Mzingatie sana tusije tukaangamia kwa Corona'' - Dkt. Mpango

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameendelea na ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma, ambapo katika moja ya hotuba zake amewataka wananchi kuchukua tahadhari.

MPANGO-WEB.jpg

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango
Dkt. Mpango amewasisitiza wananchi wa eneo hilo kuendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa wa Corona.

''Corona Wimbi la tatu limeshaingia katika mkoa wetu wa Kigoma. Kati ya mikoa 10 yenye wagonjwa wengi na Kigoma imo. Kabla ya tarehe 10 mwezi huu wa saba tayari tulikuwa na wagonjwa 18, na wimbi hili linaonekana kali kweli, hivyo mzingatie sana maelekezo tusije tukaangamia'' - Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais.

Aidha amewaagiza viongozi wa serikali kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwani mkoa wa Kigoma unatajwa kuwa kati ya mikoa kumi inayoongoza kwa maambukizi nchini.
 
Inapendeza kuitaja na hiyo mingine ili kuwakumbusha wananchi walioko huko kwenye hiyo mikoa tisa iliyobaki sawia na hao wanaohutubiwa, in other words hotuba moja iwakumbushe mikoa yote kumi mihanga badala huo mmoja unaotembelewa na kiongozi
 
Viongozi wetu wanaogopa kutoa takwimu sahihi zinazohusu visa vipya vya maambukizi na hata idadi ya vifo. Sijui hofu yao inatokana na nini!? Hawatambui ya kuwa mficha maradhi kifo humuumbua.

Ni vyema wakafunguka na kuwa wawazi kuhusu hali halisi ya gonjwa la UVIKO 19 hapa nchini. Inawapasa kufanya hivyo tena mara kwa mara ili wananchi wapate picha halisi na kuchukua hatua.

Nafikiria hatua za dhati tafadhari zilizochukulia wakati wa wimbi la kwanza na kidogo wakati wa wimbi la pili ndivyo ambavyo inapaswa kufanyika. Hizi "mere words" kutoka kwa viongozi wakuu hazitatufikisha popote pale zaidi ya kuja kujikuta tupo kwenye maangamizi mithili ya yale yaliyojili kule nchini India.
 
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameendelea na ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma, ambapo katika moja ya hotuba zake amewataka wananchi kuchukua tahadhari.

MPANGO-WEB.jpg

Dkt. Mpango amewasisitiza wananchi wa eneo hilo kuendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa wa Corona.

''Corona Wimbi la tatu limeshaingia katika mkoa wetu wa Kigoma. Kati ya mikoa 10 yenye wagonjwa wengi na Kigoma imo. Kabla ya tarehe 10 mwezi huu wa saba tayari tulikuwa na wagonjwa 18, na wimbi hili linaonekana kali kweli, hivyo mzingatie sana maelekezo tusije tukaangamia'' - Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais.

Aidha amewaagiza viongozi wa serikali kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwani mkoa wa Kigoma unatajwa kuwa kati ya mikoa kumi inayoongoza kwa maambukizi nchini.
tahadhari zipi sasa zichukuliwe mkuu, mbona yeye haja vaa barakoa
 
Back
Top Bottom