Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

mshana jr au mwingine mwenye uzoefu nataka kuagiza raum, ila watu wanasema old model ni imara kuliko new model, please mwenye kujua haya magari vizuri, na matatizo yake,

Raum afadhali hata hizi new model ndugu yangu lakini fact moja ni kwamba gari nyingi hizi zenye cc ndogo na za kisasa ni gari za kufanyia mambo mepesi hazitaki shuruba
 
Naomba kujuzwa kuhusu toyota belta. Zina uzuri au ubovu gani.. naona haziko nyingi mjini..
 
Naomba kujuzwa kuhusu toyota belta. Zina uzuri au ubovu gani.. naona haziko nyingi mjini..

Sio gari maarufu na hata mi mwenyewe nimeziona nafikiri mbili au tatu hivi hivyo ni ngumu kuzijadili
 
New model yake c mbaya kama akiitunza vizuri.ila old ni imara zaidi,mi old nna mwaka 4 huu haijanisumbua kabisa na njia zangu ni za makorongo makorongo
 
Raum afadhali hata hizi new model ndugu yangu lakini fact moja ni kwamba gari nyingi hizi zenye cc ndogo na za kisasa ni gari za kufanyia mambo mepesi hazitaki shuruba

Uko sawa kbs mkuu, gari kama Passo, ist, raum na hizo gari zenye cc chini ya 1800 yani sio gari ambalo unaweza jiamini sanaa kuwa una gari hasa kama ni mtu wa mishe mishe na bht mbaya iwe ni barabara yenye makorongo
 
Wadau wa magari tujuzane ongezeko la kodi kwenye kuimport gari toka nje imeongezeka kwa kiasi gani kwenye bajeti iliyosomwa leo. Na je itaathiri magari yaliyoagizwa tayari?
 
Wadau wa magari tujuzane ongezeko la kodi kwenye kuimport gari toka nje imeongezeka kwa kiasi gani kwenye bajeti iliyosomwa leo. Na je itaathiri magari yaliyoagizwa tayari?

Kuna ongezeko? Confused !! I guess ni yale yatakayofika/kulipiwa after 1st July
 
Nawashukuru sana mshana jnr na ansah miles , rav4 shida yake space ndogo sana! Mbona kuna wengine wanadunda nazo sana hizo hizo harrier?

Kaka pia angalia na mahitaji yako ya gari yanalenga zaidi nini..suala la space lifikirie kwa undani kidogo....maana Rav 4 hasa old model naziona kama bado ni vehicle of choice kwa normal SUV...maana watu wanatumia mpaka Duet ...suzuki kei. .vits na passo...gari kubwa kama ni kwa long safari is ok ila kama ni kwa mambo ya town trip baki na Rav 4 yako...harrier si gari imara vile na engine na gia box zinasumbua watu wanatoa 1mz wanaamua kufunga 3s ...modification zinakuwa kibao....kwangu mimi bado ni mshabiki wa gari ndogo nina move na ninafika popote pale bila shaka..kama ni second choice think for kluger 2.4
 
Sio gari maarufu na hata mi mwenyewe nimeziona nafikiri mbili au tatu hivi hivyo ni ngumu kuzijadili

Nasikia ni succesor wa toyota platz na cc zinafanana na zile zaplatz.. ila sijajua kuwa hizi ukiachana na kuboreshwa muundo ni bora zaidi kuliko platz au?
 
Nasikia ni succesor wa toyota platz na cc zinafanana na zile zaplatz.. ila sijajua kuwa hizi ukiachana na kuboreshwa muundo ni bora zaidi kuliko platz au?

Yawezekana kabisa lakini kwa platz ni gari nyanya kwa kweli
 
Hii expire date vip? Nimetoa spre tyre niangalie isije expire. Nimekuta ImageUploadedByJamiiForums1434265729.439142.jpg kama hiyo picha hapo. Hii ni brand new Bridgestone iliyokuja na gari ya mwaka 2006. Je hiyo 3205 ni kuwa iliexpire 2005 wiki ya 32 ama ni 2015 wiki ya 32?
 
Hii expire date vip? Nimetoa spre tyre niangalie isije expire. Nimekuta View attachment 260004 kama hiyo picha hapo. Hii ni brand new Bridgestone iliyokuja na gari ya mwaka 2006. Je hiyo 3205 ni kuwa iliexpire 2005 wiki ya 32 ama ni 2015 wiki ya 32?

Nachofahamu kwa hiyo 3205 ni maelekezo kuwa hiyo tyre imetengenezwa lini, so kwa tafsiri ni kuwa imetengenezwa wiki ya 32 mwaka 2005,
 
Back
Top Bottom