Machimbo ya dhahabu bado nayadai

Next time ukiona sehem Kuna fursa usiwe na haraka ya kujikita kwenye eneo la tukio.. jitahidi kusoma mchezo unavoenda, fanya research ndogo ndogo kuhusu shughuli husika. Angalia changamoto zake na kama una uwezo wa kukabiliana nazo. Hio 28m uliyopoteza kama ungetuliza akili basi ungekuwa mbali sana bila hata kuumiza kichwa na kushika suluhu kuchimba miduara. Kwenye machimbo ya dhahabu Kuna mahitaji mengi ya kibinadam ambayo ungejikita nayo kwanza, unachukua mali town unapeleka chaka kiboss boss huna strees.. huku unatoa service, huku unapata somo on the field.. Kuna machimbo mengine kama pale tabora ndani ndani nimepasau jina.. kule mjomba mpaka hizi chupa za maji zilizotumika ni hela kama una usafir wa uhakika unabeba unapeleka kwenye viwanda wanafanya recycling..
Maji ya shida kule, kulala kwa shida kule.. hizo zote fursa mzee Yuda Legacy
 
Mkuu hiyo detector ulichukua kiasi gani?
 
Nimekupata mkuu [emoji120][emoji120]
 
Kama una uzoefu naomba unijibu. Kwa makadirio, kila watu 100 wanaokwenda kubahatisha kupata utajiri wa dhahabu, ni wangapi wanapata na ni wangapi wanafeli? Kujua mahesabu kama haya ni vizuri sana kabla hujaamua kuingia huko.
 
Ujue kabla hujafanya kitu chochote ni vzr ukafanya utafiti wa kutosha nini matokeo yake hiyo M50 akiamua kuwa mnunuzi wa dhahabu maarufu kama kota ni nyingi sana wewe unakua unanunua kitu kilichokamili, ila yakupasa kuwa na elimu pia na hiyo biashara sababu ukizubaa unauziwa feki au pungufu so inabidi uwe na lesini mzani pamoja na ofisini then usiwe na tamaa nina mengi ya kuandika ila mimi mvivu wengine wataongeza
 
Kama una uzoefu naomba unijibu. Kwa makadirio, kila watu 100 wanaokwenda kubahatisha kupata utajiri wa dhahabu, ni wangapi wanapata na ni wangapi wanafeli? Kujua mahesabu kama haya ni vizuri sana kabla hujaamua kuingia huko.
Kwenye 100 mnaweza msitoboe wote bro wakitoboa wengi ni 5-8 wakifika 15 machimbo hayo yatakua maarufu sana na watu hawataondoka kirahisi hapo

Ila wapo wanaotoboa katika machimbo kwa kufanya shughuli zingine zisizo za kichimbaji kama vile wauza vyakula, maji vinywaji vinatoka sana hasa machimbo yenye population kubwa.
Wapo wanaoenda kwa kuanzisha biashara ndogo na baadae wanafungua maduka makubwa ya jumla
 
Kale kashimo ninako kaona ndio unaenda kuzama pale?
 
Hayo ndio ya kuzingatia sana,
Siwezi kukurupuka kwani nimefanya baishara nyingi tu huwa nina machale sana yaani huwa naona tapeli kabla hajaniibia
Nafuatilia sana na kufanya utafiti hata kutafuta references za huyo mtu kama anajulikana au la
Hii baishara ni ngumu ninavyoisikia na ina matukio mengi sana hata mauwaji kushinda biashara zingine
Nitajitahidi kuyasoma mengi zaidi Asante sana
 
Nawezaj Naweza pata hyo miwani?
 
Ujambazi haupo tena hata kuubiwa kumepungua sana sababu kuna vifaa vingi sana vya kutambua vip feki na kipi ni sahihi nimekua kwenye hiyo secta na nilianza na laki tano tuu nilishikwa mkono na mtu ambae tulijuana huko huko poloni na nilikua vzr sana bahati mbaya sana jamaa alikuja kupata ajali na mbaya zaidi siku hiyo ndo nilikua nimetoka poli dhababu yote ilikua kwake ndo ukawa mwisho wangu kwa hasira sikutaka tena nikaondoka sa hv nipo dsm but dhahabu ukiiheshimu itakuheshimisha pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…