Mkuu tuwe pole sana kwa wote!!
Maana hii hali na mie naipitia sasa hakuna kitu kibaya kinachovunja morali na confidence ya mtu kama kuwa jobless,nazungumzia ule u jobless wa kutokuwa na hata mia mpaka usaidiwe na ndugu wema au wazazi japo kajihela cha vocha.
Yaani kila mda unakuwa ni mtu wa kujilaumu tu na kujiwazia mabaya hadi kutamani kutoweka hapa duniani, hususani ukiwa ni mtu ambaye usha struggle sana kutafuta ajira alaf ukaishia kapa.
Hii ni hali halisi nliyonayo kwenye maisha yangu mpaka mda huu ninavyoandika mkuu.
Binafsi nimesoma wala sikupoteza mda katika kusoma vyeti nnavyo vizuri tu lakini linapofika katika ishu ya upatikanaji wa riziki/ajira inakuwa kizungumkuti mpaka ikawa inanipitikia kwenye akili yangu kuwa nina mikosi au nitakuwa nimerogwa mie,makombe nishakunywa ya kutosha nishapitia nyuzi nyingi humu jamii forum za kujitibia mikosi kwa kutumia chumvi ya mawe nimeoga maji nliyoyanyunyiza chumvi ya mawe tena kwa kunuia kwa ajili ya kuoga kama tiba ya kuondosha mikosi ,nimeoga kwa miezi miwili mfululizo huku nikihangaika na utafutaji wa ajira kote bila bila mamaae!!mpk sasa nimeacha najiangalia tu.
Nime develop tabia mbaya ambazo hapo awali sikuwa nazo hii yote kutokana na stress licha ya kulelewa kwenye maadili ya dini....
Naomba nikazie hapa katika ''maadili'' kuwa katika hali ya idle mda wote ni jambo baya sana kwa mtu hii itakufanya uwe na tabia mbaya ambazo hapo awali Hukuwa nazo.
Binafsi nimekuwa mtu wa kutawaliwa sana na hisia za kufanya ngono kila mda bila ya kuangalia hadhi ya mwanamke yoyote malaya hata wale wa bei chee twende!!mpk najishangaa nna nini mimi!!
Kujiunga katika mitandao ya uesharati kuazia magroup ya malaya telegram, WhatsApp..... mitandao kama ya badoo, tinder yaani kiufupi balehe inanipelekesha aisee japokuwa nishavuka katika stage ya ubalehe now na approach 30 tena ila bado ni jobless.
Nimekuwa na tabia ya kutembea usiku mkubwa bila ya kuwa na woga wowote!!

Na sana hupenda kutembea sehemu za starehe au madanguro ya malaya wabovu kabisa,,, dahh aise sitosahau juzi kati nlivyodakwa na askari kwa tabia za uzururaji usiku tena katika sehemu hatarishi ambazo kufa ni kugusa tu.
Hii yote kusaka mbususu tu


( sio la kucheka)
Askari wawili walianidaka saa 7 za usiku wakaniuliza unafanya nini hapa, piga kamba za hapa na pale lakini wapi?
Kila nikijitetea ......

lakini hakukuzaa matunda..
Mmoja wa askari kati ya wale wawili akanionesha picha katika simu yake kijana mmoja alieuwawa kwa kuchomwa visu usiku na wahuni na kufariki karibia na maeneo hayo ya malaya huku baadhi ya malaya wakiwa ni kama wenye woga wakishuhudia live kijana akiuwawa...( Askari akaniambia unaona malaya walivyo muuza jamaa hapa?)
Nilijawa na hofu sana....Nikajiuliza kwenye akili yangu je hii kitu ingenitokea mimi

Na je mama yangu na baba yangu pamoja na ndugu zangu ningewaacha katika majonzi ya namna gani?
Na je mwanangu bado mdogo sana wa miezi kadhaa, baba yake ningefariki katika hali ile angekuwa yatima asiyemjua baba yake kabisa!! So sad

.
Baada ya hapo askari wakanifunga pingu mikononi mwangu akaitwa dereva bajaji aliekuwa akipita njia ili niingie katika bajaji nikajieleze kituo cha polisi , nikaona kisanga hiki wakati hiyo hali haikuwahi kunitokea katika maisha yangu,nikasema hii kweli leo za mwizi arobaini , nikajitia kugoma na kuleta ukaidi , askari alinichenjia kwa sauti ingia kwenye bajaji au unataka tutumie nguvu, nikiangalia mkononi mwake ana mkia wa taa!!!
Dah sitosahau ikabidi nikubali tu kuingia kwenye bajaji, huku njiani nikijiuliza kichwani mwangu hiki nini??
Na je ikiwa kama ni wahuni tu wanaojifanya askari wakija kujifanyia uhuni itakuwaje na mikononi nimefungwa pingu??
Dah sikuacha kujititetea huku bajaji ikiwa katika mwendo omba msamaha kama wote ilimradi tusifike kituoni kesi ikawa kubwa na kuingia aibu, nikijiangalia mfukoni sikuwa na hongo ya kutosha


Huku askari akiniambia kujitetea kwako hakusaidii kitu labda uwe na laki moja!!
Nikiangalia mfukoni nina kama 14k na kwenz ya 200 na pipi za tropical kali


Daah tukafika hadi kituo cha polisi kushuka sasa nikaleta mbinde halmanusura nichapwe ikabidi nishuke na kukubali kuingia kituo cha polisi nikiwa mnyonge kabisa ( kumbuka ni hali ambayo haikuwahi kunitokea maishani mwangu kupelekwa kituoni)
So nlikuwa na hofu ya hali ya juu kwa aibu yangu kufika kwa wazee wangu na mama mtoto wangu Dah nlijilaumu sana nikasema nini hiki!!
Dua kama zote kimoyomoyo!!
Nikatupia macho mule kituoni nikaona vyumba kama vitatu, nikasema kimoyomoyo leo hii ndio nalala humu na pingu mikononi kama mhalifu mtu na elimu yangu, sivuti bangi wala silewi?
Nikafunguliwa pingu nikaambiwa kila nlichonacho mfukoni nitoe niweke mezani, nikatoa kama buku 4 nlizoweka mfuko wa mbele wa suruali pamoja na simu na coins ya 200, huku 10k ikiwa nimebanisha mfuko wa nyuma ya suruali, nikasema hapa wanataka na hii ten yangu waichukue, askari akaendelea kunisachi baadi ya kutoa vile vitu si akaiona na ile ten nikasema nimekwisha hata ya nauli sitokuwa nayo!! Na nikiangalia huko nitokako kuna umbali.
Nikahojiwa jina langu na umri wangu na je nna familia.
Mungu akanipa ujasiri nikayajibu maswali yote waliyoniuliza.
Wakataka vitambulisho nikawaambia vyote nime scan katika simu wakata niwaoneshe ile kutaka kuwaonesha katika screen lock ya simu yangu,ipo picha ya princess wangu mwanagu wa kike, wale askari watatu wakasema kumbe na jamaa ana mtoto kabisa bado anafanya mambo ya kijinga ( kiasi flani picha ya mwanagu ilinitetea kwa kuona kuwa nina familia)
Nikaulizwa una elimu gani nikasema ni degree ya kwanza (bachelor degree) degree gani?
Nikasema degree ya uhandisi ujenzi..( siwatukanishi wahandisi wenzangu ni ujinga wangu mwenyewe).
Wale askari wakasema kumbe hili lijamaa ni lisomi kumbe alaf unaona linavyojielewa vitambulisho vyake na vyeti vyake vyote anavyo kwenye simu alaf ana familia kabisa.
Wakaniuliza unafanya kazi wapi? Hapa ikabidi niseme kuwa bado jobless ila nafanya inten( sehemu flani) hapa ni katika kujitetea nisionekane nipo idle.
Ikabidi wanihurumie na kusema zitakuwa stress tu maana wanawake nao wanazingua huku wakisema hivi vitu havina msomi.
Wakaniachia buku 4 ile ten wachukua nikaanza kupata faraja kidogo katika moyo wangu...
Baada ya hapo nikaambiwa vaa viatu vyako nikavaa na kupewa onyo na tahadhari kuwa nisipende kutembea usiku katika maeneo yale maana kufa ni kugusa tu.
Nikaambiwa huyu bajaji akupeleke nyumbani au utaenda kutulia sehemu salama yaan lounge nikasema wacha nitulie lounge mpk asubuhi saa 12 nikapanda daladala nikasepa.. kufika gheto nimechoka kinyama,nikasema Alhamdullilah nimetoka katika jaribu lile la aibu kabisa... Nikalala mpaka mida mida.
Kupambazuka vyema sikuamini kama nimetoka pale na kujihusia katika nafsi yangu kuwa ujinga ule sitofanya tena na wala sitotembea usiku mkubwa tena. Na Mungu anipe nguvu juu ya kulisimamia maana lile ni pepo lililonivaa mtu utajiaminisha vipi kutembea usiku pekee yako!! Kwani usiku ni wangu??.
Nilichojifunza kupitia mkasa wangu huu ni haya yafuatayo:-
* Kuwa na familia i mean mke/mpenzi(haijalishi umeoa, hujaoa ila kuoa ni vyema zaidi kwa maadili ya dini zetu) ni jambo zuri maana litakuepusha na mengi, maana lau angelikuwepo mke wangu nyumbani pamoja na mtoto wangu nisingelipata ujasiri wa kutembea usiku mkubwa maana ningejiskia noma au nisingekuwepo nae angenipigia simu na kuniuliza upo wapi? Na kujawa na mawivu kibao ningehisi soo na kurudi mapema japo kuwa sometimes tunakerana kwa hii kutokuwa na ramani yoyote just rizki za kuunganisha tu ila hivyo hivyo ananistahmilia maana kwa wanawake wetu wengi wa siku hizi angelikuwa kashanikimbia.
*Mtoto ni faraja na ni neema kubwa sana kutoka kwa Mungu, imagine kuonekana kwa picha ya mtoto tu nikonekana ni mtu mwenye kujielewa kwa kuwa tayari nina familia as well well as well educated.
Na personality au mavazi nayo hukuheshimisha au hupunguza ukali wa kesi inayokukabili (hutegemea na kesi i.e sio kuuwa au kubaka na nyengine kesi za jinai) nazungumzia hizi kesi ndogo ndogo. Nimekuwa mtu wa kujiweka maridadi licha ya ujobless wangu.
*kuweza kuzidhibiti nafsi zetu hata kwa ukubwa wa matatizo tunayoyapitia na kuzindle stress zetu maana majuto ni mjukuu maana likishakutokea baya la kukutokea shida utawapa wazazi wako na familia yako.
* Wanaume pindipo tutakapofanikiwa tukumbuke nyuma tulikotokea ( wazazi, ndugu, familia) mke/mpenzi tulio struggle nao katika shida bila kutuwacha mkono wakati wa shida,, maana mke/mpenzi anaekustahmilia wakati wa shida bila ya kukimbia huyo ndio mke sio ushafanikiwa ndio unawaona wakina paula hao wakukuchuna tu hawana mapenzi na wewe kabisa,na mke unaeanza nae wakati huna kitu huyo ndie mke maana kakupenda katika hali hiyo hiyo uliyo nayo.
** Mwanaume rijali na unaejielewa tafuta mke/mwenza unae endana nae katika maono sio kuangalia uzuri wa sura na umbile tu maana sura na umbo huchakaa mwanamke ni upendo, ustahmilivu, kukuliwaza wakati wa shida huyo ndio mwanamke.
** Na ndio maana baadhi ya nyadhifa hupewi kama huna mke/mume kama uraisi kama huna mke/mume utaonekana ni muhuni tu.
Nimeona ni share nanyi mkasa wangu huu kwa wanangu wa JF kama funzo kwa vijana wenzangu na majobless wenzangu kuwa mwenye kutafuta hachoki na akichoka ujue amepata.
Samahanini sana kwa gazeti
Nimemaliza