Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Nimesikia Rav 4 ya 1998 na rav 4 new model....ni bora zile za 1998... Je kuna ukweli ndani yake....naomba maelezo tafadhari
 
Mshana,hivi Suzuki Maruti ina CC ngapi,na Nisaan Patrol ,na Toyota Hilux zina CC ngapi mwenye uelewa anijuze tafadhari sana
Kamwe huwezi kulinganisha engine ya Suzuki Maruti na ya Nissan Patrol au Toyota hilux...nisingumzie kwenye cc bali ni kwamba Maruti engine yake ni ndogo sana kisha inafuatia hilux kishapo Nissan
 
Suzuki Alto
 

Attachments

  • 1454955942303.jpg
    1454955942303.jpg
    65.3 KB · Views: 83
Mshana jr ,
Naomba ushauri nataka kuchukua hii suzuki alto
Ya 1998,, vipi kuhusu spera , uimara wake
Ila ina CC 660
 
Namaanisha in terms of durability na pia engine....nasikia VVTI ni bora kuliko D4 ila sina uhakika kuhusu hilo
Kuna post ya LEGE ilichambua vizuri sana D4 sio mbaya kama tunavyodhani au kuaminishwa kikubwa na cha muhimu ikitokea shida upate fundi sahihi
 
Inategemea na cc


Mkuu Mshana jr, niliuliza kuhusu Mitsubishi Airtrek lakini hakuna aliyenip ABC zake. Vipi wewe mkuu huna wasifu wa hii gari?

Lakini pia nmevutiwa na gari aina ya Ford xcape hasa ile ya cc1980 na ile ya 2260(cc2300),sasa je ipi ni nzuri kati ya hizo, ipi ni 4cylinder na ipi ni V6?

Nitashukuru mkuu
 
Wakuu nahitaji gari ya kutembelea ngumu kidogo ningependa zaidi Rav 4 nina 15M naweza pata mpya wakuu ni mgeni kwenye idara ya magari!
 
Nimesikia Rav 4 ya 1998 na rav 4 new model....ni bora zile za 1998... Je kuna ukweli ndani yake....naomba maelezo tafadhari
hakuna ukweli hapo mkuu new model ni nzuri zaidi kuliko hiyo ya mwaka 1998 new model ina udambwi dambwi mwingi zaidi ya kisasa zaidi ina mambo mengi zaidi kuliko hiyo old model new model ina ABS,VSC,TRC,AIR BAG, n.k
kwenye suala la mafuta hata usiulize new model inakula mafuta vizuri zaidi kuliko hiyo old new model ina nguvu zaidi new model ni rafiki wa mazingira na hasa ukiipata yenye engine ya d4 achana na wanga wa magari wababaishaji wasio jua juu ya uzuri wa d4. na nini maana ya d4


ww mpaka gari za diesel now ni d4d kuna gari za diesel zinakwenda mpaka 18km kwa lita
 
Mkuu Mshana jr, niliuliza kuhusu Mitsubishi Airtrek lakini hakuna aliyenip ABC zake. Vipi wewe mkuu huna wasifu wa hii gari?

Lakini pia nmevutiwa na gari aina ya Ford xcape hasa ile ya cc1980 na ile ya 2260(cc2300),sasa je ipi ni nzuri kati ya hizo, ipi ni 4cylinder na ipi ni V6?

Nitashukuru mkuu
CHAZA hizi gari zote sina uzoefu nazo ndio maana hata mimi nilikaa kimya kusubiri wajuzi wengine
 
Mshana gari yangu inashindwa kuwaka hadi nirudie zaidi ya Mara moja ni corolla110


Na kama sio starter ni kabureta ishawai nitokea iyo tatizo..
 
Mshana gari yangu inashindwa kuwaka hadi nirudie zaidi ya Mara moja ni corolla110


Na kama sio starter ni kabureta ishawai nitokea iyo tatizo..
Nenda kwa fundi starter kwanza aicheki inawezekana brush zimeisha
 
ni.gari aina gani mkuu na.je huwa inawaka taa gani?? maana kuna taa 2 za tempereture blue /green hii kawaida na red hii ndio mbaya inamaanisha gari inachemsha au overheating je ww huwa inawaka ipi kati ya hizo.
Gari ni Toyota platz, taa inayowaka huwa n blue
 
service inafanywa kutegemea na aina ya oil uliyoweka. Kuna oil kama za bp premium zinaenda mpaka km 5000 bila kuchoka ila kama watumia oil za kawaida elf 3 ndo mwisho wake hebu taja oil unayotumia
Pia inashauriwa hata kama oil hiyo ni km say 3000 usisubiri hadi zifike exactly..ukisubiri iwe chafu sana unaua engine..mi nilikua natumia bp standard kwa nissan ila nikifika 2500 naitoa.ila kwa sasa nimehamia kwenye fully synthetic ya km 20,000 ndo service.
 
Back
Top Bottom