Mada maalum: Tuijadili Tanganyika

Mada maalum: Tuijadili Tanganyika

1759382358010.jpg
 
Si busara wala si uadilifu mnapozungumzia changamoto za Taifa lenu Tanganyika kisha mkawapa lawama wazanzibar

Si busara wala hekima kuwaona wanzibar wote ni wenye makosa kwa makosa ya mzanzibar mmoja

Huu ujinga pia niliuona X, watu mnaweka chuki kwa watu ambao nao kama watanganyika tu wanaathirika kama sisi tunavyoathirika

Lakini tuwe wakweli tu,je matatizo ya wananchi wa Tanzania yameanza hii awamu ya sita tu?

Unapojadili mambo jitahidi sana kuwa objective,kwakuwa objective utayaona mambo katika uhalisia wake lkn ukiwa tayar na Tanganyika yako mkononi lazima uteleta ujinga wa kuwalaumu wazanzibar wote
kwanza nitamlaumu sana nyerere huyu ndio chanzo cha yote.pia rais karume mwenyewe alipo jaribu kuukataa huu muungano alipewa onyo kali
 
JE, MUUNGANO NA TANGANYIKA VIMEBAKIA KUWA MFUPA WAKATI ZANZIBAR INANAWIRI?

Kila mtu anaweza kutafsiri tofauti kazi yoyote ya sanaa ingawa maana iko kwa mtunzi. Tafsiri yangu kwa hiki kikaragosi (katuni) cha Masoud Kipanya ni hii: Skeleton (huyo samaki mkubwa aliyebakia mkia na kichwa) huonyesha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (iliyowakilishwa kama kichwa) na Tanganyika (iliyowakilishwa kama mkia).

Samaki wadogo walionenepeana ni Zanzibar (samaki mkubwa kidogo) na Visiwa vya Unguja na Pemba (samaki hao wadogo) pamoja na visiwa tegemeo ambavyo huunda Zanzibar. Wanaonekana siha au afya yao inatokana na wao kupata lishe kwa kumla samaki mkubwa.

Tafsiri hii katika literature (fasihi) ndio ambayo tunaita reader response ikiwa na maana kuwa msomaji anaweza pia kutoa maana yake katika kazi ya faisihi hasa ambayo mtunzi wake yuko mbali au hawezi kuwa huru kufafanua maana.

Tafsiri yangu inakwenda na muktadha na siku ambayo kikaragosi hiki kimetolewa, tarehe 12 Januari 2026 ambayo ni siku ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Lakini kama wewe huamini katika uhuru wa kazi za fasihi waweza kwenda kumtia pingu Kipanya hata 'kumpilipili' Askofu Mwamakula ambaye ndiye mchambuzi wa kikaragosi cha Kipanya.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandakile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 12 Januari 2026; Saa 12:03 asubuhi.
1768227936756.jpg
 
John Heche anena mazito juu kalia zinazotolewa toka Zanzibar ;
Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara..

Maneno muhimu kutoka kwako:

Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari?

Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika.

Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika.

Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko?

1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar?

2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu,

Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika?

Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara?

Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar?

Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya….

Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu?

Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na hakuna kauli yet kutoka kwa aliewateua… Kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao.

Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?
1781066921403.jpg
 
Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?View attachment 3604787
Hawa siku zote hawawaoendi watanganyika.
Viongozi kutoka Zanzibar ni wengi sana kwenye serikali na wanatibiwa bure kwa kodi zetu,leo hii wanaanza kubagua! Maana yake watanganyika walipo Zanzibar wafe kwa kukosa matibabu!
 
Nimekutana na hii video Vijana wa Kitanganyika walitakiwa kuonyesha vitambulisho vya Uzanzibari kama hawana wanapoteza kazi.
 
Back
Top Bottom