Machozi ni suluhisho la matatizo ya mwanamke?

Machozi ni suluhisho la matatizo ya mwanamke?

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,092
Reaction score
34,904




​
Wanawake wengi sana wamekuwa wakilia pindi wanapo pata matatizo, wameshindwa kuvumilia yale yanayotupata, mfano wengine huniambia tunawaambia wakilia wana machozi ya promotion.

Hii pia nimeiona kwa wanawake wengi, wanalia weeeeeeee, wakinyamaza wanaona kama wameshatua mzigo kwa kiasi fulani, kama ni hasira basi wanaona imepungua kwa sehemu.






Utakuta mtu anatafuta na private place, anajifungia kama ni chumbani peke yake, analia kwa uchungu sana, na anaweza kuchukuwa muda mrefu sana kwa kulia.






but problem inabaki pale pale




hali hii humfanya mwanamke kuwa mpweke sana kwa muda mrefu,



mwingine hataki kubembelezwa hata kidogo, yani ukimbembeleza ni kama umemwambia azidi kulia





​
Mwingine akitoka kulia huwa na hasira sana, atapiga watoto, usimsemeshe, anaweza kukupa jibu moja tu, ukanyanyua mikono juu.

Lakini tatizo linakuwa palepale, sasa hebu tusaidiane kushauriana juu ya hili, je inawezekana mtu kuiacha hali hii??? na utaiachaje? ili ukipata tatizo usilie tena?


 
Hata ningeambiwa kuna dawa ya kunifanya nisilie nikiwa na matatizo nisingekubali kuitumia,kulia kunanisaidia sana.
Nikilia vizuri then nikanyamaza nitaweza kutoa maamuzi mazuri zaidi.
Kama ni mtu yuko around ndio aliyesababisha nikalia,akae tu mbali na mimi maana nitamfurahisha nikitoka hapo!!!!
 
hili swala si kwa wanawake tu hata kwa wanaume mfano ukifiwa na mtu mwenye thamani kubwa kwako, kama wazazi, mke au mtoto usijizuie kulia kwani kulia kunakupa nafuu kubwa sana kuliko kukomaa na maumivu tu moyoni.

ila ziko angle mwanaume hupaswi kulia kama kutoswa na demu na vitu vya namna hiyo.
 
machozi yanasadia kupunguza maumivu ya moyo na unajistukia unalia haiwezekani kuzuia hii hali ingawa wengine wanaitumia vibaya
 
kwani kuna shida gani mtu akilia MziziMkavu mpaka tutafute dawa ya kuacha kufanya hivyo?
Hiyo tabia inakuudhi, au kukufanya ujisikie vibaya?
Mi naona mtuache tu tulie tukimaliza mambo yanaenda sawa.....
Kama nimeudhiwa, kulia kunanifanya nipunguze hasira. Kulia ni kiburudisho kizuri sana cha moyo, badala ya kufanya mashambulizi ni bora ulie ili ujitulize......
Kama nimefurahishwa, sijui kwa nini huwa nalia, najikuta tu nimejawa na donge na machozi yananitoka. yaani mtu akinifanyia kitu kizuri, hasa kuonyesha ananijali saaaanaaaaa huwa nalia.
 
Last edited by a moderator:
nikiwa na hasira nakuwa na kitu kama donge limenikaba kooni, nakuwa siwezi ongea wala kufanya kitu chochote productive. ila nikilia na machozi yanavyotoka nahsi kama yanayeyusha kile kitu kilichonikaba kooni.
baada ya hapo hata sijuagi usingizi unatokaga wapi ila kinachofata ni kulala na nikiamka nakuwa fresh kabisa.
 
Back
Top Bottom