Macho ya Bundi

Macho ya Bundi

[h=1]Macho ya Bundi- 20-[/h]ILIPOISHIA
Nilimuangalia mume wangu huku nikitokwa na machozi. Nilijaribu kusema jambo lakini ulimi ulikuwa mzito. SASA SONGA NAYO...


MUME wangu aliamua kujilaza kwenye kochi kisha kunitaka niwe karibu naye ili aniambie jambo. Nilipomsogelea alisema nisijali kwani maneno ya yule mwanamke, yaani Mei yasinitie wazimu.
“Kwa nini amenidhalilisha?”
“Yule Mei japokuwa ni mkwe wangu sitataka akanyage hapa tena.”
“Unasema kweli?” nilimuuliza mume wangu.
“Nakuapia. Hakanyagi hapa. Ninachowaza ni mtoto wangu tu maana bado ni mdogo na najua hana uwezo wa kumtunza.”
“Nikuambie jambo?”
“Sema.”
“Yule amefanya hivyo kwa kuwa anataka mtoto wako amfanye mtaji, yaani apate matumizi ya kila siku kupitia mwanao…”
“Thubutu, hapati kitu hapa!”
Mara tulisikia breki ya gari ambalo lilisimama nje ya nyumba yetu. Nilichungulia na kumuona Mei akitoka huku uso ukiwa umevimba.
Aliingia ndani bila kubisha hodi.
“Nimegeuza gari. Njiani nimemuuliza Pili kama umetoa fedha za matumizi ya mtoto akasema hujatoa, nikamuamuru dereva ageuze gari.”
Tuliangaliana mimi na mume wangu kwa kuwa hayo tulikuwa tukiyazungumza dakika kama mbili zilizopita. Mume wangu aliinuka na kukaa kwenye kochi huku akiwa amekunja uso, aliniangalia nami nikakunja uso.
“Lakini Mei kwani wewe ni mke wangu? Hayo mambo angefanya Pili siyo wewe.”
“Mimi nahusika mia kwa mia, kwani Pili anakwenda kukaa kwa nani?”
“Pili kwenda kukaa kwako ni wewe umejitakia, kwani mimi nimeshindwa kumlea?”
“Kwa maana hiyo unataka kuniambai hutoi?”
“Kwako Mei sitoi hata senti tano. Hapa umemchukua Pili kwa nguvu hata muda wa kumpa hizo fedha ingekuwa saa ngapi”
“Kwani kutoa fedha kunahitaji winji, kalete hizo fedha tuondoke zetu.”
“Nakuambia nenda kwenye gari na ukabaki na mtoto kisha mtume Pili aje hapa nimuelekeze cha kufanya.”
“Yaani unaniamuru kwamba niende nikamchukue mtoto ina maana unanigeuza mimi ni yaya siyo?”
“Hapana.”
“Sasa kwa nini unasema niende kwenye gari nikampakate mtoto, unanivunjia heshima Bwana Chinchi kuwa umemzalisha mwanangu?”
“Huyo ni mke wangu, wewe ulitaka nizae na nani?”
“Na huyo mkeo wa kwanza.”
Baada ya kusema hivyo alinitibua nikasimama na kutaka kumuendea pale alipokuwa amesimama lakini Chinchi mume wangu akanizuia.
“Hebu niache, nikamfundishe adabu huyu pimbi.”
“Nani pimbi.”
“Wewe pimbi, sasa hivi umeponea tundu la sindano na umerudia tena kosa lilelile, sasa nakuua kabisa.”
Wakati nasema hivyo Pili aliingia ndani huku akiwa na mtoto wake.
“Mama, sasa hivi ulikuwa umezimia na unarudia tena kutaka kugombana na mama mkubwa, unafanya vibaya mama.”
“Sifanyi vibaya, mimi napigania haki zako, huoni kwamba huyu bwana anataka kukutesa?”
“Hapana mama, mambo yangu na huyu bwana tuachie wenyewe tutayamaliza.”
“Acha kunifundisha cha kufanya, kosa mimi unadhani huyu bwana angekuoa, si angeendelea kukaa na huyu mwanamke tasa hapa ambaye anajaza choo tu!”
Maneno hayo yalinifanya nitoke jikoni huku nikiwa nimeshika panga, hasira zilikuwa zimenikaa barabara kichwani. Haraka kama umeme mume wangu alinishika huku akipiga yowe:
“Salome utaua, utaua mke wangu…”


Je, nini kilitokea baada ya hapo? Fuatilia
 
[h=1]Macho ya Bundi- 21-[/h]
"Acha kunifundisha cha kufanya, kosa mimi unadhani huyu bwana angekuoa, si angeendelea kukaa na huyu mwanamke tasa anayejaza choo tu!"
Maneno hayo yalinifanya nitoke jikoni huku nikiwa nimeshika panga, hasira zilikuwa zimenikaa barabara kichwani. Haraka kama umeme mume wangu alinishika huku akipiga yowe:
"Salome utaua, utaua mke wangu…" SONGA NAYO...


Mume wangu alikuwa na nguvu kuliko mimi, alishika panga na kuninyang'anya lakini wakati huo Mei alikuwa ametimka na kuwa nje ya nyumba yetu lakini alikuwa bado anabwabwaja maneno.
"Unataka kunichinja kwa kuona nafaidi siyo, huwezi kuniua mimi wewe kwa sababu ya kupigania haki ya mwanangu. Huniwezi kwa lolote," alisema Mei.
Pili baada ya kuona vurugu hiyo alitoka nje na kumsihi mama yake waondoke kwa ahadi kwamba kesho yake angefika na kuonana na mume wetu.
Binafsi nilimuona Pili ana adabu na anastahili kuwa mke wa pili kwa mume wangu.
Ni kweli kwamba sijazaa na mume wangu licha ya kuishi naye miaka minne sasa na Mei ambaye nilimshirikisha tangu wakati wa uchumba tulipokuwa tunakutana na Chinchi Masasi Hoteli anajua.
Mawazo yalinijia na kujiuliza sababu za Mei kutaka kuvunja ndoa yetu wakati nimekubali mtoto wake Pili aolewe na mume wangu.
***
Ni miezi miwili sasa tangu tuwatimue Pili na mama yake Mei. Nilimshauri mume wangu kwamba ampangishie nyumba badala ya kwenda kwa Mei na akafanya hivyo.
Siku moja nilikuwa na hamu ya kwenda kumuona mtoto na nilinunua nguo kadhaa kama zawadi za kichanga.
Tulikwenda na mume wangu nyumbani kwa Pili na kumkuta akicheza na mwanaye maana tukiwa nje tulisikia akimbembeleza kwa nyimbo za kwao za Kimakua.
"Kinomvelhelha mwana wa numwane (namsindikiza mtoto kwa mama yake), mwanalolha nounlha, mwanalolha noulha mwana noulha, chiichii unanchia (mtoto huyu analia, mtoto huyu analia, chichiii kwanjiwa)".
Ndiyo wimbo aliokuwa akiimba Pili pale sebuleni. Tulikuta kuna viatu nje ya nyumba nikahisi inawezekana mama yake alifika pale.
Tulibisha hodi na kukaribishwa. Tulipoingia tukakuta kumbe aliyekuwa akiimba wimbo ule ni Mei na wala siyo Pili.
"Karibuni, karibuni," alisema Pili.
Tulisalimiana wote na kwa mara ya kwanza Mei alionekana kuchangamka, aliacha kabisa makeke yake ya siku zote.
Nilitoa zawadi zangu kwa mtoto na Pili alizifurahia japokuwa mama yake hakuwa na furaha sana.
Nilizikunjua nguo zote ambazo zilikuwa kwenye kisanduku kidogo na kumpa Pili. Mei hakuchangamka kabisa, hali iliyonishangaza.
Baada ya mazungumzo mafupi tuliaga bila kula chochote kutokana na kumhofia Mei ambaye alijifanya yupo bize jikoni.
Tuliingia kwenye gari na kutoweka nyumbani kwa Pili, ajabu ni kwamba mara tu baada ya kufika nyumbani bundi alipita karibu na uso wangu, akatua katika dirisha la chumba chetu cha kulala macho yake yalikuwa yaking'aa, ghafla nikaanza kutapika.
"Nini tena Salome, una malaria?" aliuliza mume wangu.
Sikumjibu na hali ilizidi kuwa mbaya. Mume wangu akaamua kunikimbizia hospitali baada ya kuniona nanyong'onyea na kuishiwa nguvu kutokana na kutapika sana.

Je, Salome alirogwa na Mei? Fuatilia leo jioni
 
hizi mbili za mwisho nimezisomea ofisini asbh asbh umefanya niwahi. Safi sana Kiongozi
 
Macho ya Bundi- 22-

Tuliingia kwenye gari na kutoweka nyumbani kwa Pili, ajabu ni kwamba mara tu baada ya kufika nyumbani bundi alipita karibu na uso wangu, akatua katika dirisha la chumba chetu cha kulala macho yake yalikuwa yaking'aa, ghafla nikaanza kutapika.

"Nini tena Salome, una malaria?" aliuliza mume wangu.
Sikumjibu na hali ilizidi kuwa mbaya. Mume wangu akaamua kunikimbizia hospitali baada ya kuniona nanyong'onyea na kuishiwa nguvu kutokana na kutapika sana…SONGA NAYO...


Tulipofika hospitali haraka sana niliingizwa kwenye chumba cha daktari akaamua nifanyiwe vipimo.
Nilienda maabara ambapo nilipimwa damu kuchunguza malaria na kuona kama sukari ipo sawasawa mwilini.
Nilichukuliwa damu nyingine kwa ajili ya kupimwa kama nina taifodi.

Baadaye karatasi za vipimo zilipelekwa kwa daktari ambaye aliniita chumbani kwake ili kunisomea majibu, mume wangu Chinchi nilimuacha akiwa amekaa kwenye benchi.

"Mama matokeo ya vipimo yanaonesha huna ugonjwa wowote," alisema daktari huku akigeuzageuza ile karatasi aliyopewa na kuniangalia.
"Sasa kama sina ugonjwa wowote kwa nini natapika sana?"
"Kwani katika mwili wako unajisikia kuumwa chochote licha ya kutapika?"
"Hapana."
"Sasa vipimo vinaonesha huna ugonjwa mama."
"Ushauri wako ni nini sasa kama mtaalamu?"
"Yule aliyekuleta ni nani wako?"
"Ni mume wangu."
"Unaonaje tukimuita ili nikueleze tulichogundua?"
"Umegundua nini wakati umesema sina ugonjwa?"
"Huna ugonjwa lakini una jambo zito?"
"Zito? Nini tena, niambie… mimi si ndiye mgonjwa?"

Moyo wangu ulienda mbio na kujiuliza hawa jamaa wamegundua kuwa nina ngoma? Sasa kama nina ngoma kwa nini wanataka kumuambia mume wangu badala ya kunijulisha mimi kwanza?

Maswali hayo nilijiuliza moyoni huku nikumuangalia daktari aliyekuwa akitabasamu.

"Usitabasamu daktari, niambie kama nimeathirika nijue. Sasa unataka kumuambia mume wangu bila mimi kujua kwanza kwa nini? Huwa mnasema kabla ya mtu kuambiwa kuwa ana ngoma, anapewa ushauri nasaha, sasa mbona hufanyi hivyo?"

"Sikiliza Salome. Nimekuambia huna ugonjwa wowote lakini wewe unakazania kwamba labda una ngoma, sasa kama ungekuwa na tatizo hilo kwa nini nishindwe kukuambia wakati maadili ya kazi yanasema hivyo?"

"Nashangaa, swali hilo jiulize wewe."

Wakati nikitafakari la kufanya daktari huyo alishika kiwiko cha simu yake ya mezani na akampigia nesi.
"Nesi huyo mzee aliyekuja na huyu mama mwambie aingie ndani," sikusikia upande wa pili alijibu nini.
"Ndiyo ni huyo aliyekaa kwenye benchi ana ufunguo wa gari mkononi."
Sekunde chache baadaye mume wangu aliingia katika chumba cha daktari na kunikuta nikiwa natokwa na jasho.
"Amezidiwa, niambie daktari amezidiwa?" alisema mume wangu huku akionesha wasiwasi mkubwa.
"Hapana, nimekuita kuna jambo tumegundua."
"Jambo gani tena daktari!"
"Huyu ni mkeo?"
"Ndiyo."
"Napenda kukuarifu kwamba, hana ugonjwa wowote unaomsumbua isipokuwa…"
"Isipokuwa nini,kwa nini anatapika mfululizo?"
"Mzee wangu ungesubiri basi nimalize kutoa maelezo."
"Sawa. Nakusikiliza."

Je, Salome amegundulika na tatizo gani? Pata jibu
 
Macho ya Bundi- 23-


ILIPOISHIA
Sekunde chache baadaye mume wangu aliingia katika chumba cha daktari na kunikuta nikiwa natokwa na jasho….
"Napenda kukuarifu kwamba, hana ugonjwa wowote unaomsumbua isipokuwa…"
"Isipokuwa nini,kwa nini anatapika mfululizo?"
"Mzee wangu ungesubiri basi nimalize kutoa maelezo."
"Sawa. Nakusikiliza."
SASA PATA MAMBO...


"Mzee tulia nikupe habari."
"Haya sema sasa."
"Mzee kwani mlikuwa na mpango wa kupata mtoto hivi karibuni?"
"Unasemaje?"
"Hukusikia?"
"Rudia!"
"Nimekuuliza mlikuwa na mpango wa kupata mtoto hivi karibuni?"
"Kwa nini unaniuliza hilo swali?"
"Jibu kwanza swali huwezi kupandanisha maswali."
"Nijibu kwa nini unaniuliza hivyo?"
"Mkeo ni mjamzito!"
"Siamini!!"
"Mkeo ni mjamzito ndiyo maana anatapika. Haumwi chochote."
"Salome, Salome, nakupenda sana."
Alinikumbatia tukiwa tumesimama wima. Nilishindwa kuvumilia, nilitokwa na machozi na kuanza kulia kwa kwikwi. Mume wangu naye alibubujikwa machozi hali iliyomfanya daktari kushangaa.
"Jamani, kwa nini mnalia?"
"Ni hadithi ndefu sana, hatuamini hiki unachotuambia," alisema mume wangu na kuanza kumsimulia mkasa wote uliotaka kusambaratisha ndoa yetu.
"Basi Mungu alisikia kilio chenu, mama una ujauzito na kwa kuwa una miaka thelathini na tatu itakubidi uwe karibu sana na hospitali ili upate uangalizi wa karibu wa madaktari. Unajua ukipata ujauzito ukiwa na umri kama wako kunahitajika uangalizi wa karibu."
"Daktari wangu atakuwa wewe," nilisema huku machozi yakiendelea kulowanisha mashavu yangu.
Tulitoka ndani ya hospitali hiyo tukiwa na furaha kubwa sana. Hakika tulijiona kama vile tumefunga ndoa leo.
Tulipofika nyumbani kijana wetu wa kazi alitushangaa kwani mara tu baada ya kushuka kwenye gari tulikumbatiana na kuingia ndani.
Nilipoingia, nilikwenda moja kwa moja kuchukua shampeni isiyo na kilevi na kuifungua. Nilimmwagia yote mume wangu, naye akaenda kuchukua yake akafanya kama nilivyofanya mimi.
Nilifungulia muziki sauti ya juu tukawa tunacheza na mume wangu. Tulikatizwa na Mei aliyefika ghafla na kugonga mlango.
"Nini tena? Mei nilikuambia usije tena hapa?" alifoka mume wangu.
"Nimekuja kukuarifu kuwa mwanao mgonjwa."
"Kwa nini Pili asinipigie simu na ukaamua kuja wewe?"
"Hakupiga kwa sababu naye analia baada ya kuona mtoto kazidiwa."
Mume wangu aliingiza mkono mfukoni na kumpa shilingi elfu arobaini.
"Nenda mpelekeni hospitali na kama atakuwa na tatizo lingine, Pili anipigie simu, tafadhali sana sitaki uje hapa nyumbani. Nasema sitaki."
Mei hakujibu chochote, alinyakua zile fedha, akatoka nje na kuingia kwenye gari lililomleta, akatoweka.
Mei baada ya kupewa fedha alikwenda moja kwa moja kunywa bia jirani na nyumba waliyopangishiwa na mume wangu.
Tulijua hayo baada ya kumshauri mume wangu apige simu kwa Pili kujua hali ya mtoto.
"Mama alikuja huko? Mbona amerudi sasa hivi na amesema anakwenda kutuliza mawazo kwa kupata bia mbili tatu, alikuja kufanya nini?"
"Kwani mwanao haumwi?"
"Haumwi. Mzima nacheza naye hapa."
"Mjinga sana mama yako."


Mei kasingizia mtoto kuumwa? Je, nini kitatokea? Fuatilia
 
Aiseee hadithi hii sijui kwa nini asiisimulie mpaka mwisho..! Inanoga balaaa..!
 
Macho ya Bundi- 24-

ILIPOISHIA
Mei baada ya kupewa fedha alikwenda moja kwa moja kunywa bia jirani na nyumba waliyopangishiwa na mume wangu.
Tulijua hayo baada ya kumshauri mume wangu apige simu kwa Pili kujua hali ya mtoto wao.
"Mama alikuja huko? Mbona amerudi sasa hivi na amesema anakwenda kutuliza mawazo kwa kupata bia mbili tatu, alikuja kufanya nini?"
"Kwani mwanao haumwi?"
IPATEPATE ZAIDI...


"HAUMWI. Mzima nacheza naye hapa."
"Mjinga sana mama yako."
"Vipi ujinga wake ni upi?"
"Kaja hapa akasema eti mtoto mgonjwa na ana hali mbaya."
"Mama kasema hayo?"
"Ndivyo alivyoniambia na nimempa shilingi elfu arobaini baada ya Salome kunishauri."
"Jamani mama ananishangaza sana, alikuwa na shida ya fedha za kunywea akaona aje kukudanganya."
Mume wangu alikata simu.
Tuliamua siku hiyo kwenda kula chakula cha jioni katika hoteli moja inayoitwa Kem, ni hoteli ya kisasa ambayo hata mwanamuziki Diamond aliwahi kuja kufanya vitu vyake.
***
Miezi ya kujifungua ilifika na siku hiyo nakumbuka ilikuwa saa tisa usiku niliposikia maumivu makali sana ya tumbo.
Nilimwamsha mume wangu na kumpa taarifa ya kuugua kwangu.
"Kama ni hivyo ni vyema tuwahi hospitali."
"Sawa."
Nakumbuka wakati tunahudhuria kliniki tuliambiwa tuandae pamba, glovu, wembe, kanga na zagazaga nyingine ambazo manesi walisema zitatusaidia siku ya kujifungua.
Nilimuambia mume wangu Chinchi achukue begi langu ambalo lilikuwa na vifaa hivyo na haraka sana akavikimbiza na kuviweka kwenye gari.
Nilijikokota kutoka nje ya nyumba yetu kwenda pale lilipokuwa gari, niliona kama vile lipo maili mbili kwa jinsi nilivyokuwa nasikia maumivu.
"Ngoja nikusaidie," alisema mume wangu huku akinishika mkono.
Ghafla tukiwa tunatoka nje ya nyumba, yule bundi ambaye huwa tunamuona mara kwa mara aliruka na kusimama kwenye dirisha letu.
"Mume wangu unamuona yule bundi anatuangalia?"
"Achananaye huyo na wala usimfikirie!"
"Nisimfikirie kwa nini wakati huwa anatoka na kusimama katika dirisha letu?"
"Nimekuambia achananaye, mara ngapi tunamuona na hakuna chochote kinachotupata? Mungu mkubwa."
"Sawa lakini ni lazima tupitie kwa Padri Kalo akatuombee."
Alinikokota hadi kwenye gari na yeye kuliwasha. Tulikwenda moja kwa moja hadi kwa Padri Kalo ambaye alishangazwa sana kusikia tunamgongea usiku ule.
"Mzee Chinchi kwani kuna nini usiku wote huu?" alihoji Padri Kalo.
"Tafadhali sana toka nje, tuna dharura."
Padri Kalo alitoka huku akiwa kavaa kanzu akaambiwa na mume wangu kuwa tumepitia tu kwake tunahitaji maombi.
"Mke wangu hajisikii vizuri, naomba umfanyie maombi kabla ya kwenda hospitali."
Alianza maombi yake: "Mungu tunakuomba malaika wako wamlinde mama huyu na wabaya wote waliomzunguka. Nakuomba uwe karibu naye wakati wote akiwa hospitali ambako anakwenda kujifungua ili ajifungue salama na aijaze dunia kama wewe mwenyewe ulivyoamuru enzi ya babu yetu Adamu na bibi Hawa. Tunaomba haya tukikutanguliza wewe Mungu. Amin."
Tuliondoka kwa padri kwa mwendo wa kasi huku tumbo likiniuma sana.



Je, Salome Katonaga atajifungua salama au bundi atafanya nini? Fuatilia baadae
 
[h=1]Macho ya Bundi- 25-[/h]
Alianza maombi yake: "…Nakuomba uwe karibu naye wakati wote akiwa hospitali ambako anakwenda kusubiri kujifungua ili ajifungue salama na aijaze dunia kama wewe mwenyewe ulivyoamuru enzi ya babu yetu Adamu na bibi Hawa. Tunaomba haya kwa jina lako. Amina.

Tuliondoka kwa padri kwa mwendo wa kasi huku tumbo likiniuma sana.
SONGA MBELE...

Nakumbuka kabla ya kuondoka Padri Kalo alichungulia ndani ya gari na kuniona nikiwa najinyonganyonga kwa maumivu.
"Mama nendeni kwa amani, Mungu atawatangulia na malaika wake wako pamoja na wewe, usiwe na wasiwasi."
Mume wangu alizidisha kasi ya gari nikamuambia apunguze mwendo, tulifika katika Hospitali ya Mkomaindo salama, nikapokelewa.
Kilichonishangaza ni kumuona bundi mwingine akiwa juu kabisa ya paa la hospitali hiyo. Macho yake yalikuwa yanang'aa. Niliingizwa hospitalini huku moyo ukienda mbio.
Haikuchukua muda nilijifungua mtoto wa kiume. Alikuwa na afya njema na baada ya dakika chache mume wangu aliitwa akamuona mwanaye.
Tulifurahi sana.
Tulirudi nyumbani tukiwa na furaha isiyo kifani.
Nilikaa na mwanangu nyumbani, siku ya kliniki ilipofika nikampeleka.
Wakati naingia hospitali moyo ulidunda paa kwani nilimuona bundi akiwa amesimama kwenye dirisha la mlango ambao nilitakiwa kupita ili niingie hospitali.
Moyo wangu ulidunda sana kwani bundi huyo hakuwa na uoga na sisi kwani mume wangu alijaribu kumfukuza lakini hakuondoka.
Sikuvumilia ilibidi nimuite nesi ambaye nilikuwa nimemzoea na nikaamua kumuuliza kwamba kwa nini kila nikienda pale, nilimuona ndege huyo akiwa amesimama dirishani au juu ya paa?
"Usiwe na wasiwasi hawa bundi hapa ni makazi yao. Wapo hapa baada ya kuhama kutoka Mlimani Mkomaindo ule palee. Wanafuata vyakula," alisema nesi na kuniondoa wasiwasi.
Niliporudi nyumbani nilitafakari jibu la nesi hivyo nilimuambia kijana wangu wa kazi atafute kwenye miti iliyozunguka nyumba yetu kama kuna kiota chochote cha bundi baada ya muda alikuja na jibu.
"Mama ule mti mkubwa pale kuna viota vingi sana vya bundi ndiyo maana usiku huwa wengi karibu na nyumba yetu."
Hapo niliondoa shaka kwamba bundi wote ninaowaona karibu na nyumba yetu kuwa ni wa kishirikina. Nilijua ni wa kawaida tu.
***
Mtoto wa Pili alikuwa ameshakuwa mkubwa na mume wangu akaniambia kuwa atakwenda kijijini kwa Pili akafanye uamuzi mzito.
"Uamuzi gani tena mume wangu?"
"Nataka kwenda kwa Mei kumtangazia kuwa namuacha mtoto wake Pili."
"Hapana usifanye hivyo, Pili siyo mbaya, ubaya anao mama yake ambaye mimi ni rafiki yangu."
"No. Nitamuacha kwa ahadi kwamba atarudi darasani na mtoto wake tutamlea sisi. Pili nitamhudumia kila kitu mpaka amalize masomo yake, kisha achukue hamsini zake."
Nilifikiri na kumshauri kwamba kabla ya kufanya uamuzi huo, ajadiliane kwanza na yeye Pili kujua kama atapenda kurudi shuleni au la.
Mume wangu aliamua kumuita Pili pale nyumbani kwetu. Wakawa wanazungumza:
"Pili nimekuita kwa jambo moja. Nilitaka urudi darasani na mtoto utuachie tumleee sisi, unasemaje kuhusu hilo?"
"Ni ghafla sana natakiwa kutafakari."
"Utafakari nini? Nenda shule mama." Niliingilia.



Pili atakubali kwenda shule? Mama yake Mei atapokeaje ushauri huo? Fuatilia sakata hili leo jioni.........
 
Back
Top Bottom