Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

π—‘π—šπ—˜π—Ÿπ—˜, 𝗝𝗔𝗠𝗛𝗨π—₯π—œ 𝗬𝗔 π——π—’π— π—œπ—‘π—œπ—žπ—”π—‘π—œ - Rubani kiongozi na msaidizi wake wamefariki dunia baada ya ndege binafsi ya kifahari aina ya Gulfstream G200 kuanguka na kulipuka wakati ikijaribu kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa La Romana nchini Jamhuri ya Dominika.

Ndege hiyo yenye usajili wa Marekani (N318JF), inayomilikiwa na kampuni ya Aibonito Aviation LLC, ilikuwa ikisafiri kutoka La Romana kuelekea mji wa Austin uliopo jimboni Texas, Marekani.

Muda mfupi baada ya kuruka, marubani waliripoti dharura kutokana na matatizo makubwa ya kiufundi yanayosadikiwa kuwa ni hitilafu ya injini na kupoteza nguvu za ndege.

Wakati wakijaribu kugeuka na kurudi uwanjani huku wakikabiliana na hali ngumu, ndege hiyo ilipoteza utulivu wakati wa kushuka, ikaacha njia baada ya kutua kwa nguvu na kulipuka kwa kishindo kikubwa kwenye eneo la nyasi pembezoni mwa uwanja huo.

Mamlaka za usalama zimeshafanikiwa kuwatambua marubani waliopoteza maisha kuwa ni Erick Javier Diago na Rudy Ghazal, huku ikithibitishwa kuwa hapakuwa na abiria mwingine yeyote ndani ya ndege hiyo.

Kwa sasa, Taasisi ya Usafiri wa Anga ya Jamhuri ya Dominika (IDAC) ikishirikiana na Tume ya Uchunguzi wa Ajali za Ndege (CIAA) zimeanza rasmi uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha hitilafu hiyo ya kiufundi iliyosababisha maafa hayo makubwa.
1780900468113.jpg
 
Shirika la ndeege la Riyadh Air limepokea rasmi ndege zake mbili za kwanza aina ya Boeing 787-9 Dreamliner kwenye Uwanja wa King Khalid International, Riyadh.
Kuja kwa ndege hizo ni hatua kubwa kwa shirika jipya la Saudi Arabia linalojiandaa kuanza safari za kibiashara.

Ndege hizo za Dreamliner za kizazi kipya zimeundwa kwa starehe zaidi, matumizi ya mafuta kidogo, na uwezo wa kuruka masafa marefu bila kuacha ubora.

Kwa Riyadh Air zitaifanya Saudi Arabia iunganike kwa urahisi na miji mikuu duniani huku ikitoa uzoefu mpya wa usafiri wa hadhi ya juu.

Ndege hizo zilisindikizwa na ndege za kijeshi za Saudia wakati zikiwasili.

Wadau wanasema kuwa, kuwasili kwa ndege hizo za B787siyo tu ongezeko la ndege, bali ni ishara ya azma mpya ya tasnia ya anga ya Saudi ya kisasa, yenye malengo makubwa, na wazi kwa ulimwengu.
1780907516328.jpg
 
HOLLYWOOD: Mwigizaji maarufu na mshindi wa tuzo ya Oscar, Morgan Freeman, alithibitisha kuwa umri ni namba tu mara baada ya kufanikiwa kupata leseni yake ya urubani wa ndege binafsi wakati akiwa na umri wa miaka 65

Freeman, ambaye tangu ujana wake alitamani kuwa rubani wa ndege za kivita, alijiunga na Jeshi la Anga la Marekani (US Air Force) mwaka 1955.

Hata hivyo, katika kipindi hicho alihudumu kama fundi wa rada kabla ya kuacha jeshi hilo na kuingia kwenye uigizaji.

Ndoto hiyo ilikuja kutimia rasmi mwaka 2002 baada ya kufanya mafunzo na kufanikiwa kufanya urubani wa ndege mbalimbali za kifahari zikiwemo Cessna Citation na Emivest SJ30.

Hata hivyo, kutokana na ajali mbaya ya gari aliyopata mwaka 2008 iliyomsababishia uharibifu wa neva mkononi, Freeman kwa sasa hawezi tena kupita vigezo vya afya vinavyomruhusu kurusha ndege peke yake.

Licha ya changamoto hiyo, bado anaendelea kufurahia mapenzi yake ya anga kwa kuruka akisindikizwa na rubani msaidizi (co-pilot).
1780944095634.jpg
 
Aliyekuwa Nahodha wa Air Canada, Geoffrey Wall mwenye umri wa miaka 59, amefunguliwa mashtaka ya kitapeli baada ya Jeshi la Polisi la Peel nchini Kanada kubaini kuwa alisafiri kwa zaidi ya safari 900 za ndege akitumia leseni ya kughushi ya urubani wa usafirishaji wa anga ATPL.

Wall alifanya kazi Air Canada kwa miaka 27 na wakati wote huo alikuwa akiongoza ndege kubwa za abiria aina ya Boeing 767, 777 na 787 kama rubani mkuu.

Licha ya kuhudumia maelfu ya abiria, anashukiwa kuwa hakuwahi kufanya wala kufaulu mitihani ya kupata leseni ya juu inayomruhusu kisheria kuwa nahodha wa ndege hizo.

Polisi walisema ilibainika kuwa Jeffrey Wall, mwenye umri wa miaka 59 kutoka Ontario, alikuwa akirusha ndege kwa kutumia vyeti bandia tangu alipopandishwa cheo kuwa rubani mwaka 2009, na sasa anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya ulaghai.

Udanganyifu huo ulikuja kubainika wakati wa tathmini ya kawaida ya kiutendaji iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toronto Pearson.

Kufuatia uchunguzi, mtuhumiwa sasa anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya kijinai ikiwa ni pamoja na utapeli wa kiwango kinachozidi $5,000 na kutoa nyaraka za kughushi.

Geoffrey Wall amepangiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya Brampton mnamo Juni 29 kujibu mashtaka yanayomkabili.
1781078791846.jpg
 
Ndege ya Kenya Airways aina ya Boeing 707 yenye nambari 5Y-BBK ilionekana kuegeshwa kwa muda mrefu pembezoni katika Uwanja wa Ndege wa Bole Addis Ababa ambayo mara nyingi ilisemekana kuwa "imetelekezwa”.

Lakini kulingana na kumbukumbu za anga, ndege hiyo haikuachwa bali iliandikwa kuwa haifai kutumika tena baada ya ajali.

Tukio hilo lilitokea Julai 11, 1989 wakati ndege hiyo iliposhindwa kusimama baada ya kutua kutokana na hitilafu ya mfumo wa magurudumu ya kutua ambapo iliacha njia ya kutua na kuharibika vibaya.
Kwa bahati nzuri abiria wote pamoja na wafanyakazi wa ndege walinusurika bila majeraha makubwa.

Baada ya ajali hiyo ndege haikuruka tena na tangu wakati huo imekuwa imekaa katika eneo la uwanja wa Bole.

Hali yake ya kuonekana kutelekezwa imetengeneza hadithi nyingi mtandaoni, lakini ukweli ni kuwa ilitolewa rasmi kwenye matumizi baada ya uharibifu wa Julai 1989 na haikuweza kurekebishwa kurudi angani.
1781090261988.jpg
 
WASHINGTON – Serikali ya Marekani imethibitisha kuwa helikopta yake ya kisasa ya kijeshi aina ya AH-64 Apache iliangushwa katika Mlango-bahari wa Hormuz baada ya kugongwa angani na ndege isyo na rubani 'drone' ya mashambulizi ya Irani aina ya Shahed.

Tukio hili lisilo la kawaida limezua maswali mengi ya kiusalama kwani ndege hizo zisizo na rubani za gharama nafuu kwa kawaida hazitengenezwi kwa ajili ya mapambano ya angani dhidi ya ndege au helikopta zenye ulinzi mkubwa kama Apache.

Wachunguzi wa kijeshi bado wanajaribu kubaini iwapo 'drone' hiyo ililenga helikopta hiyo kimakusudi au kama lilikuwa mgongano wa bahati mbaya wakati ndege hiyo siyo na rubani ikipita katika anga hilo.

Helikopta ya Apache ilikuwa kwenye doria za kawaida karibu na pwani ya Oman wakati shambulio hilo lilipotokea na kusababisha Helikopta hiyo kuangukea baharini.

Licha ya ajali hiyo, marubani wote wawili walinusurika bila majeraha makubwa na waliokolewa kwa mafanikio ndani ya saa mbili na boti ya kisasa isiyo na rubani ya Jeshi la Majini la Marekani, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe kuokoa wanajeshi vitani.

Kufuatia tukio hilo, Rais Donald Trump na Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani waliamuru mashambulizi ya kuliza kisasi ambapo ndege za kivita zilishambulia mifumo ya ulinzi wa anga, rada, na sehemu ya vituo vya kuongozea ndege zisizo na rubani vya nchini Irani.
1781158946004.jpg
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Nigeria (NCAA) imezuia ndege moja ya kibinafsi aina ya Canadair CL-600 Challenger baada ya kutua kwa dharura na kisha kupaa kinyume cha sheria kutoka kwenye barabara kuu katika jimbo la Delta.

Tukio hilo lilitokea mnamo Juni 10, 2026, pale ndege hiyo yenye namba za usajili N989BC iliposhindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Asaba kutokana na changamoto za kiufundi, hali iliyowalazimu marubani kuishusha ndege hiyo katikati ya barabara kuu ya Ogwashi-Uku.

Watu wote wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo walitoka salama bila majeraha yoyote.
Saa chache baada ya kutua huko, marubani wa ndege hiyo waliamua kuwasha injini na kupaa tena kutokea barabarani kuelekea jiji la Lagos bila kupata kibali kutoka kwa mamlaka za udhibiti wala kuwajulisha waongoza ndege.

Hatua hiyo ilisababisha sintofahamu kubwa na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara na anga.

Mara tu ndege hiyo ilipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Murtala Muhammed mjini Lagos, maafisa wa usalama waliizingira na kuishikilia.

NCAA imesitisha leseni ya uendeshaji ya mmiliki wa ndege hiyo na kuweka vyeti vya marubani husika chini ya uchunguzi mkali, huku Idara ya Uchunguzi wa Usalama wa Usafiri (NSIB) ikianza uchunguzi rasmi kubaini chanzo cha dharura hiyo na ukiukwaji huo mkubwa wa sheria za anga.
1781172135015.jpg
 
𝗦𝗨𝗠𝗕𝗔π—ͺπ—”π—‘π—šπ—”, π—₯π—¨π—žπ—ͺ𝗔 - Mkoa wa Rukwa umeingia katika historia mpya ya usafirishaji baada ya Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga kupokea ndege ya kwanza ya kibiashara Juni 10, 2026.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa maboresho makubwa ya miundombinu ya uwanja huo yaliyokamilika mwezi Aprili mwaka huu, na kufungua rasmi milango ya usafiri wa anga kwa mkoa huo.

Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL), ndilo lililozindua safari hizo kwa kutumia ndege yake aina ya De Havilland Canada Dash 8 Q400.

Ndege hiyo ilitua uwanjani hapo asubuhi na kulakiwa kwa shangwe kutoka kwa viongozi wa serikali na mamia ya wakazi wa Sumbawanga waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Serikali imeeleza kuwa kuanza kwa safari hizi ni ukombozi mkubwa wa kiuchumi kwa ukanda wa nyororo za uzalishaji za Rukwa na mikoa jirani.

Usafiri huo wa anga unatarajiwa kurahisisha kwa kiasi kikubwa harakati za kibiashara, kuongeza uwekezaji, na kuchochea sekta ya utalii kwa kuunganisha mkoa huo na soko kuu la Dar es Salaam pamoja na mikoa mingine nchini.

Katika awamu hii ya kwanza, shirika hilo limepanga kufanya safari zake mara mbili kwa wiki, yaani kila siku ya Jumatano na Jumapili.

Ratiba inaonyesha kuwa ndege hiyo itaondoka Dar es Salaam saa 11:00 alfajiri na kuwasili Sumbawanga saa 1:30 asubuhi, kabla ya kurejea Dar es Salaam kupitia Tabora kuanzia saa 3:40 asubuhi.

Ili kuvutia wasafiri wengi zaidi, shirika hilo limetangaza ofa ya nauli ya shilingi 200,000 kwa safari ya upande mmoja na shilingi 350,000 kwa safari ya kwenda na kurudi.
1781252410920.jpg
 
π—Ÿπ—”π—šπ—’π—¦, π—‘π—œπ—šπ—˜π—₯π—œπ—” - Mwenyekiti wa kampuni ya BUA Group na bilionea wa pili kwa utajiri barani Afrika, Abdul Samad Rabiu, amepokea rasmi ndege mpya ya kifahari aina ya Bombardier Global 8000 yenye thamani ya takriban dola milioni 81 za Kimarekani, ambazo ni sawa na karibu naira bilioni 110.

Hatua hii imethibitishwa kufuatia taarifa zilizochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ikionyesha kuwa mkataba wa manunuzi ya ndege hiyo ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2025 jijini Dubai.

Ununuzi huu unamfanya mfanyabiashara huyo kuwa miongoni mwa Waafrika wa kwanza kabisa kumiliki ndege hii ya kisasa, ambayo kwa sasa inatambulika kama ndege ya kiraia yenye kasi zaidi duniani tangu zama za ndege ya Concorde.

Ndege hii mpya yenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu bila kusama njiani inaungana na ndege nyingine mbili za kifahari zinazomilikiwa na kampuni hiyo, zikiwemo Bombardier Challenger 350 na Bombardier Global 6500, lengo likiwa ni kurahisisha safari za kibiashara na upanuzi wa miradi ya BUA Group kimataifa.

Ukuaji huu wa usafiri wa anga wa kampuni hiyo unaenda sambamba na ongezeko kubwa la utajiri wa Abdul Samad Rabiu, ambao umeongezeka kwa asilimia 120% na kufikia dola bilioni 11.2 ifikapo mwaka 2026.

Ongezeko hili kubwa la utajiri linatajwa kuwa ndilo kubwa zaidi kurekodiwa barani Afrika kwa mwaka huu, likichochewa zaidi na mafanikio makubwa ya biashara zake za uzalishaji wa saruji, sukari, miundombinu, pamoja na uwekezaji mkubwa katika sekta ya nishati na usafishaji wa mafuta.
1781311107588.jpg
 
Back
Top Bottom