Mabasi kutoka mikoa ya mbali kulala Morogoro

Mabasi kutoka mikoa ya mbali kulala Morogoro

Wanajamvi, imekuwa ni jambo la kawaida kwa mabasi kutoka Mwanza Tukuyu Songea Mwanza Kigoma kuzuiliwa Morogoro.

Pamoja na nia nzuri ya usalama lakini abiria wanateseka sana hasa ukizingatia kipindi hiki gharama za maisha Imekuwa juu.

Jana nilikuwa mhanga baada ya kukwama mji kasoro bahari nikitokea Mwanza.

Nadhani sasa wadau ni wakati muafaka wa kufuta safari za moja kwa moja kutoka katika hiyo mikoa ili abiria ajue kabisa kwamba atalala njiani.

Nawasilisha wakuu kwa mawazo yenu ju ya jambo hili.
Kipi kizuri, ulale morogoro kisha ufike salama kesho yake au uruhusiwe kusafiri usiku halafu uvamiwe na majambazi, au kupata ajali usiku, (kumbuka usiku ndio wakati gari za mizigo zinasafiri pia madereva wanakuwa wamechoka)
 
Wa kyela anawahi wa tukuyu analala moro??
Hayo mabasi mnayopanda ni mikangafu, yanafika moro saa tano na kuendelea hivyo yanazuiwa.
Siyo mikangaf....unadhani uendeshe kilometa 80 kwa saa utafika? Hizo kilometa 80 kwa saa gari ni kama linakwenda kupaki. Na polisi wetu wamekaririshwa sheria badala ya kutumia akili. Wanatumia uchochoro wa udhaifu wa sheria kujipatia rushwa. Mitochi barabarani utafikiri taa za barabarani bwana!!!! Lo!
 
Movements za watu na shughuli zikienda haraka basi na uchumi wa nchi husika utakwenda haraka, hawa jamaa wanadhani wanawakomoa wenye mabasi bila kujua kuwa yale masaa wanayopoteza pale Morogoro ni uchumi unaopotea.
Utasemaje kuwa kutoka Dodoma saa nne usiku hadi Mrogoro saa saba ni salama lakini Moro-Dar hakuna usalama!
 
Mi najua mabas ya Musoma, Kagera, kigoma... Ndo yanayolala morogoro coz yanachelewa kufika... Kwa mabasi ya mwanzalabda bovu tuu likachelewa kufika, coz last week nlipanda gar frm dar to musoma, tukalala mwanza, na wakat wa kurud tukalala moro na tulikua na OTA ya kigoma, mi nlikua na JM luxury, pia kulikua na gar nyingne za kagera.. Hakukua na gar ya mwanza hata moja
 
Wa kyela anawahi wa tukuyu analala moro??
Hayo mabasi mnayopanda ni mikangafu, yanafika moro saa tano na kuendelea hivyo yanazuiwa.
Hapana mkuu sasa hivi wanadhibiti sana mabasi yote kina Najumnisa
 
Ila hata mabasi ya mwendo kasi siku hizi ikipanda ni kichefuchefu, spidi ya kobe, hawa polisi waache ujinga.
 
Wa kyela anawahi wa tukuyu analala moro??
Hayo mabasi mnayopanda ni mikangafu, yanafika moro saa tano na kuendelea hivyo yanazuiwa.
mkuu,gari zote zinazotoka kyela zinapita tukuyu na hakuna gari inanzia tukuyu....so kyela=tukuyu kama ni basi
 
Kipi kizuri, ulale morogoro kisha ufike salama kesho yake au uruhusiwe kusafiri usiku halafu uvamiwe na majambazi, au kupata ajali usiku, (kumbuka usiku ndio wakati gari za mizigo zinasafiri pia madereva wanakuwa wamechoka)
bhas kama wanakuwa wamechoka inatakiwa gari ikifika dar ipumzke isigeuze siku iyo au kufanya safar nyingne...kwa maana bado gar inakuw imechoka pia madereva
 
Kwahiyo kutoka hapo morogoro kwenda dar pana ajali ndio manake mnalala hapo morogoro?.Mbona kenya ni 24 hrs na hakuna ajali. Waweke madereva watatu mmoja ananzia mwanza mpaka Manyoni a na fika anakabidhi chombo, mwingine anapokea Manyoni mpaka moro anakabidhi chombo, mwingine anapokea moro mpaka dar chombo kinafika.
 
Wanajamvi, imekuwa ni jambo la kawaida kwa mabasi kutoka Mwanza Tukuyu Songea Mwanza Kigoma kuzuiliwa Morogoro.

Pamoja na nia nzuri ya usalama lakini abiria wanateseka sana hasa ukizingatia kipindi hiki gharama za maisha Imekuwa juu.

Jana nilikuwa mhanga baada ya kukwama mji kasoro bahari nikitokea Mwanza.

Nadhani sasa wadau ni wakati muafaka wa kufuta safari za moja kwa moja kutoka katika hiyo mikoa ili abiria ajue kabisa kwamba atalala njiani.

Nawasilisha wakuu kwa mawazo yenu ju ya jambo hili.
Wewe huna taarifa sahihi. Mabasi yanayolala Morogoro ni ya Bukoba, kigoma na Musoma, mengine yote yanafika Dar japo inakuwa usiku.
 
Kwa mabasi yanayotoka Mbeya (Tukuyu, Tunduma, Kyela) kulala Moro itakuwa ni kuwachosha abiria kwa sababu basi huwa zinafika hapo msavu saa 9 au 10 jioni muda ambao ni mapema kbs.
 
Yah! Huwa inasaidia kuwafanya madereva wapimzike kidogo kuliko kulazimisha kufika mwisho wa siku ajali zinazidi kutumaliza, nadhan si jambo baya kwa upande wangu.

Nakubaliana na wazo hili, ni kweli kabisa kuwa madereva muda huo wa usiku wanakuwa wamechoka sana kutokana na safari ndefu na pia kwavile Traffice Police na tochi zao hazipo usiku, mwendo wanaokwenda nao ni wa kasi sana na hivyo uwezekano wa kusababisha ajali ni mkubwa.. Pengine ni busara tu kwa wahusika Sumatra kuweka utaratibu mzuri ili abiria na wamiliki wa mabasi waweze kufahamu ratiba na mazingira ya maeneo ambapo mabasi ya abiria yanalazimika kulala, ili maeneo hayo yaandaliwe ili kuwepo huduma zote muhimu na usalama wa abiria pia uzingatiwe
 
Huu no upuuzi tu wa kitanzania, huwezi kutengeneza 24hrs economy kwa kulaza watu njiani, polisi wafanye kazi yao waweke road blocks kila baada ya umbali fulani, nchi ya amani ya nchi hii na barabara zilivyoboreshwa kuwaambia watu walale njiani ni kudharau intelligence ya watanzania inamaanisha hawawezi kujisimamia kuanzia serikali yenyewe hadi watumia Barabara.
kwa mfano ukiingia dar saa saba usiku utafanya shughuli gani za kiuchumi?
 
Back
Top Bottom