Gogle
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 1,495
- 871
ILIPOISHIA Salome alishangaa, Au jana aligundua nimeona kitu kinachopumua sandukuni mwake? alimuuliza mwenzake. SASA ENDELEA... Mei hakunijibu haraka swali hilo. Alinitazama kwa sekunde chache, tukaendelea kupata kifungua kinywa. Baada ya kumeza funda moja la chai alinijibu: Siyo kwamba aligundua jambo, anasema ulimuudhi, inawezekana kuna kitu alikuambia nawe ukakataa. Kama ulikuwepo. Aliniambia ana jambo anataka kuniambia akataka turudi chumbani mimi nilimkatalia. Basi kama ni hivyo ni bora tungoje nini atashuka nacho kutoka huko ghorofani. Hakuchukua muda mrefu Chinchi alishuka akiwa na kifurushi mkononi. Nilihisi kile kifurushi kile ndicho kilichokuwa kwenye sanduku kikipumua. Chinchi baada ya kufika kwenye meza yetu alikiweka juu kikawa kinaendelea kuonekana kana kwamba ndani kuna kitu kinapumua. Salome hii ni zawadi yako, alisema Chinchi. Sikutabasamu wala kuifurahia zawadi hiyo kwa kuwa sikuwa najua nini kilichowekwa, tena basi kinachopumua. Niliogopa hata kukishika kifurushi hicho. Mbona unaonekana kutofurahia hii zawadi. Sijui ni zawadi gani, naiogopa, mbona kuna kitu kama vile kinapumua humu ndani na kwa nini unizawadie. Sikiliza Salome. Usiwe na wasiwasi, kwani kitu kibaya naweza kukupa tena mbele ya watu namna hii? Alichukua kile kifurushi na kukifungua. Mimi na rafiki yangu Mei tukiwa tunatumbua macho kukiangalia. Mimi na rafiki yangu tuliangua kicheko baada ya kukiona kilichokuwemo ndani ya kifurushi. Mbona mmecheka sana, au zawadi hii ziyo nzuri? Niliishuhudia saa nzuri sana ambayo ilikuwa ina umaridadi wa hali ya juu. Ilikuwa imetengenezwa mfano wa tumbo na kila dakika zinapogonga, tumbo lilikuwa likifutuka kana kwamba inapumua. Baada ya kumshukuru aliniambia ameniita kwa nia moja tu, kwamba anataka kunioa. Hujawahi kuwa na mke katika maisha yako? Sijawahi. * * * Tulioana na Chinchi. Ndoa ilikuwa ya kifahari kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha aliokuwa nao. Baada ya ndoa nilimshauri mume wangu twende tukamtembelee Mei nyumbani kwake, akakubaliana nami. Alinisindikiza hadi nyumbani kwa rafiki yangu huyo. Kiumri Mei alikuwa mkubwa kuliko mimi japokuwa tulikuwa marafiki sana. Mwenzangu tayari alikuwa na binti wa kike aliyekuwa anasoma kidato cha pili anayeitwa Pili, mimi nilikuwa bado sijazaa. Karibu na nyumbani kwangu kulikuwa na jirani yetu ambaye alikuwa anaitwa mama Koki, siku moja alipofika kwangu nikasikia mtu anagonga mlango kwa nguvu. Karibu, mama Koki. Sijui utanielewaje, nimeona nikuambie ujue la kufanya.Una kifua shoga? Niambie tu mama Koki. Mama Koki alinyamaza kwa muda akaniambia kuwa jambo analotaka kuniambia ni zito. Sikiliza Salome. Kuna msichana ulinifahamisha siku moja kuwa anaitwa Pili na ni mtoto wa rafiki yako Mei. Huwa anakuja hapa kwako mara kwa mara kila unapokuwa umeenda kazini. Anamkuta mumeo tu, mama Koki alinyamaza akaniangalia. Huyu binti nina wasiwasi naye, atakuvunjia ndoa yako. Fanya uchunguzi. Machozi yalinitoka na kujiuliza kweli mtoto wa Mei anaweza kuniingilia katika ndoa yangu? Nilichanganyikiwa.
Itaendelea
Itaendelea