Swali la ufahamu!
Kwanini LATRA wanatoa mitihani kwa madereva wa mabasi na malori?
LATRA ni mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu (Land Transport Regulatory Authority). Ilianzishwa mwaka 2019.
Huku nyuma kulikuwa na mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA) ambayo iliundwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa. Mwaka 2019, SUMATRA ikagawanywa na kuzaa LATRA inayosimamia usafiri wa nchi kavu na TASAC inayosimamia usafiri wa majini.
LATRA sio taasisi ya elimu. Hata kwenye majukumu yake yaliooanishwa kwenye sheria ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu hakuna jukumu linalofanana na kutoa elimu ya kitaaluma.
Sasa kwanini LATRA wanatoa mitihani kwa madereva?
Je! LATRA wana chuo cha udereva?
Dereva anasoma VETA, kisha anapatiwa cheti cha kuhitimu. VETA nayo ni taasisi ya umma (inaendeshwa na serikali). Baada ya kuhitimu VETA au kwengineko, Dereva anakwenda NIT kuthibitisha uwezo wake ili apewe Leseni ya daraja analostahili.
NIT ni taasisi ya umma inayoendeshwa na serikali. NIT taasisi ya kitaaluma, pale kuna miundombinu ya kitaaluma na wakufunzi wa taaluma ya udereva. Dereva akifika NIT anafanya mtihani wa vitendo na kuthibitishwa, kisha anapatiwa leseni.
Swali! Kwanini LATRA wanatoa mitihani kwa madereva? Ndio kusema VETA na NIT hawaaminiki kwahiyo kwenda VETA na NIT hakuna maana?
Kama VETA na NIT ambazo ni taasisi za elimu haziaminiki, kwa LATRA ambayo sio taasisi ya elimu iaminike?
Kwakuwa hii mitihani inalipiwa; Je! Ni sawa kuitazama kama mbinu ya kutanua vyanzo vya mapato?
Mbaya zaidi, maderava wanadai mitihani hii haina viwango vya kitaaluma kutokana na baadhi ya maswali yanayoulizwa!
Nauliza!
Dr. Chris Cyrilo.