~ * ~ Mabusu Yangu Dazeni ~* ~ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~ * ~ Mabusu Yangu Dazeni ~* ~

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 7, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  HAYA NI MABUSU YANGU DAZENI


  Mabusu yangu dazeni, nayatuma kwako moyo!
  Ulipo hapo mjini, natuma bila uchoyo,
  Pokea wangu wa ndani, ni dazeni nikupayo,
  Kwa hili Busu la kwanza, beti nazifungulia!
  Mwah!!
  Hilo la kwanza kwenye paji!

  Mabusu yangu dazeni, moja moja narushia,
  Nimeketi barazani, ujumbe nakutumia,
  Wenye wivu jinyongeni, wa kwangu namwagia,
  Kwa hili busu la pili, asante kwa yote pia!
  Mwah!!
  Hilo la pili, shavu la kushoto!

  Mabusu yangu dazeni, tumetoka sisi mbali,
  Nakumbuka vya zamani, tulipoanza wawili,
  Mioyo ikashikani, mahaba yakashamili,
  Kwa hili busu la tatu, mbali nakukumbushia!
  Mwah!
  Hilo la tatu, shavu la kulia!

  Mabusu yangu dazeni, ninamshukuru Mola,
  Mtukufu wa Mbinguni, mwenye kuzipinga hila,
  Kakuleta ubavuni, ni bure siyo kwa hela,
  Kwa hili busu la nne, ujue nakuhitaji!
  Mwah!
  Hilo la nne, shingoni kushoto!

  Mabusu yangu dazeni, nisamehe nipokosa,
  Yamenijaa pomoni, hata uliponiasa,
  Kurudia sitamani, kufanya hivyo ni kosa,
  Kwa hili busu la tano, nakuomba samahani
  Mwah!
  Hilo la tano, shingoni kulia!

  Mabusu yangu dazeni, Mungu amekujalia,
  Uzuri wako wa shani, binti wa Kitanzania,
  Wengineo siwaoni, wewe najichagulia,
  Kwa hili busu la sita, nashukuru wewe wangu!
  Mwah!
  Hilo la sita, mgongoni!!

  Mabusu yangu dazeni, penzi lako limefana,
  Twapendana kama nini, mitimani twashibana,
  Kama tuliopeponi, mahaba yametunona,
  Kwa hili Busu la saba, mpenzi nakutamani!
  Mwah!
  Hilo la saba, kwenye titi la kushoto!

  Mabusu yangu dazeni, wanipa penzi si haba,
  Wanipa kiulaini, tena siyo kwa kibaba,
  Ya wengine siyaoni, la kwako limeniziba!
  Kwa hili busu la nane, naapa mimi ni wako!
  Mwah!
  Hilo la nane, kwenye titi la kulia!

  Mabusu yangu dazeni, wewe nakuaminia,
  Mashaka kwako sioni, penzilo limetulia,
  Habiba waniamini, moyo umenishikia,
  Kwa hili busu la tisa, asante kuniamini!
  Mwah!
  Hilo la tisa, kitovuni!

  Mabusu yangu dazeni, tusiwajali wakora,
  Kulivunja watamani, penzi letu lawakera,
  Visa wanavyovibuni, tuachane kwa papara,
  Kwa hili busu la kumi, tugange mbele kwa mbele!
  Mwah!
  Hilo la kumi, nyongani kushoto!

  Mabusu yangu dazeni, naapa mimi ni wako,
  Moyo wangu mkononi, ushike unipe wako,
  Kama kufuri langoni, funguo iwe ni yako,
  Kwa hili kumi na moja, milele tutapendana!
  Mwah
  Kumi na moja, nyongani kulia!

  Mabusu yangu dazeni, la mwisho nimefikia,
  Wabarakatau Ma'nani, kwake nimejiachia,
  Akupe afya mwilini, baraka kukumwagia,
  Kwa hili busu dazeni, UJUE NINAKUPENDA
  Mwah!
  Busu hili la dazeni!!......

  Haya basi mabusu yote,
  Mwah! kwenye paji
  Mwah! shavu la kushoto
  Mwah! shavu la kulia
  Mwah! shingoni kushoto
  Mwah! shingoni kulia
  Mwah! mgongoni
  Mwah! Titi la kushoto
  Mwah! Titi la kulia
  Mwah! Kitovuni
  Mwah! Nyongani kushoto
  Mwah! Nyongani kulia
  Mwah! ........


  na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
  mwanakijijiatjamiiforums.com
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  MKuu kumbe huvumi lakini umo ehhhhhhhh!Nilijua wewe ni wa siasa tuuu!
  Congrats kwa hizo cheche nimeanza craming nikamwimbie sabuni yangu ya roho!
  Umezipangilia kwelikweli!
   
 3. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha kofia nakuvulia mzee...
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,106
  Trophy Points: 280
  umh Mzee wewe kiboko, HEKO kwa kazi njema.
   
 5. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kweli nimeikosa hii burudani muda mrefu,wewe kweli Gwiji.sijui kwanii walitoa ile column ya lugha sikujua mambo kama yanaendelea humu kwa wapenzi.
  Hongera.
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tena kuhusu hiyo column ya Lugha mtaniwia radhi kwenda out of topic!Kuna mtu anaweza kunipa hili neno kwa Kiswahili?
  Global Positioning System ( GPS )?
   
 7. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0


  pardon me for asking but who you gonna tell abt GPS in kiswahili wakati hajui ni nini hiyo?
  au just for the seek ya kujua...?
  Ninashangaa bado.

  just google KAMASI SANIFU on line alafu utaona
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sanda... umenichekesha..

  Nadhani Global Positioning System naweza kuiita kuwa ni Chombo/Mfumo wa/cha Kuonesha Mahali
   
 9. S

  Sunshine OLD Member

  #9
  Aug 8, 2008
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Beautiful!!!!!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Asante sana sunshine!
   
 11. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mzee wa shamba kofia nimekuvulia!!
   
 12. Mzozo wa Mizozo

  Mzozo wa Mizozo JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2008
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 427
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du! Hii sasa ni kali haswa.. Mzee MNKJJ sikujua kama unagonga pande zote kwa level hizi...

  Burudani tosha asubuhi yangu ya leo...
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Aug 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nashukuru natumaini nimewapa watu burudani tosha na kwa sekunde chache kuyatoa mawazo yenu kwenye mambo ya kuumiza vichwa..
   
 14. S

  Sunshine OLD Member

  #14
  Aug 12, 2008
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Burdani kubwa sana hii!
  Whenever I visit this site, I must read the poem!
  I love it!
   
 15. Mr Q

  Mr Q JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2016
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,056
  Likes Received: 7,086
  Trophy Points: 280
  mzee siku moja moja uwe unatembelea huku siasa wakati mwingine zinatia uchizi
   
 16. Rwekaza Autonomy

  Rwekaza Autonomy JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2016
  Joined: May 4, 2013
  Messages: 317
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Hadith yko inatufndsha nn mkuu
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  May 15, 2016
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  duh.. watu mnajua kufukua; msiendelee kufukuta msije kukutana na lile la "kisu changu ni kikali"... duh!!
   
Loading...