Mabasi kutoka mikoa ya mbali kulala Morogoro

Mabasi kutoka mikoa ya mbali kulala Morogoro

Mwanza, Kagera, Kigoma, sawa... ila hiyo mikoa yako ya Tukuyu, Songea si sawa.

Niliwahi panda HOOD enzi zile Dar - Songea nilifika saa 12 jioni. Gari ilikua inapaa.
 
Hili la kulala njiani ni zuri kuliko safari kuishia njiani hapo lazima gharama ziongezeke lakini hii ya kuzuiwa mnalala kwenye basi gharama kubwa zitoke wapi?
 
Si ndio maana tumeagiza ndege zaidi, tusipominya huku kwenye mabasi kule tutapata hasara.

Kinachofuata mtalala kibaha mpaka wengi mje kupanda bombadier hehehehehe.
[emoji15] [emoji15]
 
Mkuu ameagiza ndege Nne msijari watu mwanza mtapanda bure muache kuchafua mji wetu wa Moro. jiandaeni kupanda ndege bure
 
Mkuu mimi nakumbuka miaka ya 80s mabasi yalikuwa yanatembea usiku, kwa mfano unachukua sleeping coach to mwanza unaondoka ubungo saa mbili ya usiku unalaalaa weee asubui uko nyegezi unaenda kweye mishe mishe unageuka usiku wake to dar unaingia ubungo saa mbili asubuhi unaenda kuoga halafu ofisini.
Ubungo 80's???!?? Hapakuwa na stand pale Ubungo terminal.
Nakumbuka pale Ubungo enzi za single lane palikuwa panaitwa Ubungo minazi. Mkifika mnanunua mikate kisha mnaanza mwendo
 
Kipi kizuri, ulale morogoro kisha ufike salama kesho yake au uruhusiwe kusafiri usiku halafu uvamiwe na majambazi, au kupata ajali usiku, (kumbuka usiku ndio wakati gari za mizigo zinasafiri pia madereva wanakuwa wamechoka)
Bus la new force limepata ajali mchana kweupe ndiyo maana ikaitwa ajali
 
Mwanza, Kagera, Kigoma, sawa... ila hiyo mikoa yako ya Tukuyu, Songea si sawa.

Niliwahi panda HOOD enzi zile Dar - Songea nilifika saa 12 jioni. Gari ilikua inapaa.
ni kweli mkuu,miaka ya nyuma kidgo gari zilikuwa zinatembea sana na zilikuwa chache mfano kulikuwa na bus la hood na hekima dar kyela,tukuyu ilikuwa inaingia jion kweupe kabisa saa 11/12....
 
Wanajamvi, imekuwa ni jambo la kawaida kwa mabasi kutoka Mwanza Tukuyu Songea Mwanza Kigoma kuzuiliwa Morogoro.

Pamoja na nia nzuri ya usalama lakini abiria wanateseka sana hasa ukizingatia kipindi hiki gharama za maisha Imekuwa juu.

Jana nilikuwa mhanga baada ya kukwama mji kasoro bahari nikitokea Mwanza.

Nadhani sasa wadau ni wakati muafaka wa kufuta safari za moja kwa moja kutoka katika hiyo mikoa ili abiria ajue kabisa kwamba atalala njiani.

Nawasilisha wakuu kwa mawazo yenu ju ya jambo hili.
Mabasi yanayolala msamvu ni Yale ya Kigoma,mwanza, Zimbabwe, Malawi, sumbawanga n.k tukuyu na kyela hayalali
 
Utaratibu huu umeanza lini basi inatoka Mwanza ilale morogoro sio kweli!?

Kawaida basi inayotoka Mwanza inaripoti Ubungo temino saa 5 au 6 usiku
Nna wiki ya 3Dsm nmetoka Mwanza hatukalala morogoro.
 
Mabasi ya Mwanza yanatakiwa yazuiwe Dodoma....maana huwa yanafika jioni sana sasa mwendo wanaotumia kuitafuta Morogoro ni hatari tupu mie SIKU hizi nimeua niwe nashukia Dom tu
 
Back
Top Bottom