Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,100
- 859,274
- Thread starter
- #841
FARO - Mamlaka za Ureno zimetangaza kukamatwa rasmi kwa ndege aina ya Boeing 727-100 inayomilikiwa na Jean-Pierre Bemba, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kukamatwa huko kunafanyika chini ya operesheni iitwayo "Operation Atlantic Route" inayolenga kukamata mali za viongozi wa zamani wa Kongo zinazoshukiwa kupatikana kwa njia isiyo halali.
Ndege hiyo imekuwa maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Faro - Ureno kwa takriban miaka 19 bila matumizi yoyote. Kwa mujibu wa mamlaka za uwanja, Bemba alipewa siku 60 za kuiondoa ndege hiyo na kulipa deni la maegesho linalokadiriwa kufikia karibu euro milioni moja.
Baada ya muda huo kupita bila hatua kuchukuliwa, ndege hiyo ilitangazwa kuwa imekiuka sheria mpya ya Ureno kuhusu ndege zilizotelekezwa katika viwanja vya ndege.
Operesheni ya Atlantic Route inaendeshwa na Sekretarieti ya Usimamizi wa Mali ya Wizara ya Sheria ya Ureno.
Katika hatua ya hivi karibuni ya Februari 2026, operesheni hiyo ilikamata na kuuza kwa mnada nyumba ya kifahari iliyopo Quinta da Marinha, Cascais, inayomilikiwa na Waziri wa zamani wa Kongo Gilbert Ondongo.
Nyumba hiyo yenye vyumba saba, bwawa la kuogelea, ukumbi wa mazoezi na ukumbi wa sinema iliuzwa kwa zaidi ya euro milioni 10.9.
Kukamatwa kwa ndege ya Bemba si tukio la kwanza linalohusisha mali za viongozi wa Kongo nchini Ureno. Hata hivyo, tofauti na nyumba ya Ondongo, ndege ya Bemba haijauzwa bado bali imekamatwa rasmi na mamlaka kutokana na ukiukaji wa kanuni za uendeshaji wa viwanja vya ndege.
Wakati Bemba hajatoa kauli rasmi, watu wa karibu naye wanasema jukumu la gharama hizo linapaswa kubebwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai. Wanadai kuwa mahakama hiyo ndiyo iliyoweka zuio kwenye mali zake wakati alipokuwa anakabiliwa na mashtaka, kabla ya kuachiliwa huru mwaka 2018 baada ya mashtaka hayo kufutwa.
Kando na hilo, Novemba 2025 ndege iliyobeba Waziri wa Madini wa sasa wa DRC, Louis Watum Kabamba, ilipata ajali ya kuteleza nje ya barabara ya kuruka na kuteketea kwa moto ingawa alitoka salama. Tukio hilo halihusiani moja kwa moja na operesheni ya Atlantic Route.