SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,916
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa vigezo gani CAF waliitangaza Al Ahly kuwa ni timu bora ya karne ya 20? Wengi mnadhani ni kwa kubeba makombe mengi kuliko timu nyingine yoyote lakini siyo kweli.
Karne ya 20 iliisha 31/12/2000. Katika mafanikio ya Al Ahly hadi kufikia tarehe hiyo, katika mashindano yanayoandaliwa moja kwa moja na CAF Al Ahly walichukua makombe 6 na moja la mabara (Afro-Asia Cup).
Wakati huo huo, Zamalek hadi kufikia mwisho wa karne ya 20 ilikuwa imechukua makombe 7 ya CAF na mawili ya mabara (Afro-Asia Cup).
Kilichoipa tuzo hiyo Al Ahly ni system ya kuhesabu point iliyotumiwa na CAF ambayo iliyapa points tofauti makombe na hatua mbalimbali ambazo timu ilifikia, kama wanavyofanya sasa hivi kwenye ranking zao. Kutokana na kutokubaliana na hilo, ilifika wakati Zamalek nao wakajitangaza kuwa wao ndiyo Club Sahihi ya Karne. Huu ulikuwa ni mgogoro mkubwa uliodumu kwa miaka mingi.
Al Ahly toka karne hii ya 21 imeanza ndiyo wamekuwa hawana mpinzani linapokuja suala la makombe.
Hivi TFF wakisema watangaze Club Bora ya Tanzania kwa Karne ya 20 wakizingatia mafanikio katika ligi ya ndani pamoja na kwenye mashindano ya CECAFA na CAF, timu gani inastahili kutwaa tuzo hiyo?