Wakuu naombeni ushauri,kwa kuzingatia uimara,upatikanaji wa spare na ulaji wa mafuta,kati ya toyota altezza na mazda attenza sport nijitwalie ipi?
But naona altezza nyingi ni 2000cc na mazda attenza ni 2260cc,so nikadhani mazda attenza inabugia zaidi wese.JIBU: 1. Uimara= zote ni imara sana ukizingatia ni sport sedans,sport cars huwa na added advantage ya uimara,so hilo ondoa hofu.
2. Upatikanaji wa Spare parts= Hilo pia usihofu Spea za Mazda zipo Keko garage na Nduvini huziagiza Nairobi au Japan lakini pia spare siku hizi za mkono wa pili zipo tele gulioni Kariakoo ukikosa unaagiza Kenya au kwa car dealers kv be forward wanaleta spare yoyote utakayo unawapa sample tu.
3.Ulaji wa wese= zote mbili zinameza ila mazda ina nafuu alteza power train yake ipo juu.
KILA LA KHERI...KWANGU YOTE BOMBA
Habari? Ndugu zangu naomba ushauri nimeipenda gari aina ya subaru legacy (picha ntaiweka hapo chini) naomba ushauri wenu juu ya masuala mbalimbali ya kiufundi, gharama, spea na ziada yoyote kwa mjuzi au aliewahi kuitumia. Asanteni
Gari nzuri usiwaze sana kuhusu parts dunia imekuwa kijiji
Asante na nashuruku kwa ushauri wako. Naomba ushauri wa kiufundi mwingine katika gari yangu aina ya toyota altezza sport. Gari kiujumla ni nzuri sana kuanzia ulaji mafuta, utulivu barabarani, mwendo n.k ila tatizo lipo kwenye sauti tu. Inatoa sauti kubwa (vijana wa mjini wanaita chipolopolo) sasa mimi binafsi siipendi itoe mlio huu kwani mwanzo nilijaribu kufanya hadi modification ya kutoa original exhaust pipe ba kuweka ya kawaida lakini sioni mabadiliko yoyote. Sasa je utakuwa unafahamu namna ya kuinyamazisha hii kitu. Thanks
Gari nzuri usiwaze sana kuhusu parts dunia imekuwa kijiji
Inawezekana lakini ni complicated kidogo na kwakweli hatuna mafundi wazuri kivile na hubadili exhaust pekeyake bali mpaka muffler
Yaaah awamu ya kwanza walifanya hivyo kama ulivyosema, later wakasema sijui unaweka mashilingi lkn hakuna changes za maana ninaziona. Sasa sijui ni mafundi sio competent enough au laah ingawaje nimekuwa na hawa mafundi nina muda nao mrefu sana katika magari yangu mbalimbali
Unajua hizo ni sports cars na mafundi wetu wengi wana ufundi wa mazoea kwa mfano ishu ya exhaust na huo mngurumo inaanzia kwenye systems za aircleaner na air compression toka kwenye engine
But naona altezza nyingi ni 2000cc na mazda attenza ni 2260cc,so nikadhani mazda attenza inabugia zaidi wese.
nimenunua body used kwaajili ya gari yangu imepata ajali nahitaji kujua jinsi ya kubadilisha maelezo ya kwenye kadi yangu yaendane na hili body jingine toyota kikorola flani old model.
Poa nimekuelewa. Duuuh basi ngoja nivumilie tu maana nisije leta tatizo katika gari ilhali ilikuwa nzima.
Turudi katika ile subaru legacy, maana ulinipa general advice basing on spare parts, je specifically katika masuala haya ipo vipi?
1. Ulaji wa mafuta (niliuliza cc zake nimeambiwa 1990 kama hii altezza niliyonayo)
2. Uimara na kutulia barabarani
3. Service charges zake
4. Kuna any special and unique condition kwa ajili ya hizi gari tu