Mabomu msafara wa Lowassa, hii inaashiria nini?

Mabomu msafara wa Lowassa, hii inaashiria nini?

tikatika

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
2,330
Reaction score
4,123
Maafa yalioikumba Tanzania huko Kagera na sehemu zingine yameleta simanzi kwa watanzania wengi. Hiyo imewalazimu watu wa kada tofauti tofauti kufika eneo lile. Kuanzia wa upinzani na CCM na serikali, mpaka majirani kama Kenya wamefika.

CCM wametembelea bila shida, Waziri Mkuu bila shida, upinzani akina Mbowe na Mbatia walipata figisu figisu kidogo.

Lakini alipoingia Lowassa police wakajaza magari mafuta mabomu wakapakia, bunduki wakazikoki na hatimaye wakatawanya watu wanaompokea anapowasili kwanini? Kwani hao wengine hawakupokelewa na watu?

Swali Lowassa ana nini kibaya katika Serikali hii?
Kwanini Serikali inamwandama kila anapokwenda?
 
Jamaa ana nyota ya Asali na maziwa mana anauwezo wa kuwapeleka wananchi katika nchi ya viwanda hasa kwa msisitizo wa elimu,elimu,elimu na kuuchukia umasikini siyo wengine wanaupenda umasikini na hawawataki mema wananchi wao.
 
Inashangaza sana!!Huyu Mzee wanamuandama sana...Mpaka sasa tunaanza kuamini kweli walimuibia kura zake.Maana yaani huku na huko ni kufitini tu.Walianza kwa kumzushia ugonjwa,wengine wakaanza wao kufa na wengine sasa tumeona kwenye kurasa za mbele za magazeti wakiwa vitandani wanapewa pole.Mungu apishie mbali wanaweza kutangulia wao na jamaa akaendelea kubaki.

Mwanadamu hajakamilika,inawezekana ni kweli huyo Eddo ni "Fisadi" mkubwa sana...Lkn ni dhahiri sasa kuwa huyo Eddo ni "Mtu mwenye hekima" sana ktk wanasiasa wa level yake.Ana kifua,anastahimili,yote yanayotupiwa kwake anabariki na kusamehe...Muda wote tabasamu na maneno ya kusamehe.Alaumu mtu wala hatukani mtu...Amekaa katikati ya wale waliomtukana miaka mingi na akasema "Tusameheane na tusonge mbele"...Aliokaa nao miaka zaidi ya 40 wakimpenda na kumpa vyeo ndio leo wanamtukana na kumsimanga.Lkn amekaa kimya,akipata muda wa kujibu atasema "Nimesamehe,sina kinyongo".

Walimwambia kajiny....ea...Mbele ya mke,watoto na wajukuu wake.Alitabasamu na kusema "Siasa zao si za kistaraabu".Akapiga moyo konde na kwenda mbele....Sikuwahi kumpenda huyu jamaa,lkn mapito yake yamenifundisha kitu kikubwa sana ktk ulimwengu huu na walimwengu!!SILAHA KUBWA YA KUKABILIANA NA MAJARIBU NI UKIMYA MKUU NA HEKIMA!

Kuna jamaa yeye akitekenywa kidogo tu anaibuka...Sijaribiwi,ooooh ntafunga mtu!!Oooh anayeficha sukari atahama nchi!Mara wenye hela na matajiri lazima waishi kama Mashetani!!Akistuliwa kidogo utasikia natumbua mtu sasa hivi...Watu Ijumaa walikuwa wanapanda ndege wanaenda Dubai,Jpili wanarudi na J3 wapo kazini...Hawa utawala wangu Dubai wataisikia!!ha ha ha ha hizi ni "Poverty Mentality"....Mtu anafikiri kuishi kimasikini ndio sifa...Yaani fikra za kimasikini zimeganda akilini mpaka mtu anaona kuishi maisha mazuri ni dhambi ila kuishi kimasikini ndio fahari.

Huyu akiona watu wanaenda Ibiza weekend anaumia....Hataki watu waende na familia Znz weeknd na jpili warudi Dsm....Edward unawafundisha sana watu nini maana ya "HEKIMA"

Sasa ndio nagundua..Mfalme Suleimana na ufahari wake wote,alipoambiwa na Mungu anataka apewe nini?badala ya kuomba majeshi na watumwa wengi na fahari ya mifugo....Aliomba HEKIMA!
 
Maafa yalioikumba tanzania huko kagera na sehem zingine yameleta simanz kwa watanzania wengi. Hiyo imewalazimu watu wa kada tofauti tofaut kufika eneo lile . Kuanzia wa upinzani na ccm na serikali, mpaka majirani kama kenya wamefika.

Ccm wametembelea bila shida, wazir mkuu bila shida , upinzani akina mbowe na Mbatia walipata figisu figisu kidoogo.!!

Lakin alipoingia Lowassa police wakajaza magari mafuta mabomu wakapakia, bunduki wakazikoki, na hatimaye wakatawanya watu wanaompokea anapowasili kwann??
Kwan hao wengine hawakupokelewa na watu??

Swali lowassa ana nn kibaya katika serikali hii??
Kwann serikali inamwandama kila anapokwenda??
Aache kutafuta kick kwa kutumia majanga! Kama ana Pesa akachangie madawati na huduma zingine!
 
Maafa yalioikumba tanzania huko kagera na sehem zingine yameleta simanz kwa watanzania wengi. Hiyo imewalazimu watu wa kada tofauti tofaut kufika eneo lile . Kuanzia wa upinzani na ccm na serikali, mpaka majirani kama kenya wamefika.

Ccm wametembelea bila shida, wazir mkuu bila shida , upinzani akina mbowe na Mbatia walipata figisu figisu kidoogo.!!

Lakin alipoingia Lowassa police wakajaza magari mafuta mabomu wakapakia, bunduki wakazikoki, na hatimaye wakatawanya watu wanaompokea anapowasili kwann??
Kwan hao wengine hawakupokelewa na watu??

Swali lowassa ana nn kibaya katika serikali hii??
Kwann serikali inamwandama kila anapokwenda??


Kura milioni sita si jambo dogo kaka!?
 
Back
Top Bottom