Mabomu msafara wa Lowassa, hii inaashiria nini?

Mabomu msafara wa Lowassa, hii inaashiria nini?

Alienda kagera kama nani? Waziri mkuu mstaafu , kiongozi wa upinzani, raia wa kawaida au kama kada maarufu wa chadema?

Sheria ya nchi iko wazi mikusanyiko ya aina yoyote ni lazima yaombewe kibali ikiwa ni hata kama mapokezi ili serikali itoe ulinzi kwa hao wapokeaji na wasio wapokeaji ambao wanaweza kukwazika na huo mkusanyiko.

Je aliomba kibali? Huu ni utawala washeria mambo ya kienyeji enyeji yaliyashakwisha tangu enzi za mkwere. Na bahati yake wangemvunja kiuno ili next time ajifunze kuwa akitaka kuingia kwa mtu yoyote lazima apige hodi
Mbona mwenyekiti .wa jumia ya wazazi wa ccm alikuwa na mikusanyiko ?? mbona mabomu hayakupgwa??jaribu katumia akili kdogo
 
Ni dhahiri kuwa serikali imeshindwa kuwa na amani na Lowassa kwa sababu wanazozijua wao vizuri sana tena tangu akiwa ndani ya CCM. Jinsi walivyohitimisha suala la Richmond wengine tulibakia na maswali mengi tu.

Baada ya hapo wamemuendeshea kampeni ya kufa mtu kumnasibisha na ufisadi papa - kuwa ndiye kinara wa ufisadi nchini! Haya, wakaenda mbali zaidi kumthibitisha ugonjwa. Push-ups zikapigwa majukwaani kuonyesha tofauti. Kampeni ikazidi kutumbukia kwenye majitaka kumdhalilisha kabisa utu wake.

Pamoja na yote akapata uungwaji mzito katika kampeni na uchaguzi mkuu wenyewe. Sasa ni mwendo wa makatazo, vitisho, mabomu ya machozi, hoja za kipuuzi za polisi, n.k. Manake hamna namna nyingine tena. Wamejitahidi kuwaambia wananchi kuwa Lowassa ndiye kubwa la mafisadi lakini wapi! Umati unaendelea kumfuata tu. Quite frustrating.

Pamoja na mkao wake wa kistaarabu, kwangu mimi bado sijamuona Lowassa kuwa mtu wa maana sana kimaadili. Hadi sasa namhesabu kama mmoja wa mtandao wa uongozi wa CCM uliojenga na kuuimarisha mfumo wa ufisadi unaoliangamiza taifa hadi Leo hii. Labda kuna siku atatoa msimamo wake rasmi dhidi ya mtandao huo.

LAKINI sikubaliani kabisa na juhudi za serikali na CCM kumgeuza Lowassa kuwa ndiye shetani wetu mkuu halafu wao eti ndio mnabii na mitume wetu waliodondoka toka mbinguni majuzi! TENA nina mashaka kuwa wanaogopa kuwa huenda jamaa ndio anajitoa kwenye mtandao ilhali ana siri zao nyingi. Hawana imani wala amani. Ni kuota majinamizi kwa kwenda mbele. Dawa pekee waliyobakia nayo nionavyo, ni kumfikisha Lowassa kwenye mahakama ya mafisadi kama kweli wana jeuri hiyo. Manake hapo ni lazima waweke "suicide pact".
 
Mbona mwenyekiti .wa jumia ya wazazi wa ccm alikuwa na mikusanyiko ?? mbona mabomu hayakupgwa??jaribu katumia akili kdogo
Alienda kama mwenyekiti na taarifa alitoa kwa mamlaka husika na escort akapewa. Mwenyekiti alijielewa na akawaelewesha wenye mamlaka na wakamwelewa. Huyo wa kwenu alifikiri Kagera ni kwenye mazizi ya ng'ombe wake. Na mmwambie hata chooni watu huwa wanapiga hodi.

Akirudia tena tutadili nae na atafanya kioja kama kile alichofanya Nzega Stand.
 
Aache kutafuta kick kwa kutumia majanga! Kama ana Pesa akachangie madawati na huduma zingine!
KunA watu sio wazima humu me nikajua ni kule wanapaita IG kumbe hata huku..daaah Tanzania yangu
[HASHTAG]#MunguTuacheTufe[/HASHTAG]
 
mliolisaidia hili jamaa kuiba sauti na maamuzi ya wananchi hadi likaingia pale magogoni mungu anawaona.. linaboa hili lishamba!!!
 
Mbona mwenyekiti .wa jumia ya wazazi wa ccm alikuwa na mikusanyiko ?? mbona mabomu hayakupgwa??jaribu katumia akili kdogo
Me nahic hawa vijana wa Uhuru kunA kitu huwa wanalishwa sio bure
 
Me nahic hawa vijana wa Uhuru kunA kitu huwa wanalishwa sio bure
Hicho kitu tumelishwa sisi au nyie ambao mnaweza kuaminishwa kuwa kinyesi ni keki na mkala. Mnapiga kelele Rais hafati sheria huku nyinyi hizo sheria mnazisigina na mnataka muonekane mko sawa. Hata wapiga vigodoro usiku huwa wanaomba vibali iweje isiwe nyinyi au mnajifanya watoto wa mfalme?

Sheria iko wazi mkusanyiko wowote ule lazima uombewe kibali hamtaki lazima myaoge mabomu ya machozi. Kudos tuu Polisi Kagera kwa kuyatawanya hayo Mavunjifu ya Amani.
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] umenichekesha sana

Halafu kibaya zaidi Lowasa sio mtu wa kuongea hovyo hovyo ,hivyo ukimya wake unatisha ,yaani unashindwa kubashiri next move yake
Ndio maana hata mhe alisema amepokea muujiza!
 
Nazidi kushawishika kuwa huyu "fisadi" alipata kura zaidi ya zilizo tangazwa na Lubuva
 
Hicho kitu tumelishwa sisi au nyie ambao mnaweza kuaminishwa kuwa kinyesi ni keki na mkala. Mnapiga kelele Rais hafati sheria huku nyinyi hizo sheria mnazisigina na mnataka muonekane mko sawa. Hata wapiga vigodoro usiku huwa wanaomba vibali iweje isiwe nyinyi au mnajifanya watoto wa mfalme?

Sheria iko wazi mkusanyiko wowote ule lazima uombewe kibali hamtaki lazima myaoge mabomu ya machozi. Kudos tuu Polisi Kagera kwa kuyatawanya hayo Mavunjifu ya Amani.
Kwani ilikuwa ni maandamano au alikwenda kutoa mkono wa pole na rambi rambi kwa wahanga!?.
[HASHTAG]#MunguTuacheTufe[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom