Mapokeo Mabaya ya Iphone 15

BROKE BOYS

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
13,218
39,049
Juzi tu hapa tulishuhudia Apple wakirelease brand mpya tofauti ikiweko na simu iphone 15 series. Iphone 15 haijapata mapokeo makubwa kama miaka ya nyuma kwa matoleo mengine, wengi wameonekana kutoikubali maana imekuja tofauti na matarajio yao.

Kutokana na tovuti mbalimbali za kibiashara zinaripoti simu hii haitafanya vizuri kama matoleo mengine yaliyopita. Licha ya kutoa toleo jipya pia shares za apple zimeendelea kushuka.

Kutokana na watumiaji wa iphone sehemu mbalimbali duniani wanasema iphone 15 haina utofauti na iphone 14, kwani apple wanachofanya kwa sasa nikubadili vitu vidogo tu afu wanaweka simu sokoni.

Kwa miaka mitano (5) mfululizo iphone wameshindwa kubadilisha hata muonekano wa Camera tu. Wanatumia muundo uleule wa Camera ila wanasema wameongeza ubora wa camera.

Je apple wamekosa ubunifu kwasasa? Maana kwasasa huawei Mate 60 pro ndo inafanya vizuri sokoni.

Haya ni baadhi ya maoni ya wadau mbalimbali ulimwenguni.

IMG_2769.jpg

IMG_2765.jpg

IMG_2766.jpg

IMG_2767.jpg

IMG_2768.jpg

IMG_2764.jpg

IMG_2763.jpg

IMG_2773.jpg
 
Iphone 15 pro max ukiikunja kwa mikono tuu inapasuka kwa nyuma.. Hii ni sababu imetengenezwa kwa Titanium materials ambayo Apple walijitapa ni magumu kushinda Aluminium.. Hii test aliifanya jamaa maarufu anayeitwa "Jerry Rigs Everything" kule Youtube.

Yani alitumia nguvu kidogo tu ikavunjika kwachaa.

Ila Iphone 15 na 15 plus zenye Aluminium zimesurvive hii test...
 
Back
Top Bottom