Elections 2010 Machozi ndani ya daladala

Mwenye contacts za Dr Slaa na meneja wa kampeni wa Chadema awapelekee haraka hii habari ya mama mjamzito kulia kwenye daladala sababu ya uchungu na hasira ya kuambiwa na Kikwete eti wajawazito watanunuliwa Bajaji. Hii hoja itawaongezea Chadema kura kibao. Huu ujumbe usisitizwe kila kampeni ya Chadema kuanzia dakika hii hadi mwisho wa kampeni. Ujumbe ukishamfikia Dr. Slaa na Baregu na Chadema kwa ujumla tujulishwe jamvini. Ni hayo tu.
 
Such a moving story. Shida tuliyonayo watanzania wengi, bado hatujagundua nguvu ya kura zetu kwenye kuleta mabadiliko na tunaona kama umasikini ni sehemu ya maisha yetu.

Ndio maana watu wakiambia kwamba inawezekana kuwa na maisha bora zaidi wao wanasema 'haiwezekani'...
 
Machozi (mateso) ya mwenye haki ni mengi lakini bwana humponya nayo yote. The day is coming kama sio leo? kesho, lakini siku ipo. Ashukuriwe Mungu afanyae mambo kwa wakati, aonae hata yaliyofichaka, asemaye imetosha.
 
Bei halisi ya Bajaji ni 500,000. Hizo bei za 2 or 3M ni za uchakachuaji. Kodi na faida kwa wahindi to
 
:A S 13: Mi pia mchozi umenilenga lenga, sijui JK anafiiri kwa kutumia ubongo au udongo, Pole mama mtarajiwa huyo ndio rais wako bwana muombe Mungu amtoe duniani asiwe rais maana akiwa hai sisiem watiba hizo kura warudi madarakani, na huyo mchanga aliye tumboni kwako amesikia kilio chako naamini hata chagua CCM kabisaaaaaaaa enzi zake zikifika.
 
Ile message ya kumchafua Dr Slaa ni ya JK kwani nimemsikia Songea jana akisema "mtu anaetaka damu imwagike msimchague", haya maneno yanaendana sana na yale yaliyoko kwenye message. Tutalia sana mwaka huu. Uchaguzi ukiwa huru na haki harudi huyu mtu, hata wanaomchekea chekea wamemchoka, na kura ni siri ya mtu.
 
Du Mubezi, hii nayo kiboko. Hivi Mubezi huyu jamaa hajakutafuta bado? Ningekuwa mie ndo Rais, Mubezi ungeingia kwenye washauri wangu wa mambo ya Habari. Naunga hoja mkono wa ndugu mmoja aliyependekeza kutoa copy ya hii hadithi ya kweli na kuisambaza. Mimi nimeshatoa copy 100 na kuzisambaza maeneo ya Ubungo stand ya mkoa. Nina uhakika haina shida.
 
Si afadhali huyu mama anayo nauli amepanda daladala na bila shaka atajifungulia zahanati au hospitali? Mambo ni mabaya sana vijijini kwa akina mama kama huyu. Lakini ndio hivyo. Watanzania kwa CCM na JK ni kama MBWA anayekabiliana na CHATU uso kwa uso! Come October 31st, JK 81%, Dr Slaa 9%,......
 
Another sad story...nimelengwa na machozi tena....kumbe huyu ndie mwandishi wa mama muuza ndizi ifakara??? so outstanding mkubwa.
 
Hata leo kuna hoja kamahiyo iliibuka kwenye daladala kutoka tabata kwenda posta, tumetumia zaidi ya masaa mawili watu wamechoka,joto kali konda kadata basi ni hasira kwa kwenda mbele, ndipo mtu mmoja kasema '' kwa hali hii watu bado wanatoa kura kwa ccm'' kila mmoja kaja na lake wengine wanasema hatudanganyiki pamoja na mameseji ya kututisha, kila mtu anatoa simu yake na kuonyeshana zile meseji za kumchafua dr Slaa.

Chamsingi watu wengi washachoka na ccm, imebaki huko vijijini sana, watu hawasikii kuhusu ccm, Chadema tufanyeni kampeni za kukata nashoka sasa maana ccm wanachafua hali ya hewa. Kikwete naye anahubiri kumwaga damu nani kamwambia kunamgombea anataka kumwaga damu? wamekosa sela, ahadi zimewaishia wameanza vitisho, walianza na redet, wamekuja navitisho vya kumwaga damu, wamekuja synovete sijui leo watakuja na nini? kampeni chafu zimeanza huku wao wakihimiza ustaarabu.

Tuamkeni zimebaki siku chache sana, chadema nunueni air time kwenye radio na tv. wanataka chadema waache kuhubiri sera zao ili muanza kujibu tuhuma kuweni makini. by the way where is Mpendazoe, afanye kampeni hata kwenye madaladala asubuhi panda basishuka kituo cha pili panda lingine hivyo hivyo. kampeni si lele mama.
 
Hivi huyu Mkuu amewahi kupanda bajaji? nimatusi sana katutukania mama na dada zetu na ana lengo la kufanya taifa liwe la matahira watupu ili familia yake watutawale kirahisi!, hivi mtikisiko wa bajaji kwenye barabara za vijijini licha ya kumsababishia mama mjamzito kujifungua kabla ya wakati siunaweza pia kumsababishia mtoto atakae zaliwa apate mtindio wa ubongo?

UNAJUA MTU KAMA RAISI LAZIMA AFANYE CONSULTATION NA WATAALAM KABLA YA KUTOA AHADI AMBAZO HAJUI Madhara yake, HUU aliouonyesha sasa ndio UROPOKAJI, kutoa ahadi bila kuzingatia outcome, kwani WASHAURI Hana?.

Chagua DR Slaa.
 
Kwa mara ya pili wakati nasoma post hii ya Mubezi nimetokwa machozi. Mara ya kwanza ni ile post yake tena ya mama muuza ndizi wa Ifakara.

Asante Mubezi kwa utaalamu wa uandishi wa kugusa hisia.

Lakini la msingi ni taarifa hii yenye kugusa uhalisia wa maisha ya kila siku ya watanzania. Ni wazi kuna watanzania wengi wanaotoa machozi kila siku kwa sababu ya adha ya uongozi wa CCM uliojikita katika ubinafsi na ufisadi wa mali ya umma.

Ee Mungu usikilize kilio cha watu wako, tunaomba tuondokane na huo uongozi dhalimu kwa awamu ya 4......
 
Inasikitisha. Ee Mungu tusaidie waja wako tuelewe maana halisi ya maisha hapa duniani. Usimtende mwenzako usivyotaka wewe kutendewa. Viongozi wa TZ mbona hivi?
 
Ahamishe nafsi.tufanye mama salma ndo mjamzito,halafu amebebwa kwenye bajaji,yeye Kikwete angejisikiaje.???????
 
Inasikitisha sana,ila kila kitu kina mwisho wake,
hao watalia na kukumbuka yote waliyoyafanya,
Hayati Nyerere alisema:

Ole wako Tanzania ;
Tusipoisaidia!
Niwezalo Nimefanya,
kushauri na kuonya,

Nimeonya Tahadhali,
Nimetoa ushauri,
Nimeshatoka kitini,
Zaidi nifanye nini?

Namlilia Jalia
Atumlikie njia
Tanzania ailinde
waovu wasiivunje

Nasi tumsaidie
Yote tusiya mwachie
Amina tena Amina
Amina Tena na Tena.
 
wana jf tuache kulalamika kwani tumeyataka wenyewe sasa munambiwa ari zaidi kwanza anaumwa sijui kama 5 itaisha salaama uchungu nilionao mie hata huo hautoshi huku kijijini kwetu watu hoi lakini hakuna lolote wanategemea wizi na hilo ndilo tegemeo lao,wajinga siku zote hasara ndiyo yao
Pole sana mama
Conquest-kwani lazima kutawala miaka 10 tusimchague:decision:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom