Machozi ya Dkt. Mpango yasiende bure

Feb 18, 2019
34
400
Kwanza naomba nianze kwa kumpa pole Dkt. Philip Mpango kwa kupambania afya yake kwa hizo wiki 2. Mungu amjalie apone kabisa mapema ili aweze kujumuika na familia yake.

Tukirudi kwenye mada, kwanza kama hujaitazama ile interview nenda youtube ukaitazame ndipo urudi hapa kuendelea kusoma. Kama haujaumwa au haujamuona anayeumwa hii nimonia kali tuliyonayo kwa sasa unaweza usielewe ukatili wa kirusi cha corona.

Tumshukuru Dr Mpango kwa kufanya ile press conference,nadhani sasa watu wataelewa na wote tutazingatia njia za kujikinga na hiki kirusi. Waziri ametoa chozi hadharani sio kwa sababu nyingine bali ni kwa sababu ameponea chupuchupu. Hii nimonia kali haifai kabisa, omba isikukute.

Machozi ya Dr Mpango yawaamshe usingizini viongozi wetu na wajue kwamba this life is precious to everyone, hakuna asiyependa kuendelea kuishi, kila uhai unatakiwa kuthaminiwa na kupewa ulinzi wa hali ya juu. Hivyo wachukue hatua sahihi zinazohakikisha kila mtu analindwa na hatari yoyote.

Dr Mpango amesema alikuwa anaishi kwa mtungi wa oksijeni nyumbani. Baadaye akahamishiwa hospitalini ambako amekaa kwa wiki 2 akipumulia oksijeni. Sasa tujiulize ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kununua mitungi ya oksijeni na kukaa nayo nyumbani pindi wanapoumwa?

Ni wachache sana hata asilimia 1 haifiki. Kwa muktadha huo njia rahisi na nyepesi ya kuepuka kufika huko ni kwa kuchukua tahadhari. Kinga siku zote huwa ni cheap kuliko tiba.
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
2,442
2,000
Magufuli ulitumiwaje SMS namtu anapumulia machine. Lakini mpango hata ungelia utoe machozi damu.mpo mnashinda na jiwe kwann hammshauri.Ila umenyooka.tujiulize kwamaskini mwezangu wa Chunya.
 

wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
2,296
2,000
Naomba kujua kichwa cha habari niipate youtube. Nadhani sasa atavaa barakoa haijalishi yuko wapi na yuko na nani.
 

mttupolli

JF-Expert Member
Feb 9, 2019
419
500
Hivyo wachukue hatua sahihi zinazohakikisha kila mtu analindwa na hatari yoyote.

Ina maana watu hatuwezi chukua hatua wenyewe mpaka tushikiwe fimbo?
UK USA na KN mbona wameswagwa kufanya hili na lile na hakuna walichofanikiwa??

Ombi langu kwa raisi wetu mpendwa:-

Endelea hivyo hivyo na misimamo yako. Kwani hakuna ujanja katika hili.
 

DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,139
2,000
Kwanza naomba nianze kwa kumpa pole Dr Philip Mpango kwa kupambania afya yake kwa hizo wiki 2. Mungu amjalie apone kabisa mapema ili aweze kujumuika na familia yake...
We unadhani tahadhari gani ichukuliwe kujiepisha na hii airborne disease?
 

DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,139
2,000
Hivyo wachukue hatua sahihi zinazohakikisha kila mtu analindwa na hatari yoyote...
We ndo umemaliza kila kitu, watu kelele nyiingi ...tahadhari tahadhari wakati wanaochukua tahadhari huko duniani goma linashika kazi,this is airborne disease how can you get rid of it?
 

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,272
2,000
Mungu amjalie uponyaji, angalau atakuwa ndo chanzo cha mabadiliko kwa viongozi wengine kusema ukweli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom