Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mkuu nashukuru kwa kunijuza bei ya turbo,lakini hebu jikite kwenye maswali yangu matatu halo juu utakuwa umenisaidia sana.
Cc:mshana jr,RRondo na wengineo mkuje huku

Kazi kubwa ya turbo ni kuongeza nguvu na mwendo kasi wa gari turbo ikifunguka mlimani inatembea sana. Turbo inamhimu sana kwenye gari za diesel turbo ikifa mlimani hata mwendesha baiskeli anakupita.
 
kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.

Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.

Kwa uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake

karibuni sana

ushauri: Jinsi ya kununua gari iliotumika ndani ya tanzania


View attachment 225786
mkuu tunaitaji msaada wenu kati ya hizi gar mbili, mazda rx8 na toyota celica, katika mafuta na spea. Natanguliza shukrani
 
kazi za ECT ile button imeandikwa POWER,ECT NA SNOW ukiswitch power maana yake gia zinachelewa kubadilika km manual ukiweka gia unavutaaa pedo wee afu gia ingine unakanyaga mafuta weee,ukiweka snow ni nchi za barafu gia box inaongeza nguvu kwenye gia ya aina moja inayokubali hali iliyokuwepo ya barafu
 
wadau nina pickup ya hilux ni automatic, niliishusha mashine na kufanya overwhole ya mashine. Gari ina nguvu na kila kitu kiko sawa ishu imekuja kwenye ulaji wa mafuta.
Nilikua natoka point A kwenda point B kwa mafuta ya elf 20 ila sasa naweka ya elf 30 kwa umbali ule ule. Mda mwingine hata hayo ya elf 30 yanakata gari imekua kama jini linanyonya uchumi wangu.
NB. Gari haina mis na nimesafisha plug zote zinachoma vizuri tu na gari ina nguvu sana
 
Jamani kwa mwenye kujua ni wapi nitaweza pata gari used ya kununua!…aina ni Rav4,Escudo milango 5(auto/manual) Noah old model na nyinginezo!…karibuni!
 
Jamani kwa mwenye kujua ni wapi nitaweza pata gari used ya kununua!…aina ni Rav4,Escudo milango 5(auto/manual) Noah old model na nyinginezo!…karibuni!

Pana mdau yuko humu wanaofis pale quality centre yuko njema sana....wanaitwa Autojapan...mpate muwakilishi wao kwa namba hii 0767 328 063...jamaa yuko friendly sana atakutake through:

Disclaimer: haya ni maoni yangu kutoka na uzoefu wangu na huyu bwana...sikuhakikishii usalama wa fedha zako...hivyo zingatia vigezo vya kiusalama vya manunuzi mtandaoni. Asante.
 
Jamani kwa mwenye kujua ni wapi nitaweza pata gari used ya kununua!…aina ni Rav4,Escudo milango 5(auto/manual) Noah old model na nyinginezo!…karibuni!

Nina escudo ya 1999, automatic, namba B, milango 5, km 99993... Nipe namba yako nikutumie picha whatsapp
 
Wakuu heshima kwenu, ningependa kufahamu zaidi kuhusu hizi Battery Powered Cars ubora wake na ulaji wake wa mafuta kiujumla. mshana jr proNDO na wadau wengine
 
Last edited by a moderator:
wakuu ningependa kujua kuhusu
kupatikana kwa spares za gari
aina ya Honda fit umekaaje
bongo kwani nimetokea
kuipenda nisije nikanunua
ikawa majanga pale spare parts
sake zitakapo hitajika.
 
wakuu ningependa kujua kuhusu
kupatikana kwa spares za gari
aina ya Honda fit umekaaje
bongo kwani nimetokea
kuipenda nisije nikanunua
ikawa majanga pale spare parts
sake zitakapo hitajika.

Kiukweli spare zake sio nyingi but zinapatikana...
 
Vipi washikaji,

Niko na swali moja hapa, hivi nimekuwa nikiyaangalia magari yanayouzwa kwenye mtandao kama vile Kupatana.com na nikashangazwa sana ni kwanini Toyota Crest ama Toyota Mark II GX100 yanauzwa kwa bei ya chini mno?

Kwa mfano unaweza kupata Cresta iliyo nzuri kabisa inauzwa milioni tano tu! Ni vipi yanauzwa kwa bei nafuu hivyo? Ama ni kwasababu engine zao kubwa sio unywaji wao wa mafuta uko juu sana?
 
Ahsante mkuu nimetafuta fundi akafunua head cylinder akaichonga pia kuna ile ckumbuki jina lake ina wembamba wa kadi ila ina matundu kama manne inakaa katikati inaozuia maji yasiingie kwenye piston ilikua imekatika so maji yakawa yanaingia

Nunua Over-haul kit ya gari yako utakuta takataka zote ziko humo, hiyo ambayo huikumbuki inaitwa Cylindr head gasket. Kwenye Overhaul kit kuna kila kitu na zipo kit za ubora mbalimbali maana wachina wanahudumia makabwela kwa budget zao.
 
Kiukweli spare zake sio nyingi but zinapatikana...

Mkuu mim naomba unipe mwanga. Kuna gari Vw Touran ya mwaka 2007, 1380cc, CIF yake ni US$3,225 hadi bongo. Je hii itaweza kugharimu kiasi gani kwenye mambo ya kodi, clearance, exercise duty na mengine kiujumla hadi kukabidhiwa ufunguo. Natanguliza shukrani kwa wote jukwaani.
 
Nunua Over-haul kit ya gari yako utakuta takataka zote ziko humo, hiyo ambayo huikumbuki inaitwa Cylindr head gasket. Kwenye Overhaul kit kuna kila kitu na zipo kit za ubora mbalimbali maana wachina wanahudumia makabwela kwa budget zao.
Ahsante mkuu exactly ndio hiyo gasket niliyoisahau, samahan tena hiyo kit inapatkana wapi na shingap kigar changu ni duet 1999 manual transmission
 
Back
Top Bottom