Mabondia wetu njaa au utapia mlo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabondia wetu njaa au utapia mlo?

Discussion in 'Sports' started by Fidel80, Dec 18, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nimesikitika sana mabondia wetu wanashindwa hata kupata milo ya maana kujenga miili yao.
  [​IMG]
  Kulia ni bondia Festus Omondi kutoka nchini Uganda atakaye pambana na hasimu wake Mbwana Matumla (kulia) katika raudi 12,uzito wa Bantam Weight.Mbwana Matumla ana uzito wa Kg 53 na Festus Omondi ana Kg 51
  [​IMG]
  Bondia Festu Omondi kutoka Uganda akipima uzito leo mchana ndani ya ukumbi wa Idara ya habari Maelezo  [​IMG]
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Yaani.njaa tupu.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wanatia huruma, na wamepauka mbaya kabisa...huh!
   
 4. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa sijawaelewa mnatakeje. Huo uzito wanaopigania si ndio miili yao? Au mnataka wawe na miili ya kilo 90? Shaurini vyama vya ndondi viondoe uzito mwingine wabakishe uzito wa juu pekee hapo ndio mtapata wenye miili mikubwa.
   
 5. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 424
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Umenena vyema mkuu ! Ndo mana kuna uzito tofauti tofauti katika ndondi, kuna uzito wa unyoya (feather weight), uzito mwepesi (light weight), bantam weight, mpaka heavy weight...sasa mtu wa uzito wa unyoya hawezi akawa na mwili kama Kaseba..it's not rocket science
   
 6. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  zisi iz siriazi
   
 7. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sio njaa wala utapiamlo, ni ukapa!
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sio njaa wala utapiamlo, ni ukapa!
  Anyway, lakina wanakaribia kufanana na Avator yako
   
 9. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2009
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kha aisee yani wewe utakua mtu wa ajabu sana kama hulioni tatizo hapo....hebu jaribu kuangalia tena hizo pics....hatuzungumzii ukubwa wa miili tunazungumzia ''''AFYA BORA''''....we wazani kunenepesha matumbo kwa wabongo ndo sign ya afya bora kama wanavyojidanganya waliowengi... it means huoni kabisa hizo physical appearance zinakushow sign gani wewe kama Great thinker??????
  .....so unataka nambia wakilinganishwa na mabondia wengine wa uzito sawa toka sehemu zenye akili duniani ..... watafanana appearance yao??????
  ......u must be jokin' hommie....
   
 10. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  BABA,
  Huyo mwingine si ni bondia kutoka Uganda si nasikia kule wanakula Matoke kwa Sangara na Sato!
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahahaha!hii no njaa
   
 12. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2009
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jamani huyo akipigwa ngumi iliyoshiba si anakufa kama sio kuzimia wiki nzima!! wangeweka sheria zinazolenga pia body structure na weight ya mchezaji...yani sisi kwetu njaa tu, mpaka mashindano ya mbuzi, utakuta mbuzi nao utapiamlo mtupu,
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hivi matokeo yako vipi??????
  cheka kadundwa????????
   
 14. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Cheka au Mbwana Matumla? Ninadhani huyu jamaa hakuwa miaka 2/3 iliyopita. Kutakuwa na tatizo.
   
 15. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Cheka, Matumla wangÂ’ara Dar

  MABONDIA wa Tanzania Francis Cheka na Mbwana Matumla, juzi usiku walingÂ’ara kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa ya kimataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa PTA Sabasaba.

  Cheka bondia anayezidi kujizolea umaarufu alitetea taji la UBO na kutwaa taji la WBC uzito wa kati.

  Kwa upande wa Matumla alitetea taji la ICB na kutwaa la UBO uzito wa Bantam. Hata hivyo, Cheka hakupigana na Muargentina Enrico Areco kama ilivyokuwa ikitangazwa na waandaaji wa mapambano hayo Prime Time Promotions na badala yake alipigana na Isak Tavares wa Brazil.

  Kwa mujibu wa waandaaji, bondia Areco alishindwa kufika nchini baada ya kutokea matatizo katika hati yake na kusafiria na ndipo ilipoamuliwa aje Tavares ambaye alifika Jumamosi mchana.

  Mabondia wote walishinda kwa KO katika raundi ya pili na ya tano ya mapambano yao.

  Tangu kuanza kwa pambano lake, Cheka alionekana dhahiri kumtwanga mpinzani wake kwani alimuangushia makonde ya nguvu na kumuangusha mara mbili katika raundi ya kwanza.

  Alifanya vivyohivyo katika raundi ya pili ambapo alimuangusha mara mbili tena kabla ya mwamuzi kumaliza pambano ili kumuokoa Mbrazil huyo.

  Kwa upande wa Matumla aliyepigana na Francis Omondi wa Uganda alimchapa kwa KO katika dakika ya kwanza ya raundi ya tano.

  Kabla ya kumshushia kipondo hicho alimuangusha mpinzani wake mara tatu mfululizo katika raundi hiyo


  Source: habarileo

  Hapa nomba mwenye kujua hii mikanda iliyotajwa inatambulika??

  UBO......
  ICB......
  labda WBC lakini kwenye web yao hakuna hawa watu maajabu
   
Loading...