Machozi ndani ya daladala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machozi ndani ya daladala

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mubezi, Oct 11, 2010.

 1. Mubezi

  Mubezi Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nikiwa kati ya WATU waliohudhuria mikutano ya kampeni hasa ya urais,nimeona mengi,nimesikia mengi,ahadi kemkem,tam,nzuri na zenye kuvutia na kama JK,SLAA au LIPUMBA mmoja wo akishinda na kutekeleza ahadi zake basi TANZANIA itakuwa kama Boswana au kama sio kuifikia Afica kusini. Sina sababu ya kuzitaja ahadi kwani wengi wenu mwazijua.

  Ni saa 12:30 za jioni siku ya ijumaa,natoka ofisini kwangu JMOO nakwenda posta ili kupanda gari la kuelekea mbezi nyumbani kwangu(mbezi ya kimara).Abiria ni wengi kama kawaida,wezi wamo,ila kuna magari ya kwenda mbezi ya buku(elfu moja) naingia na muda si mrefu gari inajaa na kuondoka,wote tumekaa,foleni ni kama kawaida kwani inaanzia faya na uku gari ikiwa imewekwa radio moja ya chama tawala.Watu tupo kimya na aliyesimama ni konda tu.

  Mara hiyo radio ikaanza kutangaza sera za mgombea uras wa chama tawala,ahadi nyingi,kile mara iki najua mwazijua sina shida ya kuzitaja ila ni moja tu ambayo nitaitaja ambayo imenipelekea kuandika UJUMBE huu kwenu,ni ile ya KUNUNUA BAJAJI 40 KWA WAMAMA WAJAWAZITO,hapo ni saa 1:30 za jioni na hatujavuka magomeni.

  Mara baada ya huyo mgombea kutaja iyo ahadi,nikasikia sauti kuoka nyuma ya gari ikisema “ZIMA RADIO YAKO AU BADILISHA STESHENI”ni sauti ya kike tena mwanamama mjamzito.Dereva alizima radio,tukawa kimya kila mtu nahisi alikuwa anajiuliza kwanini huyu mama kasema radio izimwe au ibadilishe stesheni,ukimya ulitawala kama dk 15.Tukiwa tunaanza foleni ya ubungo pale mahakama ya ndizi au bigbrother, na ikiwa ni saa 2:07 za usiku,nikasikia sauti ya mwanamama mwingine(sio mjamzito) ikisema “KAMA MIMBA ZINGEKUWA ZINABEBWA KWA ZAM HUYU KIKWETE ASINGETAMKA MANENO HAYO”nikashtuka nikageuka nyuma nikakutana uso kwa uso na yule mama mwenye mimba,mimba yake ilikuwa ni kama ya miezi nane tena ilikuwa kubwa(namaanisha tumbo ni kubwa sana).

  Tukiwa tupo stand ya mkoa na gari likiwa limesimama na ni saa 2:45 usiku kumbuka nimetoka posta saa 12:30 za jioni.Yule mama mjamzito akasimama akaanza kusema “MIMI SITOMPA KURA KIKWETE KWA JAMBO ILI,NILIKUWA NIMPE ILA KWA JAMBO KAMA ILI SIWEZI KUMPA”uku akilia na kutokwa na machozi,yule mama mwingine aliyesema “kama mimba zingekuwa zinabebwa kwa zam huyu kikwete asingetamka maneno hayo” akaanza kumbembeleza yule mama mjamzito akimsii akae.Nilimtazama kila mtu ndani ya gari sura zilibadilika zikawa sura za majonzi.

  Nikatoka kwenye daladala(kimawazo) nikaleta taswila ya BAJAJI nikamuweka yule mama nyuma na mimi nikawa dereva,nikafikiria umbali wa kilometa 50 toka kijijini kwetu kule kanyigo kuja hospital,barabara imejaa mashimo,nikawaza tumbo la yule mama akiwa yuma na uchungu na babaji ikiwa inayumba kwenye mabonde ya barabara,”NILILIA” nilishutushwa na honi nyingi za magari ambazo zilikuwa zikilipigia daladal letu kwa kutotembea, kwani kila mtu alikuwa kwenye mawazo ya yule mama(naisi) na dereva alijisahau kwa kumuonea huruma yule mama.Nilikuwa karibu na dereva nikamuuliza vp?,akajibu “WE ACHA TU”uku akitoa leso na kufuta machozi na kuanza kuendesha gari.

  Ni saa 3:07 usiku tupo kimara tunaanza foleni ya kimara stopover,watu wote wapo kimya akuna aliyeshuka mpaka sasa na konda kaka kwenye mlango ameinama,kila mtu kainama,uku wengine wakivuta mafua,na yule mama mjamzito akionekana ana asira na uku machozi yakimtoka yenyewe.Nikajiuliza ina maana watu wote tunakwenda mbezi?,pia huyu mama vp mbona kabadilisha kila mtu ndani ya daladala? Katumwa nini?.Nikasikia sauti ya baba mmoja kutoka katikakti ya gari akisema shusha konda hapo,konda akasema wapi?,baba akajibu hapo hapo,Mmmmmmmmm?,”Samahani konda nilikuwa nashuka bucha nimejisahau” alisikika yule baba akisema,Mmmmmmmmm?.Ndipo nilipoona kila mtu karudi katika hari yake ya kawaida na wengine wakashuka hapo kama watu sita hivi.Nikajiuliza je walikuwa wanawaza nini? Mpaka wapitishwe kituoni?.Je walikuwa katika taswila kama yangu?,au uchovu wa kazi?

  Kati ya wale walioshuka pale njiani(sio kituoni) baba mmoja akasema akimwambia yule mama mjamzito “POLE SANA MAMA NA MIMI NAKUHAIDI SITOMPA KURA KIKWETE”akatelemaka.Tunavuka stopover na ni saa 3:30 usiku,kila mtu kaanza kusema lake”KIKWETE HANA AKILI”alisikika baba mmoja,”KIKWETE NI MGONJWA” alisikika dada mmoja,”WANAIGEIZA NCHI YA FAMILIA KWANI HAPA TUNATAWALIWA KIFALME” alisikika kaka mmoja.Ni saa 3:45 nashuka kibanda cha mkaa na niliposimama nikwaambia abilia “HUYO NDIO RAIS WENU HATA KIWA CHIZI SI MLIMCHAGU WENYEWE” nikajibiwa na konda “SHUKA UKO NA NENDA ZAKO”,Mmmmmmmm ata konda?

  Nikiwa njiani nakwenda kwangu nikawa natafakari “JE YALE MACHOZI YA MAJI YALIYONDONDOKA NDANI YA DALADALA LEO”je ni ya bure tu?,na je “IPO SIKU YATALIPWA”?,na je “IPO SIKU YATAGEUKA KUWA NI MACHOZI YA DAM”? nisingependa ilo tafakari langu la mwisho litokee.

  Je wewe unatoa machozi gani au maneno agani?,je machozi ya furaha? Au ya uzuni kama yule mama mjamzito?au maneno ya kumtukana rais wako kama wale watu kwenye daladala.Kazi kwako. Nikipata nauli kabla ya UCHAGUZI nitakwenda kanyigo nimuulize babu “JE BABU UMESHAWAI KUONA KICHUGUU CHA SENENE”?.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wakati yeye anatembela V8 wateja wake anataka watembelee BAJAJ what a shame!
  Angalau angesema tutanunua cruza mkonge,BAJAJ si za kwenye rami tuu
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  Nchi nzima ndivyo hivi sasa inavyomwona JK na D-Day atukabidhi nchi yetu bila zengwe
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  si ndo mnachositahili jamani! mnataka nini tena hadhi yenu ya bajaji tuu!
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  So sad...
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  yani mwaka huu...chichiem lazima waibe kura tu!vinginevyo wametolewa nje!!
   
 7. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  hata mimi machozi yamenidondoka,naahidi sitompa kukwete kura yangu
   
 8. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hata mi simpi ng'oo!!
   
 9. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kikwete
   
 10. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hata mm simpi kura yangu,nikifikiria kwa undani zaid yani ni unyanyasaji wa kinyinsia yy atembelee v8,mama zake waliomza awape bajaj ni ukatili mbaya sana kweli oct 31 jk imekula kwake
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma mkuu. Hata mi machozi yamelenga machoni. Lakini nauliza, mbona ile makala yako ya mkutano wa moro na mama wa ndizi ulitumia kiswahili fasaha kuliko makala hii?
   
 12. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Am happy that Big percentage of Intellectuals Don't like him.
  It has even be proven here. mwenye kutaka proof nitampa
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Rais wangu anapenda kucheka-cheka
   
 14. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Du! Kama move story ila ndo ukweli wenyewe.
  Jk kubaki ikulu achakachue tu ila damu ikimwagika kila atapoenda itamfuata.
   
 15. h

  hagonga Senior Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kweli
   
 16. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi wajameni mi nilikuwa ninafikiria, mfano tukisema tujitolee kufotokopi hiki kisa ambacho ni cha ukweli kabisa na kusambaza nakala zake bure kwa wasomaji .....itakuwa tumetenda kosa???? ushauri jamani!!!!!!
   
 17. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mubezi,

  BIG UP sana kwa simulizi yako nzuri. Pamoja na kero za ahadi za kusimu, hili la kutoka Posta saa 12.30 jioni na unafika nyumbani (umbali usiozidi 30km) saa 4.30 halionekani kuwa ni tatizo ambalo wala halihitaji miujiza kulitatua, kabla ya matuta ya barabara ya morogoro, tulikuwa tunatumia si zaidi ya masaa mawili kutoka posta hadi Kibamba lakini tangu wakati ule sasa tunatumia mpaka masaa matano na katika ahadi zote za kuzimu hii bado si kero na haijaadiwa kutatuliwa
   
 18. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,754
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Rais gani wimbo wa taifa unamgomea???
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  nimemfikira huyo mwanamke mwenzangu yupo kwenye foleni muda wote huo mfano tu uchungu ungempata ghafla na hayo mafoleni cjui ingekuwaje, khaa hii nchi inakera kweli, yaani unatoka ofcn saa 1:30 unafika nyumbani 9:45, mtoa thread umeandika kwa hisia kweli...inaumiza sana!
   
 20. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kumchagua JK ni kujiwekea laana juu ya nchi kwa niaka mingine mitano.Yeye benz 300ml kwenye lami. mama mjamzito bajaji 2mil. kwenye vumbi+mashimo.
   
Loading...