Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mkuu hiyo gari haikuwa na guarantee? Tafuta fundi wa uhakika au kama huhitaji hiyo 4 wheel unaweza kutoa shaft za mbele kuliko kufungua gear box inaweza ikazalisha zaidi ya hayo.
Safi sana mkuu MANI, ni vizuri atumie njia hii kama sehemu ya troubleshooting.Kabla ya kuituhumu gear box ni vema
kutenganisha shafti na hivyo ataangalia kama tatizo litaisha au litaendelea kuwepo na hapo atafanya maamuzi sahihi.
 
Last edited by a moderator:
HAKI ZA DEREVA ANAPOKAMATWA NA TRAFFIC
- Trafiki hana idhini ya kukulazimisha kumkabidhi leseni yako
-Akikukuta na kosa na kukuandikia notification na ukalipa ni lazima akupe risiti ya serikali
-Hana haki ya kukuulizia kuhusu road licence hiyo ni kazi ya TRA kwakuwa siku utakapoenda kulipa utalipia na faini
-kama huna leseni una haki kisheria kuipeleka kituoni ndani ya Massa 72 ya kazi tangu ulipotakiwa kufanya hivyo
-Akikusimamisha una haki ya kusimama sehemu ile ambayo utaona ni salama na si lazima usimame anapotaka yeye
- Sio kila kosa ni la kuadhibiwa, mengine ya kuonywa au kuelimishwa

Hapo kwenye issue za road licence matrafic kumbe wanatuonea eehh. Kuna trafic alinilamba buku tano yangu kiulani.
Na vp kuhusu insurance nayo wana haki ya kukulipisha faini km itakuwa imekwisha.?!
 
Hapo kwenye issue za road licence matrafic kumbe wanatuonea eehh. Kuna trafic alinilamba buku tano yangu kiulani.
Na vp kuhusu insurance nayo wana haki ya kukulipisha faini km itakuwa imekwisha.?!

Insurance ni haki kabisa kwakuwa ndio inakuhakikishia wewe na third party user kulindwa litokeapo tatizo la wizi, ajali au janga! Ulinzi kwa maana ya malipo, matibabu, fidia na matengenezo
 
Kwa nini taa za Dash board huwa zinga rangi nyekundu, orange, green na blue?

-Nyekundu inaashiria hatari, hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka

-orange/njano inaashiria tahadhari(warning) hivyo jiandae kuchukua hatua
-blue/kijani? Inaashiria mambo poa! Japo kwenye dashboard mara nyingi hapatakiwi kuwaka taa yeyote baada ya kuwasha gari, sana sana ni P kwa hizi automatic, na D wakati ukiwa kwenye mwendo na kama ni mchana
 
Uzi mzuri sana, nimesoma comment zote,
Sasa mkuu nipe ushauri na uzoefu wako, nataka kuchukua runx, ila itatumika zaid barabara ya vumbi, je inafaa? Vp uimara wake? Vifaa vinapatikana? Je wewe ni fundi wa magari?

Hapana mimi sio fundi, runx si ndio kizazi cha ist, Allex, duet nk? Ni gari ambazo hazitaki shida wala mikikimikiki, kwa ushauri nunua gari yeyote kizazi cha corolla100, 110 au hata GX 100 kavu! GX vvti itakutesa
 
NINI MAANA YA ALAMA HIZI KWENYE GEAR!?

P - parking
R - reverse
N - neutral
D, D1,D2- drive
D- normal drive
D1- inatumika kwenye na tifutifu na mwinuko hii mara nyingi inaenda na E-PWR- extra power, kwahiyo unapo engage D1, ni vema uka engage na E-power, mara nyingi button inakuwa kwenye dashboard! Hapa gari inakuwa nzito lakini yenye nguvu sana na mwendo unakuwa mdogo
D2 pia inaenda na E-PWR button na hii inatumika kwenye utelezi zaidi

O/D - over drive, button yake iko kwenye gearleaver, tumia O/D Mara nyingi kwenye speed isiyozidi km 80 kwa SAA
Hakuna hatari ya kuengage na ku disegage O/D kwenye mwendo mdogo lakini ni hatari mno kwenye mwendo mkubwa, ukifanya hivyo hasa kutoa O/D kwenye mwendo mkubwa gari itakuwa nyepesi ghafla hivyo kusababisha kuyumba kupoteza mwelekeo na hatimaye ajali

NB: Alama hizi zaweza kubadilika kidogo kulingana na model ya gari na usasa
 
Kazi ya N hapo ni nini? Suzuki escudo 2007 model
ImageUploadedByJamiiForums1423705336.235256.jpg
 
Kuna ile mada ina ufafanuzi kuhusu tires, traction, thread ratio nk. Mambo ya upepo nk. Kuna mtu anazo?

Mi sina lakini naweza sema neno hapo! Kwa usalama zaidi tairi haipaswi kutembea zaidi ya km elfu 40 ikizidi sana ni 50, traction inasaidia velosity ya speed na uchakavu wa tairi hivyo ni vema ukafunga kama mshale unavyoelekeza, tread ratio nayo ni muhimu na ukubwa pia, unapofunga tairi oversize ulaji wa mafuta huongezeka au kasi ya gari hupungua

Upepo pia ni muhimu kwa stability ya gari barabarani na uchakavu was tairi pia mara nyingi inashauriwa upepo wa tairi za mbele usizidi 30 na was tairi za nyuma usizidi 35
 
Hapana mimi sio fundi, runx si ndio kizazi cha ist, Allex, duet nk? Ni gari ambazo hazitaki shida wala mikikimikiki, kwa ushauri nunua gari yeyote kizazi cha corolla100, 110 au hata GX 100 kavu! GX vvti itakutesa

Mkuu mbona mafundi na wazoefu wa magari wanasema kuwa GX 100 vvt-i ni nzuri kuliko GX 100 Kavu.?! Ktk suala la ubugiaji wa wese n.k mimi naburuza GX 100 vvt-i..
 
Mi sina lakini naweza sema neno hapo! Kwa usalama zaidi tairi haipaswi kutembea zaidi ya km elfu 40 ikizidi sana ni 50, traction inasaidia velosity ya speed na uchakavu wa tairi hivyo ni vema ukafunga kama mshale unavyoelekeza, tread ratio nayo ni muhimu na ukubwa pia, unapofunga tairi oversize ulaji wa mafuta huongezeka au kasi ya gari hupungua

Upepo pia ni muhimu kwa stability ya gari barabarani na uchakavu was tairi pia mara nyingi inashauriwa upepo wa tairi za mbele usizidi 30 na was tairi za nyuma usizidi 35

Ndugu Mimi Nina Honda Crv 2002 upepo nimeweka tairi za mbele 40 na tairi za nyuma 40, je kwa usalama inafaa?
 
Ndugu Mimi Nina Honda Crv 2002 upepo nimeweka tairi za mbele 40 na tairi za nyuma 40, je kwa usalama inafaa?

Mmmh hapana weka hiyo ratio niliyosema hapo juu kumbuka gari inapokuwa kwenye mwendo msukumo huongezeka kwenye tairi hivyo waweza sababisha bust
 
Mmmh hapana weka hiyo ratio niliyosema hapo juu kumbuka gari inapokuwa kwenye mwendo msukumo huongezeka kwenye tairi hivyo waweza sababisha bust

Sawa ndugu! Sababu nilikwenda pale wanapojaza upepo nikawauliza normal upepo kwa matairi inatakiwa ngapi? Akasema 40 kwa kila tairi.
 
Sawa ndugu! Sababu nilikwenda pale wanapojaza upepo nikawauliza normal upepo kwa matairi inatakiwa ngapi? Akasema 40 kwa kila tairi.

Mmh hapana hiyo sio kubwa na hata kashata zake haziwezi kuhimili huo mzigo labda kama hiyo gari isikae juani wala kutembea barabarani

Kwa macho huwezi kuona na kama tairi ni mpya lakini kama tairi zimeshaanza kuchoka si salama kabisa! Upepo standard ni front wheels 30, rear wheels 35
 
Ok! Baadae nitapita nimuambie anipunguzie upepo
 
Back
Top Bottom