KERO DART imepandisha Nauli ya Mabadi Mapya MBEZI-KIVUKONI/GEREZANI bila taarifa

KERO DART imepandisha Nauli ya Mabadi Mapya MBEZI-KIVUKONI/GEREZANI bila taarifa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa muda mrefu wananchi wa Dar es Salaam tumekuwa tukitegemea huduma za mabasi ya UDART kwa usafiri wa kila siku.

Awali, nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara ilikuwa Tsh 500 kwa umbali wa takribani kilomita 12, huku safari ya Kimara hadi Kivukoni/Gerezani ikiwa Tsh 750 na baada kupandishwa kimyakimya mpaka Tsh 1000. Kabla ya uchaguzi wa mwaka jana kulikuwa na mabasi ya moja kwa moja kutoka Mbezi hadi Kivukoni/Gerezani, lakini huduma hiyo ilisimamishwa na abiria kulazimika kushuka Kimara na kukata nauli nyingine.

Mwezi Januari mwaka huu huduma ya Mbezi ilirejeshwa, lakini kwa kutumia mabasi ya zamani yaliyokuwa yanaishia Kimara huku nauli ya Tsh 500 ikiendelea kubaki ileile.

Kwa siku za hivi karibuni, UDART wameanza tena safari za moja kwa moja kutoka Mbezi hadi Kivukoni/Gerezani kwa kutumia mabasi mapya yanayotumia gesi. Hata hivyo, jambo linalozua maswali ni kupandishwa kwa nauli kutoka Tsh 1500 hadi Tsh 2000 kwa kile kinachoitwa huduma ya “VIP”. Cha kushangaza zaidi, hata mfumo wa tiketi bado haujatambua rasmi nauli hiyo mpya kwani abiria hukatwa Tsh 1000 mara mbili jambo linaibua harufu ya ufisadi.

Sisi watumiaji tunauliza:Je, LATRA wanafahamu ongezeko hili la nauli na wamelidhinisha kwa msingi gani? Katika kipindi ambacho nauli za daladala nchini zimekuwa zikiongezwa kwa tofauti ndogo ya Tsh 100–200 tu, ni kwa nini hapa kuwe na ongezeko kubwa kiasi hiki?

Aidha, ikiwa mabasi haya mapya yanatumia gesi ambayo gharama yake ni nafuu zaidi kuliko petroli au dizeli, sababu ya kupandisha nauli kwa kiwango hiki ni ipi?

Pia, huduma hizi zinaitwa “VIP” lakini hali ndani ya mabasi bado ni ileile ya kujazwa abiria kama kawaida. Ikiwa ni huduma ya VIP kweli, basi viwango vyake vinapaswa kuonekana wazi kama ilivyo kwenye mabasi ya mikoani, SGR, meli au hata ndege.

Tunaiomba LATRA pamoja na mamlaka nyingine husika kulifuatilia jambo hili kwa karibu ili kuondoa malalamiko na hisia za wananchi kuonewa. Wananchi wanahitaji huduma bora, zenye uwazi na zinazozingatia hali halisi ya maisha yao.
 
Back
Top Bottom