Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hiyo kitu inapatikana kwa bei gani na nini madhara ya kutobadili mapema break booster maana kwa sasa uchumi siyo mzuri
 
Leo asubuhi nimewasha gari naona inatoa moshi mweupe na haijawahi kutokea. Gari ni toyota verosa linakama wiki 3 toka niagize. Jana usiku ilinyesha mvua kubwa sana na leo haki ya hewa ni baridi sana @ mshana jr
Kama ukiziba na kiganja kwenye exhaust pipe hakuna marks basi hio ni mvuke sio moshi LA utakuwa umeweka mafuta machafu jana
 
Kama ukiziba na kiganja kwenye exhaust pipe hakuna marks basi hio ni mvuke sio moshi LA utakuwa umeweka mafuta machafu jana
Ngoja nijaribu hilo la kuziba exhaust. Ila mafuta niliweka toka jumapili na haikutoa moshi mweupe. Naweka mafuta gapco.
 
Habar wakuu! Nini tatizo la redio, flasher nk kuwa na joto sana kwenye gari wakati naendesha?? Asanteni,
Sio shida kubwa kuna baadhi ya redio coolig system yake haiweZi kuipoza kabisa redio na wakati huo huo kuna joto toka kwenye engine linapenya mpaka kwenye dashboard(kwa baadhi ya magari) hivyo kusababisha hii hali
 
bcd64e346337b9a8072a027ce53a9afd.jpg
 
Hamna tatizo, ili mradi uifanyie service nzuri na kukagua hamna tatizo kwenye gari. M niliwahi kusafiri nayo kutoka Dar hadi Bukoba carina T.I
mkuu carina ni gari makini sana. Fanya service, weka oil nzuri,kagua tairi zako, piga gia mkuu yani wala usiwaze hiyo gari ya cc 1490 inaenda popote na hongera kwa kununua moja kati ya gari ambayo haitojuta kuwa nayo
 
Wakuu hivi kunatatizo la kiufundi au kiusalama ya kutumia Carina kwa safari ndefu mfano mtwara-arusha?niliplan kununua rav4 ila bajet imegoma
Ti popote inakwenda na inakula mafuta vizuri kuliko. Nje ya mji inafikia 13km hadi 18km kwa lita 1 ya petrol. Dom - Dar kilomita 450 natumia sh 50,000/ km lita 27 wakari basi nauli ni watu wa2 tu @,25,000
Tatizo la hizi gari za cc1490 ni timming belt sio ya gia hivyo hakikisha kila km laki moja unabadili hata km imetoka Japan mengine check oil na maji kabla ya safari tyre upepo ulioidhinishwa kwa mwendo na muda wa uundaji tyre. Vinginevyo utafiks salama maana tochi ni kibao wote wanaends salama njiani

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom