Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuu naomba kujua kwa gari za auto, nawzaje kuendesha bila Ku press pedal ya mafuta kwa gari ambayo haina cruiser control
Doooo hiyo ni ngumu sana mkuu..labda kwenye pedal ya mafuta uweke jiwe au kitu kizito..hahahahaha joks tuu mkuu..nahisi haiwezekana kama haina cruiser control.
 
Habari wakuu
msaada wenu tafadhali
Ni Web gani nikiingia naweza jifunza utengenezaji wa gari,
hasa malori kama scania, volvo, mercedes benz, man, daf n.k?
 
Habari wakuu
msaada wenu tafadhali
Ni Web gani nikiingia naweza jifunza utengenezaji wa gari,
hasa malori kama scania, volvo, mercedes benz, man, daf n.k?
Naamini Watalaam wanaweza kukusaidia hizo website, ila ushauri wangu, unaweza kutumia YouTube kukusaidia kufahamu ni kwa namna gani Tatizo fulani kwenye gari/ lorry fulani linaweza kutatuliwa, and then wewe ukaenda kupractise
 
Habari wakuu
msaada wenu tafadhali
Ni Web gani nikiingia naweza jifunza utengenezaji wa gari,
hasa malori kama scania, volvo, mercedes benz, man, daf n.k?
Ni ngum sana kitu unachokitafuta na ugumu wenyewe hasa kwenye maandishi yako mm binafsi ningeweza kukusaidia lkn sijajua maana au hitaji lako..kwanza hujasema unataka ujue kutengeneza nn?? Harafu ufundio sio rahisi kama ww unavyofikilia.yaani kama hufaham lolote lilee yaani wataka ufundishwe au ujifunze kwenye website achana na wazo hilo hutoweza fanikiwa au itakubidi utumie njia ndefu na mda mwingi kwa siku nyingi.vitu utakavyo jifunza mwezi mzima na mtu atakaye kuwa gereji atavifaham kwa dakika chache..

Mfano cylinder head vitu vyake ww utasoma mwezi mzima na itatakiwa utafute video zake uangalie lkn kwa mtu wa gereji ni siku moja tuu tena dk chache anavifaham.ndio maana ukimchukua kijana ukampeleka shule ya ufundi akasomea miaka mi3 na ukaja ukamchukua kijana mwingine ukampeleka gereji mwaka mmoja ..yule wa gereji anakuwa fundi full na anafaham vitu vingi zaidi ya yule wa shuleni.
 
Ahsante kwa ushauri wako ndugu,
kifupi nami ni mechanics
ila lengo nijiongeze na kwenye web ili inisaidie zaidi,
maana kuna siku nilifungua Filters za Benz moja hivi ni Actros 963-4D
sasa ilikuwa inshu kuachanisha mfunuko wake hiyo filter, na ukiandika youtube wanaleta sivyo,
ndo maana nikaomba msaada kwenu.
 

Attachments

  • IMG_20181130_114039.jpg
    100.9 KB · Views: 99
Msaada wa kuidhibiti hii taa nifanyaje
Ni Truck mercedes benz actros
 

Attachments

  • 1543832253090.jpg
    116.8 KB · Views: 119
n
Ohooooo basi haina shida ni shakusoma mkuu na shida yako ishatatulika website zipo nyingi sana ..lkn wacha nikudondoshee 1. Duniani MHH AUTO.COM 2.CARTECHNOLOGY.COM 3.DIGITAL KAOS.

Mkuu humo utapata zaidi ya ulichokuwa unataka uzuri wa humo kama unashida ukiomba msaada wenzetu ni watu wa aina ya tofauti sana yaani ww ndio utasumbuliwa mwenye shida mpaka utashangaa..wwnapenda sana akikuelekeza kitu afike mpaka mwisho ajue kama solution yake imefaa au laa..
 
Hebu pia acheki fuel pump huenda imeshafeli tayari.
Wakubwa heshima kwenu

Napenda kutoa mrejesho wa changamoto ya gari RAV4 Kama nilivyowasilisha hapa, napenda kushukuru kuwa tatizo limetatuliwa, namshukuru Sana ndg yetu LEGE ambaye alijitolea na kufix Tatizo hilo, kilichoonekana Kama Tatizo ni mfumo wa mafuta, fuel pump na chujio lake, na nozel vilikuwa vimejaa uchavu, vumbi na takataka kibao, hivyo Mafundi walifungua tank, fuel pump, chujio na nozel na kusafishwa ipasavyo, Kwa sasa napenda kusema kuwa gari ipo vzr kabisa inapiga na kuongeza Mwendo bila kusita na bila wasiwasi wowote.

Nachukua fursa Hii kutoa shukrani za dhati Kwa ndg LEGE na wadau wote wa hii thread , mchango wenu umefanikisha kutatua changamoto iliyokuwa inasumbua.
Asanteni
 
Msaada wa kuidhibiti hii taa nifanyaje
Ni Truck mercedes benz actros
Mkuu kuidhibiti hiyo ni rahisi na nikazi ngumu kweli kweli?? Ww upo wapi ?? Mkoa gani?? Kama upo dar es salaam mm nitakusaidia kukupimia kwa bei rahisi tuu ya karibia na bure kwa kugaramikia nauli ya boda kutoka mwenge mpaka ulipo na kunirudisha mwenge.. au kama unaweza basi tafuta mtu mwenye C4 or C3 or C5 au mashine nyingine yoyote ile kisha ipime then utajua tatizo ni nn then ndio ulekebishe hilo tatizo mambo yatakwenda fresh.
 
Habari njema hii.

Ahsante kwa mrejesho mkuu.
 
Aman iwe kwenu wadau wote humu.......... Mimi sijui chochote juu ya magari lakin nategemea kumiliki gari siku za usoni..........


Naomba kuelimishwa yafuatayo :

1) mpangilio wa plate number ya gari Tanzania {kuniwezesha kuitambua gari na mengineyo}

2)Nikitaka kununu gari iwe kwa mtu au show Room nizingatie nn? {mambo muhimu}

3) Baada ya kuinunua maswala ya kisheria au utaratibu ukoje!?

4)Maintainance ikoje!?

5)kwenye maswala ya injin huwa nasikia tu CC...mara 4/6 cylinder (sielewi) manake nn!?

6)Nikitaka kununua gar imara ya kisasa ni nunue ipi (mfano nahitaji yenye sehem ya mizigo na double cabin, nyingine ya kutembelea tu)

7) kile kifaa cha kufanyia diagnosis kwenye gar kinaitwaje na kinauzwa bei gan!??

ASANTENI SANAA.......


Karibuni pia kujielimisha......
 
Mkuu mie nipo tayari kuwa mwanafunzi wako mtiifu. Nina strong passion na magari aisee
 
Mkuu mie nipo tayari kuwa mwanafunzi wako mtiifu. Nina strong passion na magari aisee
Karibu sana mkuu JO AUTO TECH tujifunze wote mm mwenyewe ni mwanafunzi siunajua vile technologia kila siku inakuwa na elimu haina mwisho..so njoo tujifunze kwa pamoja .kama upo dar es salaam karibu sana mwenge
 
Karibu sana mkuu JO AUTO TECH tujifunze wote mm mwenyewe ni mwanafunzi siunajua vile technologia kila siku inakuwa na elimu haina mwisho..so njoo tujifunze kwa pamoja .kama upo dar es salaam karibu sana mwenge
Nipo Dar mkuu. For sure nitakuja
 
Nimekusoma, na ntakutafuta soon tu
 
Lege Ofisi iko sehemu gani nikutembelee, nami nipo hapa Dar, Mbagala ndo naishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…