wewe unamkaribia frank xavier?
Tunao waandishi kibao wazuri tuu wa habari za uchunguz, naomba nisiwataje, wasije waka wau uli.
Zamani hata mimi nilikuwa Investigative Journalist, kwa sasa ni producer mostly niko behind the camera ila inapobidi. Ya mwisho nimefanya wakati wa mgomo wa madaktari, watu wamepoteza maisha na hakuna aliyewajibika!, masikini Watanzania kwanza hatujui haki zetu in case of death due to negligence na hata kwa wanao jua, gharama ni kubwa kuajiri wakili na kwa sheria zetu, hatuna pro bono!. Mwisho wa kipindi nilisisitiza lazima serikali iwajibike na kulipa fidia!. Program ilikataliwa na ku end up in my shelves!.
Tukirudi kwenye Isidingo, mimi ni mgonjwa, nilianza na Egoli, sasa niko na Isidingo, nikimiss jioni, kesho yake siondoki home mpaka saa 4 baada ya marudio, nikimisi, nasubiria Jumamosi usiku, au Jumapili asubuhi.
Ninamfahamu hadi mke halisi wa Pearsons, anaitwa Nadipha anafanya kazi Holiday Inn ya Santon town. Studio zao ziko opposite na Millband Hospital alipolazwa Kibanda.
Pasco