๐— ๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฑ๐—ถ๐—น๐—ถ๐—ธ๐—ผ ๐˜†๐—ฎ๐—น๐—ถ๐˜†๐—ผ๐—ฝ๐—ผ ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐—ถ๐—ฃ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ฒ ๐Ÿญ๐Ÿฐ

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Apple imetoa simu ya iPhone 14 ambayo sio Pro (iPhone 14 ya kawaida). Mwaka huu iPhone ya kawaida itakuwa na iPhone 14 Plus ambayo ina ukubwa sawa na iPhone 14 Pro Max.

iPhone 14 inafanana na iPhone 13 katika mwonekano.
1662635089194.png

๐Ÿ”˜ Apple imetoa aina mpya ya simu ya iPhone 14 Plus. Ina kioo chenye ukubwa wa โ€ฆ..

๐Ÿ”˜ Ina uwezo wa kutambua mtu amepata ajali

๐Ÿ”˜ Ina uwezo wa mawasiliano ya satelite

๐Ÿ”˜ Kamera yake ina Advanced dual system ambayo ni toleo jipya la kushirikisha mfumo wa kamera mbili kuwa na ushirikiano mmoja katika kupiga picha na kurekodi. Tofauti yake sio kubwa sana katika quality ya video na picha ukiilinganisha na iPhone 13.

๐Ÿ”˜ Inatumia teknolojia mpya ya Bluetooth 5.3

๐Ÿ”˜ Inatumia chip ya A15 Bionic ambayo ni sawa na chip ya iPhone 13. Lakini GPU core za iPhone 14 zipo 5 (5-core) lakini iPhone 13 za mwaka jana zilikuwa na core 4 za GPU.

Wengi wamelalamika kuwa haina mabadiliko makubwa sana zaidi ya kuweka uwezo wa Satellite na kutambua kama mtu amepata ajali. Lakini mwonekano, kamera, chip na display ni ile ile kama ya iPhone 13.
1662635205759.png





CREDIT @itsapolloo
 
Apple hawana mpya sikuhizi wanazidiwa mpaka na tecno. Sim ileile ila wanasema wamebadilisha features
 
Jambo moja ambalo halisemwi sana ni kwamba iphone 14 za Marekani zina E-sim hivyo hazitakuja makumbusho maana haziingii line, taratibu Apple wanajitenga na Refurb zisizokuwa Certified.
Wakisha roll out iphones zenye esim dunia nzima, refub zitarudi tu.

Ni tech inayokuwa, hata hii mitandao yetu itaanza ku adopt.
 
Hakuna review pale.

Ile ni hands on & first impression.

Baada ya week 1/2 ndo utaona full review ya kueleweka.
Kweli kabisa hata mkbh kasema anasubiri azitumia week kadhaa ndipo atoe detailed review
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom