Elections 2010 Mabango ya JK yaliyofichwa

Martinez

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
525
160
DSC01238.jpg

DSC01234.jpg


ELIMU BORA
CHAGUA CCM
CHAGUA KIKWETE
 
Ha ha ha haaaaaa, tuliahidi elimu bora tumetekeleza!!! inasikitisha sana. Bahati mbaya hao watoto moyoni wanasema asingekuwa yeye hata hapo wasingekaa. Mungu wangu na Mungu wa Watanzania wote nakuomba utufunulie kuujua ukweli tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Tuwachague viongozi ambao watatuongoza kwenye maendeleo ya kweli. Tazama wana wako hapo juu wanavyopata shida, Mungu ni imani yangu shida hizi wanazopata si kwa mapenzi yako Baba uliye juu, ila ni kwa kosa la watu wako ambao kwa sababu ya vipande vya khanga, fulana, kofia, pilau na pombe wakalewa wakawapa madaraka ya kuongoza nchi yako watu wasiokuwa na uwezo. Ndiyo maana ninakuomba sasa ukageuze mioyo yetu ukatuelekeze kutenda yaliyo mema kwa kufanya kucahgua viongozi wenye uwezo wa kutenda na siyo kunena, wenye uwezo wa kuthubutu na siyo kuota tu. Ameni
 
hii ndiyo tanzania bwana,hao utakuta ni lazima waimbe wimbo wa Tanzania Nakupenda...tena pale kwenye kibwagizo cha KWA MOYO WOTE inatakiwa waongeze sauti..
mwe mungu saidia watu hawa..
 
Hili ni tatizo la kujua vipaumbele vyetu kama taifa. Cha ajabu pamoja na kuwa na madarasa duni walimu duni, bado atakayekuja kukagua maendeleo ya hiyo shule (yaani wakaguzi) yeye atakuja na shangingi (Toyota Land Cruiser VX) la milioni 200. Tungekuwa tuna uwezo wa kupanga kwamba kati ya kiatu na soksi tutangulie nini, kutonunuliwa kwa mashangingi mawili kungeboresha maisha ya kielimu ya watoto hawa.

Mungu ibariki tanzania.
 
Inatia huruma. Itanisikitisha sana watu ambao wanaishi maeneo haya na wanamatatizo kama haya wadanganyike kuwa CCM itawaletea maendeleo.

CHAGUENI KIONGOZI MWENYE DIRA NA MWELEKEO WA KUWAKUMBOA WATANZANIA. SEMA HAPANA KWA CCM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi Hii ni tanzania au sudan...dah..

Ndugu, mimi niko Sudan, naomba nikusahihishe; Sudan wako Vizuri kiuchumi na miundombinu kuliko Tanzania, mgogoro wao wa Darfur usikufanye ufikiri kwamba Tanzania inaizidi Sudan kimaendeleo.....

TZ resources nyingi, serikali ya CCM ndio Tatizo....
 
Nimependezwa na kichwa cha habari na picha zenyewe.

Huo ndiyo ukweli wa Jk na CCM yake. Ni wepesi kujisifia ya kuwa wametekeleza Ilani ya uchaguzi kumbe utekelezaji huo ni kuhakikisha tunabaki kwenye umasikini milele.

mtaji mkubwa wa CCM kisiasa ni umasikini wetu tu na wala siyo vinginevyo
 
Mtaji wa CCM ni Ujinga na Umaskini wa watanzania wengi.Ndio maana wanaendeleza hayo mabango ya mafichoni ili wasije umbuka.
 
Mi nimempenda mwalimu................... very committed!

Huyu mama mwalimu ni mzalendo, ni shujaa, ni mtu wa Mungu namwombea Mungu amzidishie mema. ILA NAYE SIJUI AMEKWISHA AMUA KURA YAKE ATAMPA NANI OCT 31? Kada mmoja rafiki yake yangu wakati akirejea leo kutoka katika kampeini na shati lake la kijani amenin'goneza mbunge nitachagua wa chama changu lakini RAIS NI SLAA!!!! Nilishangaa sana, akaongeza unafikiri mimi ndiyo sitaki wanangu wapate elimu nzuri?
 
hii ndiyo tanzania bwana,hao utakuta ni lazima waimbe wimbo wa Tanzania Nakupenda...tena pale kwenye kibwagizo cha KWA MOYO WOTE inatakiwa waongeze sauti..
mwe mungu saidia watu hawa..

maisha bora kwa kila mmtanzania,hebu tubadilike sisi sio mbayuwayu
 
Inatia huruma. Itanisikitisha sana watu ambao wanaishi maeneo haya na wanamatatizo kama haya wadanganyike kuwa CCM itawaletea maendeleo.

CHAGUENI KIONGOZI MWENYE DIRA NA MWELEKEO WA KUWAKUMBOA WATANZANIA. SEMA HAPANA KWA CCM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mimi nilisema hapana miaka mingi iliyopita
 
Back
Top Bottom