Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa wanaohitaji kuwa sehemu ya majaribio, mnakaribishwa...

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!

===== UPDATES======

Changes on the new version:

1) Kuna urahisi wa kufichua mambo mazito bila data zako zozote kuchukuliwa na bila post kwenda public kwanza (utaona button ya Fichua Uovu). Hii itasaidia hata wasio wanachama (baadae) kushiriki kikamilifu kupinga ufisadi na rushwa kwa ujumla.

2) Faragha ya mwanachama imelindwa zaidi, hakuna wa kujua wewe ni nani on JF bila wewe kumpa access ya kifaa chako (simu, tablet au pc). Tulipata vilio vya watu kuchunguliwa IDs tukaja na suluhu.

3) Unaweza kuchagua kutumia JF ikiwa light version, dark mode au dark blue mode (my favorite).

4) Maandishi ya sasa yanasomeka kirahisi zaidi na wenzetu wenye uoni hafifu. Wasioona kabisa lakini wana vifaa vya kusomea wataweza kuitumia JF kwa urahisi zaidi.

5) Soon kuna mambo mapya yanaanza kufanyika via JF, mabadiliko haya yamelenga kupokea yajayo kuanzia mwezi huu na kuendelea.

6) Ukiwa kwenye forum yoyote, huhitaji kubonyeza Page 2, Page 3, Page 4. Wewe vuta kwenda chini tu, mada zitakuja (scroll down).

Nitaendelea…
Mkuu Maxence Melo tungeomba mboreshe forum kwa kuweka poll app ikiwezekana, baadhi ya kura tuwe tunapigia kupitia jamii forum. Naomba kuwasilisha.

1656920568333.png
 
Hizi stick/special thread zinakera sana...
Kama inawezeka kuwe na ki button cha kuhide na ku unhide..zinakaa juu kabisa wakati siyo kila mtu anazifungua.

Mfn NMB special thread sina hata account nao ya nn sasa kuifungua?
 
Duu... baada ya haya marekebisho muda wangu wa kukaa huku jf umepungua sana.

Duu... baada ya haya marekebisho muda wangu wa kukaa huku jf umepungua sana.
Kweli ndugu, hata mimi natumia mara chache, maana nikiingia kwenye jukwaa lolote nakuta heading moja , kuona nyingine hadi niscroll , nimewasilisha hoja , now najaribu kuona kama ni mazoea au ndio naachana nayo ado ado
 
Mzee Maxence Melo pia na swala la font size kupitia browser, with bigger font size au probably ni design ya font mnayoitumia inapunguza ufanisi, ukifungua jf tu section nzima ya Trending imejazwa na title na hints ya thread moja tu. Kuscroll kupata hints za threads zingine inapunguza efficiency kwa sababu utatumia muda mwingi kuscroll whether you go down or up. Hii pia iapply na kwenye comments za members ndani ya thread baada ya kuifungua.
Fanyieni kazi hili kuwa uhai wa hii platform
 
Kweli ndugu, hata mimi natumia mara chache, maana nikiingia kwenye jukwaa lolote nakuta heading moja , kuona nyingine hadi niscroll , nimewasilisha hoja , now najaribu kuona kama ni mazoea au ndio naachana nayo ado ado
Mi nahisi naachana nayo mdogo mdogo maana zamani ikipita nusu saa sijaingia jf naumwa ila sasa hivi naisahau kama ipo
 
Kweli ndugu, hata mimi natumia mara chache, maana nikiingia kwenye jukwaa lolote nakuta heading moja , kuona nyingine hadi niscroll , nimewasilisha hoja , now najaribu kuona kama ni mazoea au ndio naachana nayo ado ado
Halafu ukienda kwenye recommended unakuta nyuzi za uchaguzi wa kenya tu, sijui ni kwangu tu au vipi?
Why ziwe za kenya tu sijui wamenionaje hawa watu..sijawahi changia nyuzi za kenya
 
Halafu ukienda kwenye recommended unakuta nyuzi za uchaguzi wa kenya tu, sijui ni kwangu tu au vipi?
Why ziwe za kenya tu sijui wamenionaje hawa watu..sijawahi changia nyuzi za kenya

😀😀😀😀 Kiswahili chako ni cha kikenya... kiswanglish
 
Back
Top Bottom