Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Aisee hapo ni shida nilishawahi kukutana na kesi kama hiyo gearbox ikabadilishwa zaidi ya mara nne, unafunga inakuwa poa ila round moja ya kutest ukirudi Kimeo! Gearbox ya mwisho kufungwa ikatulia lakini ulaji mafuta ukawa maradufu
Ushauri : uza hiyo gari utafute nyingine
Jaribu kubadilisha ECU huwa haisomi upande wa gear yan muite fundi ajaribu kufunga ECU nyingine uone kama itafanya kazi, hapo ECU itakuwa haina mawasiliano mazuri na gear box
 
Habar za mapumziko ya Karume Day? Naomba ushauri wakuu, navua matairi kwa mara ya kwanza!
Naomba kujua nivae size ipi na aína gani kwa uimara na ubora hapa kwetu Bongo nchi ya majaribio kila leo!
Size nilizokuwa nazo toka Japan ni 185/70R14 88S!
Asanteni sana kwa huduma hii nzuri!
 
Habar za mapumziko ya Karume Day? Naomba ushauri wakuu, navua matairi kwa mara ya kwanza!
Naomba kujua nivae size ipi na aína gani kwa uimara na ubora hapa kwetu Bongo nchi ya majaribio kila leo!
Size nilizokuwa nazo toka Japan ni 185/70R14 88S!
Asanteni sana kwa huduma hii nzuri!
Ni gari aina gani? Jaribu kufuatilia vzr specs za gari yako. Mm niliwahi nunua gari yenye specs tofauti na tairi za gari hivyo nikabadilisha tairi ili kuweka zile zenyewe.

Ukiweka aina ya gari itakusaidia kukupa jibu sahihi usiamini sana size ya tairi zilizokuja na gari
 
Weka hiyo hiyo usibadili
ImageUploadedByJamiiForums1460031333.680818.jpg


Hiyo ni tairi size 17 ambayo ilikuja na gari lakini sio size proper. Gari hii ni escudo 2007 ambayo appropriate size ya tairi ni size 16. So imebidi kuvua rim na kuweka rim za 16 tofauti na zile 17 zilizokuja na gari
 
Gear box oil ya gari gani kwanza ? Kama ni za automatic gearbox za gari za kijapan, huwa haitumii oil bali ATF ( Automatic Transmission Fluid ) waswahili tunaita hydraulic oil, inabadilishwa kila baada ya Km 100,000 ( Laki moja ).
 
Back
Top Bottom