Mabomu msafara wa Lowassa, hii inaashiria nini?

Mabomu msafara wa Lowassa, hii inaashiria nini?

wengine pia walidumaa kutokana na ukisefu wa lishe bora usisahau hilo,wala elimu zao zisikutishe maana wamezipata kwa shida kweli kweli.nakumbuka wakati nasoma Mzumbe sekondari kuna jamaa yangu O level alipata one ya 17 nikamwambia ndugu umefeli maana muda aliokuwa anatumia prep na alichopawa were inversely proportional
Unatuaibisha sana kwa post zako za kijinga hizi. MTU aliyesoma Mzumbe na kulala Shaaban Robert , Mkwawa, Karume au Mirambo hawezi mpuuzi kama wewe!!
 
Ulimbukeni ni mzigo mkubwa sana.Na hili ndio tatizo la mfalme ndio maana hata wafalme walikuwa wanachaguliwa kwa busara zao.Dee key teta hawezi kuwa na busara na limbukeni hawezi kuepuka majivuno na roho ya kwa nini.
Ni ushamba tu unamsumbua huyo jamaa, kwanza kwa familia ayotoka hakutegemea kuwa hata siku moja atakuja kuwa kiongozi wa juu, kwahiyo ni kama zari.

Mtu kalelewa kimasikini hadi kaathilika akili, hadi akimuona mtu na maisha yake mazuri anaona wivu, najua sasa analala ile mbaya kwenye bangaluu letu.

Afu akiangalia kulia na kushoto analindwa yaani baaasiii anajiona yeye ndo mungu wa Tanzania, ni full kupelekesha watu bila utaratibu.
 
Ulimbukeni ni mzigo mkubwa sana.Na hili ndio tatizo la mfalme ndio maana hata wafalme walikuwa wanachaguliwa kwa busara zao.Dee key teta hawezi kuwa na busara na limbukeni hawezi kuepuka majivuno na roho ya kwa nini.
Hakika kigezo kilikuwa "HEKIMA"....Kumbe hii kitu inaitwa HEKIMA ni kila kitu ktk uongozi.
Kisa kimoja na Mfalme Suleiman na Wamama wawili waliokuwa wanagombania mtoto kinatupa fundisho nini maana ya hekima na si "maguvu na ukali wa harakaharaka.

Wamama wale wawili walipelekwa kwa Mfalme Suleiman,wakigombea mtoto mmoja,kila mmoja wa wale wanawake wawili walikuwa wanasema yule ni mtoto wao.Kwa hekima kubwa Mfalme Suleiman alipata wakati mgumu kujua haswaa ni nani Mama halali wa mtoto yule.Alijipa muda na kutumia hekima.Hakutaka "kumtumbua" mtu,bali alijipa muda wa kutafakari.

Aliwaita wamama wote wawili akiwa na mtoto mkononi,kama Mfalme alihitaji kutoa hukumu yenye HAKI.Akawaambia kwa sbb huyu mtoto wote mnamgombania,basi suluhisho ni moja...Mimi kama mfalme nitaamuru mtoto huyu achinjwe hadi kufa,ili nyote wawili mumkose na ugomvi uishe.

Yule Mama asiye mwenye mtoto akaripuka kwa furaha,akishabikia uamuzi huo na kusema ni bora achinjwe na tukose wote.Mama mwenye mtoto,akaona uchungu juu ya mwana wake aliyemzaa...Akamwambia mfalme,naomba huyu mtoto umpe huyu mwenzangu kuliko kumchinja na wote tukakosa.Mfalme kwa hekima zake akasema basi wewe uliyetaka asichinjwe huyu kweli ni mwana wako.Haya mtwae na uondoke nae.

HEKIMA ni kila kitu ktk uongozi!!Hekima huamua mambo kwa kiasi...Bila jazba na visasi na nchi ikasonga mbele.
 
Kama polisi wamekosea walalamikaji wana haki ya kwenda mahakamani.
 
wengine pia walidumaa kutokana na ukisefu wa lishe bora usisahau hilo,wala elimu zao zisikutishe maana wamezipata kwa shida kweli kweli.nakumbuka wakati nasoma Mzumbe sekondari kuna jamaa yangu O level alipata one ya 17 nikamwambia ndugu umefeli maana muda aliokuwa anatumia prep na alichopawa were inversely proportional
Kweli mkuu hata Mimi kuna maclass mate wangu, nawafahamu vizuri, walikuwa wanasoma kwa shida sana pale Musoma Tech. but leo wengi ni walimu wa secondary yaani unakutana na mtu full kujiona kama kabadilika sana, yaani kujitapa tu wakati hata robo ya mafanikio yangu wengine hawajayafikia ni full vumbi tu.
 
Tuwekee copy ya kibali cha lipumba kwenda kuvunja office za CuF hapa au ule haukuwa mkusanyiko?
Lipumba alitumia haki yake ya kikatiba kama mwenyekiti wa CUF. Na walipeleka taarifa kuwa mwenyekiti kazuiwa kuingia ofisini ndio maana akaomba msaada wa Polisi. Mikutano ya ndani ya chama imeruhusiwa au huna taarifa?

Narudia tena mkusanyiko wowote usio na kibali cha serikali ni batili. Wangevunja kiuno huyo mtu wenu ili ajue kuwa Wasio ma akili na wafata upepo mwisho wao ni ufipa.
 
Fanyeni kazi maandamano ya nini? Kama hamna cha kufanya mjini hapo Rufiji kuna pori mkalime nyanya na matikiti Maji yanalipa kuliko maandamano ya Ulipo tupo na 4U!
Kwanza siko Tanzania japokuwa Mimi ni Mtanzania halisi, pili nina uwezo wa kukulisha wewe na familia yako bila kufanya kazi yoyote maisha yenu yote na mnakula mnachotaka kila siku na posho za kutoka out nawapa.

Labda kama unashamba unahitaji mshaada wa mtaji ili uweze kujiajili uondokane na aibu ya dume zima kushinda Lumumba na kitecno chako kupiga kelele ili upate ujira wa buku saba ili familia ipate kula ni PM tuongee nione malengo yako ikiwa poa nikupige tafu.
 
Ni ushamba tu unamsumbua huyo jamaa, kwanza kwa familia ayotoka hakutegemea kuwa hata siku moja atakuja kuwa kiongozi wa juu, kwahiyo ni kama zari.

Mtu kalelewa kimasikini hadi kaathilika akili, hadi akimuona mtu na maisha yake mazuri anaona wivu, najua sasa analala ile mbaya kwenye bangaluu letu.

Afu akiangalia kulia na kushoto analindwa yaani baaasiii anajiona yeye ndo mungu wa Tanzania, ni full kupelekesha watu bila utaratibu.
Duh wewe umesema ukweli na msema kweli ni mpenzi wa mungu,hajawahi kufikiria kuwa Rais kama Edo,Lipumba,Maalim, kwa hiyo akiitwa ni chaguo la mungu watu wasichukie.
 
Duh wewe umesema ukweli na msema kweli ni mpenzi wa mungu,hajawahi kufikiria kuwa Rais kama Edo,Lipumba,Maalim, kwa hiyo akiitwa ni chaguo la mungu watu wasichukie.
Bora kuwa na kiongozi kutoka familia bora, kuliko hawa walalahoi ni shiiidaaa.
 
Inashangaza sana!!Huyu Mzee wanamuandama sana...Mpaka sasa tunaanza kuamini kweli walimuibia kura zake.Maana yaani huku na huko ni kufitini tu.Walianza kwa kumzushia ugonjwa,wengine wakaanza wao kufa na wengine sasa tumeona kwenye kurasa za mbele za magazeti wakiwa vitandani wanapewa pole.Mungu apishie mbali wanaweza kutangulia wao na jamaa akaendelea kubaki.

Mwanadamu hajakamilika,inawezekana ni kweli huyo Eddo ni "Fisadi" mkubwa sana...Lkn ni dhahiri sasa kuwa huyo Eddo ni "Mtu mwenye hekima" sana ktk wanasiasa wa level yake.Ana kifua,anastahimili,yote yanayotupiwa kwake anabariki na kusamehe...Muda wote tabasamu na maneno ya kusamehe.Alaumu mtu wala hatukani mtu...Amekaa katikati ya wale waliomtukana miaka mingi na akasema "Tusameheane na tusonge mbele"...Aliokaa nao miaka zaidi ya 40 wakimpenda na kumpa vyeo ndio leo wanamtukana na kumsimanga.Lkn amekaa kimya,akipata muda wa kujibu atasema "Nimesamehe,sina kinyongo".

Walimwambia kajiny....ea...Mbele ya mke,watoto na wajukuu wake.Alitabasamu na kusema "Siasa zao si za kistaraabu".Akapiga moyo konde na kwenda mbele....Sikuwahi kumpenda huyu jamaa,lkn mapito yake yamenifundisha kitu kikubwa sana ktk ulimwengu huu na walimwengu!!SILAHA KUBWA YA KUKABILIANA NA MAJARIBU NI UKIMYA MKUU NA HEKIMA!

Kuna jamaa yeye akitekenywa kidogo tu anaibuka...Sijaribiwi,ooooh ntafunga mtu!!Oooh anayeficha sukari atahama nchi!Mara wenye hela na matajiri lazima waishi kama Mashetani!!Akistuliwa kidogo utasikia natumbua mtu sasa hivi...Watu Ijumaa walikuwa wanapanda ndege wanaenda Dubai,Jpili wanarudi na J3 wapo kazini...Hawa utawala wangu Dubai wataisikia!!ha ha ha ha hizi ni "Poverty Mentality"....Mtu anafikiri kuishi kimasikini ndio sifa...Yaani fikra za kimasikini zimeganda akilini mpaka mtu anaona kuishi maisha mazuri ni dhambi ila kuishi kimasikini ndio fahari.

Huyu akiona watu wanaenda Ibiza weekend anaumia....Hataki watu waende na familia Znz weeknd na jpili warudi Dsm....Edward unawafundisha sana watu nini maana ya "HEKIMA"

Sasa ndio nagundua..Mfalme Suleimana na ufahari wake wote,alipoambiwa na Mungu anataka apewe nini?badala ya kuomba majeshi na watumwa wengi na fahari ya mifugo....Aliomba HEKIMA!
Big big point
 
Anafanya siasa kwenye maafa
Siasà gani kafanya?? Kumbuka nayeye ni kiongoz mkubwa so anawajibu wakuonyesha kushiriki kwenye najanga Kama haya, mbona mpaka wasanii wameenda. Nakuchangia ?? Je!! nawao wanafanya Sanaa ??ebu acheni chuki za kipuuzi
 
Woga wanamwogopa kama ukoma, wanatetemeka. Wa nakumbuka mafuriko na walisema anasomba watu kwa malori, sasa ukweli utadhiirika na ikiwa hivyo watahaibika.
 
Back
Top Bottom