Macho yangu yananidanganya?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,510
Mimi si kipofu wala si kiziwi.

Uwezo wangu wa kuona na kusikia upo juu.

Hivi hiki ninachokiona kwa macho yangu na kukisikia kwa masikio yangu ni uongo?

Nina maruerue labda? Hayo ninayoyaona ni mazingaombwe?

Kwa nyomi hizi zinazojipanga barabarani mwili wa Rais Magufuli unapopitishwa ndo tuamini kweli alikuwa anachukiwa sana na watu walio wengi zaidi?

Nahisi kuna watu wanakabwa na mafundo kooni wakiziona nyomi zimejipanga mabarabarani jijini Dar [na bado huko kwingine] zikimpa heshima za mwisho mwana udongo huyo. Hawa watu si aiabu wangependa kuona watu wachache wanaojitokeza kumuaga. La hasha.

Huwezi kupendwa na wote. Lakini pia, Rais hakuwa anachukiwa na idadi kubwa zaidi ya watu.

Licha ya mapungufu yake mengi, watu wengi walikuwa wanamkubali, hata kama si waziwazi. Na haitochukua muda watu wataanza kum miss.

Hii ni Manzese leo wakati akielekea uwanja wa Uhuru. Huyu ndo mtu anayechukiwa na watu?



Hapa ni Mwenge jana jioni mwili ukirudishwa spitali ya Lugalo. Huyu ndo mtu aliyekuwa anachukiwa? FOH.



Hapa ni jana jioni kwenye daraja la Kijazi.



Kote huko anapita. Hakuna vurugu. Watu wanamuaga kwa heshima kabisa.

Yawezekana wapo wachache wanaomtukana au kufurahia au vyovyote vile wajisikiavyo, lakini kwa hiki ninachokiona kwa macho yangu na kukisikia kwa masikio yangu, bado sijashawishika kwamba Rais Magufuli alikuwa anachukiwa na watu walio wengi.
 
Mambo ndo hayo sijui wa DW na BBC watasemaje
wasafitv_1616321654691578.jpg
wasafitv_1616321654691400.jpg
wasafitv_1616321806941293.jpg
wasafitv_1616321806968424.jpg
wasafitv_161632180697065.jpg
wasafifm_1616321860002320.jpg
wasafitv_1616321806970613.jpg
 
Niseme tu pia kuwa sipendelei mwili wake kuzungushwa zungushwa sehemu tofauti nchini, lakini naelewa.

Ila, if Dar is anything to go by, this guy was loved!

Leo mabodaboda wameongoza msafara wake kwenda uwanja wa Uhuru, tena kwa amani kabisa.

Wala hawakubugudhiwa na Askari.
 
Back
Top Bottom