji wakati akiwa kizuizini.
1780666053969.jpg
 
Ripoti ya awali ya Bodi ya kitaifa ya uchunguzi wa ajali ya Marekani (NTSB) imeeleza kuwa tarehe 3 Mei 2026 ndege ya United Airlines Boeing 767-424ER (UA169) iligonga nguzo ya taa ya barabarani huko New Jersey Turnpike wakati ikikaribia kutua njia ya kutua ndege namba 29, katika uwanja wa ndege wa Newark Liberty.

Nahodha (Captain) aliamua kuruka chini ya mteremko wa kawaida kwa kusoma "3 red 1 white" kwenye taa za njia ya kuongoza ndege kutua (PAPI) badala ya kudhibiti ndege ili kusoma taa za "2 red 2 white" katika urefu sahihi wa kutua salama.

Lakini hakuujadili mpango huo na afisa msaidizi. Afisa msaidizi aligundua ndege ikienda polepole na chini akatoa onyo "airspeed slow" na "you are still low" sekunde za mwisho, hata hivyo rubani hakuwa na muda wa kusitisha kutua (go-around).

Ingawa ndege ilitua salama lakini gurudumu za ndege na chini ya bodi iligonga nguzo ya taa ambayo nayo iligonga lori.

Ukaguzi ulionyesha mashimo matatu kwenye fuselage ya chini kushoto, kubwa likiwa inchi 46 x 4.
Baada ya tukio, shirika la United Airlines ilitoa Pilot Bulletin 26-069 ikionya marubani dhidi ya tabia ya kuruka nje kanuni "ducking under" wakati wa kutua kwa kuona.
1780670771692.jpg
 
Ndege ya shirika la Lufthansa aina ya Boeing 787-9 imepata uharibifu mkubwa leo Frankfurt baada ya gurudumu lake la mbele kutenguka wakati ikiwa imeegeshwa kwenye geti.

Ndege hiyo yenye usajili D-ABPQ, yenye umri wa mwaka mmoja ilikuwa imepangwa kuendesha safari namba LH450 kutoka Frankfurt kuelekea Los Angeles.

Kufuatia ajali hiyo safari imeghairiwa mara moja. Tukio hilo limezua maswali kuhusu hali ya kiufundi ya ndege mpya, ingawa uchunguzi kamili wa sababu ya kuporomoka kwa gurudumu la mbele bado unaendelea.

Hakuna taarifa ya majeraha kwa abiria au wafanyakazi kwa kuwa tukio lilitokea ndege ikiwa bado haijapakia abiria.

Lufthansa bado haijatoa maelezo kamili kuhusu athari za uendeshaji au muda gani ndege hiyo itakaa nje ya huduma kwa ajili ya ukarabati.
1780673158700.jpg
 
Ndege mbili mpya kabisa za Riyadh Air, Boeing 787-9 Dreamliner zenye usajili HZ-RXAA na HZ-RXAB, zimewasili nchini Saudi Arabia leo katika safari ya uwasilishaji.

Ndege hizo zilipokelewa kwa heshima kubwa zikiandamana na ndege za kikosi maalum cha anga cha Saudi Arabia, Saudi Hawks, zilizofanya doria ya heshima angani wakati wa kutua.

Kuongezeka kwa Dreamliner hizo ni sehemu ya mpango wa Riyadh Air kupanua huduma zake na kuimarisha hadhi yake kama shirika jipya la kimataifa kutoka Ufalme wa Saudi Arabia.
1780714526022.jpg
 
NASA waliacha waliacha matumizi ya penseli na kuanza kutumia “kalamu ya anga” maarufu kama "Fisher Space Pen" si kwa sababu walitaka kutumia pesa nyingi bure, bali kwa sababu penseli iligeuka kuwa hatari kubwa kwa maisha ya wanaanga na vyombo vya anga.

Penseli zina mbao na graphite ambazo zinawaka moto haraka sana. Vituo vya anga vya awali vilikuwa na oksijeni safi "Pure Oxygen" asilimia 100% ndani yake, hivyo cheche ndogo tu ingeweza kusababisha moto mkubwa kama ule wa Apollo 1.

Pia graphite ni kielezo cha umeme. Kipande kidogo cha ncha ya penseli kinachovunjika na kuelea bila uzito kinaweza kuingia kwenye bodi za saketi na kupiga shoti mifumo muhimu ya ndege. Vipande vya mbao na graphite vikiingia machoni au pua za wanaanga pia vilikuwa hatari.

NASA hata ilijaribu kutumia penseli za mitambo zilizotengenezwa maalum kwa NASA kwa dola 128 kila moja. Lakini zilivunjika mara kwa mara, zikatoa uchafu mwingi unaoelea, na hazikutatua tatizo la moto na umeme.

Hapo ndipo mvumbuzi Paul C. Fisher alipoingilia kati kwa pesa zake binafsi. Alitumia takriban dola milioni 1 kutoka mfukoni mwake kutengeneza Fisher Space Pen.

Kalamu hiyo ina wino uliofungwa kwenye cartridge yenye shinikizo la gesi ya nitrojeni, hivyo inaandika bila kujali mvuto wa dunia (gravity) hata ikiwa kichwa chini, ndani ya maji, au kwenye halijoto kuanzia -46°C hadi 71°C.

NASA walipojaribu kalamu hiyo na kuona inatatua hatari zote za penseli, walianza kuagiza. Gharama yake kwa NASA ilikuwa dola 6 tu kwa kila kalamu, si mamilioni. Hadithi ya “NASA walitumia mamilioni” si kweli. Ni Fisher mwenyewe aliyetumia mamilioni yake binafsi kabla hata NASA kuanza kununua.

Urusi walipoona usalama wake, nao wakaanza kuitumia 1969 na mpaka leo bado ni peni rasmi ya wanaanga wote.
1780757660013.jpg
 
Mwanamuziki nyota wa Marekani Lil Wayne amejijengea falsafa tofauti kabisa kuhusu umiliki wa ndege binafsi ambapo kwa miaka mingi amesimama kwenye msimamo mmoja, kukodi, na si kununua.

Rapa huyo amesema wazi kuwa anaweza kumudu kununua ndege yake binafsi, lakini anachagua kutofanya hivyo ili asije akafilisika.

Kwa mtazamo wake, watu wengi hasa wanamuziki hupoteza pesa nyingi kujaribu kujipamba na kujionyesha, jambo ambalo yeye huliita “mtego wa kuiga wengine”.

Lil Wayne anasema wazi kuwa anachoogopa zaidi ni kufika mwisho wa umaarufu bila pesa mfukoni.

"Kwa sababu katika tasnia ya muziki, umaarufu hupanda na kushuka najua hakuna mtu atakayenijia kuniokoa pale nitakapomaliza pesa zangu baada ya nyota kufifia na ndiyo maana nimekuwa nikiepuka umiliki wa ndege binafsi kama vile matengenezo, marubani, bima, na gharama za maegesho na karakana"
Alisema Lil Wayne.

Mara nyingi Lil Wayne hutumia ndege za kukodi na hata hivyo mtindo huo umewahi kumwingiza kwenye matatizo ya kisheria mara kadhaa.
Kampuni ya kukodi ndege ya Signature Group ilimfikisha mahakamani kwa madai ya kukosa kulipa kodi ya ndege iliyofikia mamia ya maelfu ya dola.

Licha ya msimamo huu wa muda mrefu wa “no purchase”, sasa kumetokea uvumi mpya mtandaoni na kwenye ripoti za sekta ya anga.
Baadhi ya vyanzo vinaeleza kwamba Lil Wayne hivi karibuni amenunua ndege ya kifahari aina ya Bombardier Global 7500 yenye thamani ya dola milioni 78.

Hadi sasa Lil Wayne hajatoa uthibitisho rasmi kuhusu ununuzi huo.
 
Majira ya joto mnamo mwaka 1983, ndege ya Air Canada (Flight 143) aina ya Boeing 767 ilikaribia kuanguka kutoka angani kwa sababu ya kosa dogo la kihesabu.

Canada ilikuwa imebadilika kutumia mfumo wa metriki na hii Boeing 767 ilikuwa ndege ya kwanza kutumia kipimo cha kilogramu badala ya paundi katika ujazaji mafuta.

Mmoja wa wafanyakazi wa chini alikosea kubadilisha hesabu wakati wa kujaza mafuta baada ya kutumia kipimo cha paundi badala ya kilogramu hivyo ndege kupaa ikiwa na mafuta nusu tu ya yale yaliyohitajika kwa safari.

Ikiwa Nusu ya safari angani injini zikaanza kukosa mafuta na kuzima.
Ndege hiyo ya tani 100 ikageuka kuwa moja ya ndege kubwa isiyo na injini kuwahi kuelea angani (Giant Heavy Glider).

Bahati nzuri, Nahodha, "Captain" Robert Pearson alikuwa rubani mzuri wa ndege ndogo zisizo na injini (Glider) hivyo kutumia mbinu za ndege hiyo ndogo kuteremsha Boeing 767 kwa zaidi ya maili 72 bila injini.

Pearson alilenga uwanja wa kijeshi uliotelekezwa huko Gimli, Manitoba lakini kwa bahati mbaya ni kwamba, siku hiyo ilikuwa 'Family Day' na uwanja huo uligeuzwa kuwa uwanja wa michezo ya watoto na mbio za vigari.

Hata hivyo Pearson aliteremsha dubwasha hilo zito lisilo na Honi kimya kimya na kwa hesabu kubwa akitumia ujanja tofauti tofauti unaotumika kurusha ndege ya 'glider', kuelekea kwenye uwanja huo.

Kwa bahati nzuri baadhi ya watu waliweza kuona ndege hiyo iliteremka kuelekea walipo kimya kimya na kuanza kutawanyika pembeni.

Mara baada ya kutua gurudumu la mbele likavunjika na ndege ikateleza kwenye njia ikizalisha moshi na cheche.

Kwa bahati nzuri mwishowe ikaishia mita chache tu kutoka kwenye umati ulipojikusanya na kwa miujiza hakuna mtu aliyejeruhiwa vibaya.

Tukio hilo lilibaki katika historia kama "Gimli Glider" na video za tukio hilo zinapatikana mtandaoni kwa jina hilo.
1780835164729.jpg
 
Ndege Hujazwa Vipi Mafuta How Are Airplane Refueled
Kwanza, timu ya mafuta hukagua ubora wa mafuta ya Jet A-1 kuhakikisha hayana maji wala uchafu.

How Is Fuel Loaded Into An Aircraft? Discover The Airplane Refueling Process!

#HowAreAirplaneRefueled #viralvideoシ #aviation #tanzania #usa


View: https://www.facebook.com/share/v/1D2vM4xyyE/
 
KAMPALA, UGANDA – Rais Yoweri Museveni amezindua rasmi ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kidepo katika eneo la Karamoja, mradi mkubwa unaogharimu dola milioni 150 za Kimarekani.

Mradi huu unatekelezwa chini ya ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi kati ya serikali ya Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Uwanja huo unajengwa kwa kushirikiana na Chemba ya Biashara na Viwanda ya Sharjah kutoka UAE, hatua inayofuatia makubaliano yaliyotiwa saini mwezi Juni 2024 yenye lengo la kufungua fursa za kiuchumi kaskazini-mashariki mwa Uganda.

Kwa upande wa viwango, uwanja utakuwa na hadhi ya “4E” sawa na Uwanja wa Kimataifa wa Entebbe na utajengwa na barabara ya ndege yenye urefu wa kilomita 3.5 inayoweza kupokea ndege kubwa za abiria na mizigo kama Boeing 777.
Awamu ya kwanza ya maandalizi tayari imetoa ajira kwa Waganda zaidi ya 1,600.

Kwa nyanja ya kiuchumi, uwanja huu unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa kutoa njia ya mkato kwa watalii wa kimataifa kufika moja kwa moja kwenye Mbuga ya Kitaifa ya Kidepo Valley ambayo imekuwa vigumu kufikiwa kwa barabara.

Pia Karamoja ina utajiri mkubwa wa madini kama dhahabu, marumaru, nikeli na chokaa, hivyo uwanja huu utarahisisha usafirishaji wa bidhaa hizo kwenda masoko ya ndani na nje.

Zaidi ya hapo, utafanya kazi kama kitovu cha vifaa kwa nchi jirani za Sudan Kusini na Kenya, na hivyo kuimarisha biashara ya kikanda.
1780839529341.jpg
 
Ndege kubwa isiyo na rubani "Drone" ya kijeshi ya China imegundulika ikituma ishara za kujitambulisha kama ndege ya kivita ya Uingereza aina ya Eurofighter Typhoon.

Tukio hilo lilitokea karibu na Kisiwa cha Hainan kwenye Bahari ya China Kusini, ambapo "Drone" hiyo ilituma nambari halisi ya ndege ya RAF ikiwa ni ZK334 na 'callsign' ya YILO2400.
Mifumo ya ufuatiliaji kama Flightradar24 ilionyesha ishara hiyo.

Wachambuzi wa anga walibaini udanganyifu huo kwa haraka kwa kizingatia sababu tatu.

Ya Kwanza, hakukuwa na ndege za kivita za Uingereza zilizokuwa zikifanya mazoezi eneo hilo.

Pili, droni hiyo iliruka kwa kasi ya chini na urefu mdogo, tabia inayofanywa na 'drone' ya doria na siyo ndege ya kijeshi ya mwendokasi (supersonic fighter jet).

Tatu, ilizunguka eneo linalotumiwa na jeshi la PLA kabla ya kutua kwenye kituo cha ndege zisizo na rubani za China Hainan.

Wataalamu wanasema hii ni majaribio ya vita vya kielektroniki.
Kwa kubadilisha ishara za ADS-B, China inajaribu kuchanganya radar na mifumo ya ulinzi wa nchi adui.

Mbinu hii ikiifanikiwa inaweza kuficha harakati halisi za kijeshi na kuchelewesha majibu wakati wa mgogoro.

Ripoti zinaonyesha droni hiyo imewahi kuiga pia ndege ya mizigo ya Belarus iliyowekewa vikwazo hapo awali.
1780855543302.jpg
 
Timu ya taifa ya Irani ya Kombe la Dunia 2026 imewasili na ndege karibu kabisa na mipaka ya Marekani, lakini bado haijaingia rasmi ndani ya nchi hiyo.

Kulingana na taarifa zilizotoka, ndege iliyobeba wachezaji ilitua umbali wa mita chache kutoka eneo la Marekani, lakini ikasimama kabla ya timu hiyo kuingia rasmi.

Tukio hilo limezua hisia mchanganyiko kwa sababu Irani na Marekani zina uhusiano mgumu wa kisiasa.

Hata hivyo kwa upande wa soka, Kombe la Dunia 2026 litafanyika kwa pamoja Marekani, Mexico na Canada, hivyo timu zote zilizofuzu zitalazimika kuingia Marekani wakati wa mashindano.

Wachezaji wa Irani kwa sasa wanasubiri taratibu za uhamiaji na kibali maalumu kabla ya kuingia nchini humo.

FIFA na mashirika husika wanasema mchakato unaendelea ili kuhakikisha timu zote zinapata haki sawa ya kushiriki mashindano bila vikwazo vya kisiasa.
1780887932791.jpg
 
NEW DELHI – Ndege tatu za abiria za shirika la Air India zilizokuwa zimeegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi zimepata uharibifu mkubwa kufuatia dhoruba ya ghafla iliyovivuruga vifaa vya kutoa huduma za ardhini.

Tukio hilo limetokea mnamo majira ya saa 10 jioni ya Jumapili katika maeneo ya maegesho ya Terminal 2, ambapo mvua kubwa na upepo mkali usiotabiriwa ulivuma katika uwanja huo bila ya kuwepo kwa tahadhari yoyote kutoka kwa mamlaka za utabiri wa hali ya hewa.

Kutokana na kasi ya upepo huo, ngazi ya kupandia abiria na jukwaa la matengenezo vinavyomilikiwa na kampuni za uandisi wa ndege vilichomoka mahali vilipofungwa na kwenda kwa kasi kuzigonga ndege hizo tatu aina ya Airbus A320 zilizokuwa zimeegeshwa.

Mamlaka za uwanja wa ndege zimethibitisha kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika tukio hilo, kwani hakukuwa na abiria wala wafanyakazi ndani ya ndege hizo wala karibu na eneo la ajali wakati dhoruba hiyo ikitokea.

Hata hivyo, ndege zote tatu zimeondolewa mara moja kwenye ratiba za safari kwa ajili ya ukaguzi na matengenezo ya kiufundi ambapo ndege mbili zimepata uharibifu mdogo na zinatarajiwa kurejea angani baada ya siku chache huku ya tatu ikisalia aridhini kwa matengenezo ya muda mrefu kutokana na uharibifu mkubwa wa kimuundo.

Wakati huo huo, Mamlaka Kuu ya Usafiri wa Anga nchini India inatarajiwa kuanzisha uchunguzi rasmi ili kubaini kama kulikuwa na uzembe wa ufungaji wa vifaa hivyo vya aridhini wakati wa mabadiliko ya hali ya hewa.
1780899907722.jpg
 
Back
Top Bottom