Uchaguzi serikali za mitaa ufanyike 2026. Je, kuna madhara yoyote?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,022
Je, haiwezekani kuahirisha uchaguzi wa serikali za mitaa mpaka 2026?

Hii itawezesha uchaguzi huo kusimamiwa na Tume Mpya Huru ya Uchaguzi badala ya Tamisemi.

Nadhani Watanganyika tusiwaige Wazanzibari kufanya chaguzi zote kwa wakati mmoja.

Nchi yetu ni kubwa sana ukilinganisha na Zanzibar.
 
Kwa hiyo umeshakubali 2025 uchaguzi mkuu utasimamiwa na Katiba hii tuliyonayo?

Ningekuelewa vizuri kama ungesema chaguzi zote mbili zihairishwe, hapo ulichofanya ni kama vile umeamua kuwapa CCM zawadi kubwa peke yao, halafu ile ndogo ukataka wagawane na wenzao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hiyo tume mpya kwa serikali isiyofuata misingi bora ya katiba kwa nchi zetu za kiafrika bado ni ndoto
 
Kwa hiyo umeshakubali 2025 uchaguzi mkuu utasimamiwa na Katiba hii tuliyonayo?

Ningekuelewa vizuri kama ungesema chaguzi zote mbili zihairishwe, hapo ulichofanya ni kama vile umeamua kuwapa CCM zawadi kubwa peke yao, halafu ile ndogo ukataka wagawane na wenzao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

1. Kuna wanaosema tumechelewa kuunda Tume Huru haiwezi kuundwa mwaka huu [ 2024 ] na kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.

2. Kuna wanaosema uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike pamoja na uchaguzi wa Raisi, wabunge, na madiwani, kwa usimamizi wa Tume Huru.

Mimi kwa mtizamo wangu naona tukichanganya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu Tume Huru itaelemewa na kutuletea matatizo.

Kutokana na mtizamo huo ndio maana nadhani ni busara zaidi uchaguzi wa serikali za mitaa ukasogezwa mbele mpaka 2026 ili uweze kusimamiwa na Tume Huru.

Je, wewe maoni yako ni yapi?
 
Kwanini unaona tukichanganya uchaguzi wa serikali za mitaa, na uchaguzi mkuu, Tume Huru itaelemewa na majukumu yake?

Kwasababu ya uchanga wake, au kuwa na watendaji wachache, au bajeti, skilled personnel au kitu gani kingine?

Mimi kwa upande wangu, nataka chaguzi zote mbili zihairishwe mpaka Tume Huru ipatikane, hili lifanyike kwa wakati na muda sahihi, huku kila mmoja akijua msimamo wetu kitaifa ni huu.

Muhimu kila mmoja akae kwenye position yake akijua uchaguzi mkuu na ule wa serikali za mitaa yote itafanyika kwa pamoja baada ya Tume Huru kupatikana, yafanyike maandalizi ya kuendana na hali hiyo ili muda ukifika, pasiwepo tena na hivi visingizio vya kutengeneza walivyovizoea kuja navyo kila mara.

..mtizamo wangu toka awali ni uchaguzi wa Raisi kutenganishwa na chaguzi zingine.

..pia Bunge likiwa ni mhimili unaojitegemea kwelikweli hakutakuwa na haja ya uchaguzi wa Raisi kufanyika wakati mmoja na uchaguzi wa bunge
 
Inawezekana kufanyika 2025 siku inayofuata baada ya Oct 30.

..Tume Mpya Huru ya Uchaguzi itakuwa bado changa.

..Tusiibebeshe mzigo mkubwa ktk wakati mfupi.

..Hii option niliyopendekeza inazima hoja ya kulazimisha uchaguzi ufanyike 2024 na usimamiwe na Tamisemi.
 
Kwa hiyo umeshakubali 2025 uchaguzi mkuu utasimamiwa na Katiba hii tuliyonayo?

Ningekuelewa vizuri kama ungesema chaguzi zote mbili zihairishwe, hapo ulichofanya ni kama vile umeamua kuwapa CCM zawadi kubwa peke yao, halafu ile ndogo ukataka wagawane na wenzao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Wanashiriki uchaguzi chini ya tume hizi za ccm
Alafu badaye wanaanza kulalamika

Ova
 
..Tume Mpya Huru ya Uchaguzi itakuwa bado changa.

..Tusiibebeshe mzigo mkubwa ktk wakati mfupi.

..Hii option niliyopendekeza inazima hoja ya kulazimisha uchaguzi ufanyike 2024 na usimamiwe na Tamisemi.
Tamisemi ni wakina nani
si hao hao ccm

Ova
 
..mtizamo wangu toka awali ni uchaguzi wa Raisi kutenganishwa na chaguzi zingine.

..pia Bunge likiwa ni mhimili unaojitegemea kwelikweli hakutakuwa na haja ya uchaguzi wa Raisi kufanyika wakati mmoja na uchaguzi wa bunge
Ni sawa kwa mtazamo wako.

Lakini kwangu naona ugumu wa mambo kwenye haya masuala ya uchaguzi tunayasababisha wenyewe, sioni haja ya kutenganisha chaguzi yoyote, tunaweza kufanya zote kwa pamoja tena very efficiently.

Kama pakiwepo mazingira bora ya uchaguzi, ushindani sawa bila upendeleo kwa yeyote, kukusanya kura, kuzisafirisha, kuzihesabu mpaka kutangaza washindi, naamini tutaepuka mambo mengi yanayokufanya uone uchaguzi ni jambo gumu linalohitaji kutenganishwa ili kulirahisisha.

Huu ugumu unaouona sasa mpaka utake uchaguzi fulani kutenganishwa na mwingine, unasababishwa na kutengeneza mazingira ya wizi yatakayowafaa wenye malengo nayo, ndio maana wanalazimisha mambo rahisi yawe magumu makusudi ili watimize malengo yao haramu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kusiwepo uchaguzi bila tume huru wala katiba mpya ni bora waachwe washiriki CCM na matawi yake kama TLP, UDP , NCCR , CHAUMA ila jumuiya ya kimataifa na waangalizi wa uchaguzi watatoa report yao kama ule ushenzi uliofanyika 2020.
 
..hapana.

..Tume Mpya Huru.

..Katiba iliyofanyiwa marekebisho madogo yanayowezesha uundwaji wa Tume Huru.
Nimekuelewa, je hayo yatawezekana ? Natamani kujua maoni na mapendekezo ya muundo wa hiyo Tume Mpya Huru na utendaji na uwajibikaji wake
 
..Tamisemi ni CCM.

..Mimi napendekeza Tume Mpya Huru iwe tayari kwa uchaguzi mkuu wa 2025.

..Uchaguzi wa serikali za mitaa uahirishwe mpaka 2026 ili uweze kusimamiwa na Tume Mpya Huru ya uchaguzi.
Naunga mkono hoja
Kushiriki uchaguz na tume hii
Ni kupoteza muda tu

Ova
 
Nimekuelewa, je hayo yatawezekana ? Natamani kujua maoni na mapendekezo ya muundo wa hiyo Tume Mpya Huru na utendaji na uwajibikaji wake

..yanawezekana.

..tatizo Watz tumefanya zoezi la kuunda Tume Huru kuwa gumu sawa na kutafuta dawa ya kutibu Kansa.
 
Back
Top Bottom