Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Hoja ipo mkuu labda kama huioni, mfano ofisi gani pale zanzibar ambayo mteuliwa ametoka bara na anaonekana kabisa huyu Mheshimiwa Rais kamtoa huko Itegambwike au Butata huko na kutokana na weledi wake anaweza kushika nafasi hiyo kwenye SMZ.

umeshasema SMZ, hiyo ni kwa ajili ya Zanzibar tu, watangnyika acheni kujimilikisha Utanzania.
 
Watu ni majuha sana Sasa hii ni habari hivi wewe ukipewa utawala utashindwa kuwapa vitengo watu wako unaowaamini?? Hii ni formula ya Dunia mzima acheni ushamba.Kila Raisi Huwa anaweka watu wake anaowaamini.
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
hii ndio sababu watu wanaitaka Tanganyika, inakuwaje mtanganyika hawezi kushika nyadhifa kule visiwani, ila wazanzibar wanashika nyadhifa tena kubwa zenye maslahi kwa Tanganyika? hapo wametega nini? yaani wanataka washike nyadhifa zooote kuanzia urais, wazili wa mambo ya ndani, waziri wa miundombinu, TRA na kwengine kote strategic?
 
The United Republic of Tanzania imeundwa na pande mbili kwa gharama ya upande mmoja kuji dissolve huku upande mwingine ukibaki. Tanganyika ilijigeuza mshumaa, ilijiangamiza kwa lengo la kuangazia wengine.
Hivyo, Muungano huu unampa Zanzibar kuwa access ya nafasi zote, maana Tanganyika ilishajiua hivyo kukabidhi kila kitu kwa Zanzibar, maana katika Muungano huu Zanzibar ndiye pekee aliye hai.
So, unapoongelea maliasili, taasisi, n.k Zanzibar ana mamlaka nazo zote, kama mmiliki upande mmoja, huku upande mwingine akiwa kama msimamizi maana Tanganyika ilipojiua iliacha watoto na wake kadhaa ambao wote walendelea kulelewa na Zanzibar. Hapo ndipo hesabu za nyerere zilipopotea na kuvurunda kila kitu.
Laiti Tanganyika ingekuwepo au ingefufuka leo, basi hapo itakua sawa kusema kuna vitu vya Muungano. Ila kwa sasa, Zanzibar ndiye anayetambuliwa ni vile tu hawaijui nguvu yao.
Sasa hivi Zanzibar wana nguvu ya kuamua lolote ndani ya Muungano na watoto na wa tanganyika wakatakiwa kupokea tu maelekezo.
Kwa kuwa Tanganyika ilishakufa, sasa hivi serikali ya Muungano inabaki kuwa chombo kinachomsikiliza zaidi Zanzibar kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale. Maana ndiye pekee aliye hai.
kati ya vitu vya kumlaumu nyerere ni hiki, hata sijui ilikuwa kwa faida gani huu muungano ambao siku zote hauna faida kwa bara.
 
Mkuu Nguruvi3, kwanza naheshimu mawazo yako yoyote hata kama sikubaliani nayo!
Kukubaliani katika kutokubaliana ni jambo lenye afya na ni uungwana.
Kuna vitu ni facts na kuna vitu ni fallacy,Miungano yote duniani, ni ama ni muungano wa union, ama muungano wa federation. Tanzania, ndio muungano pekee wa both, union at the same time ni federation!. This is unique and it's a fact.
Neno muungano 'unique' linatumika kama jibu la maswali yasiyo na majibu, si kwa maana unayokusudia wewe.
Kiukweli kabisa Watanzania tumenyimwa sana elimu ya uraia!, wakoloni wametufanya vibaya sana kwa kutoweka mitaala ya elimu ya uraia, matokeo yake tangu tumepata uhuru mwaka 1961, Watanzania hawajafundishwa kuhusu katiba wala uendeshaji wa serikali, wakoloni walifanya hivi makusudi ili watu wasijue!, lakini baada ya kupata uhuru na kujitawa kwanini watu hawafundishwi?.
Wakoloni au Watanzania hawana tatizo lolote, kuna tatizo la Katiba zilivyoandikwa.

Rejea katiba ya Uhuru, Mpito na ya kudumu utabaini zimebabaisha tu mambo.
Kwahiyo hakuna tatizo la elimu ya Uraia, kuna tatizo la mfumo wa utawala na hasa Katiba
Tulipoungana ile 1964, Watanzania tulipaswa kuelimishwa leo hawaujui muungano na ni chanzo cha i kelele na kero
Tatizo ni kutoshirikisha umma. Kwa mfano, Utawala umechukua westmister na ule wa USA.
Bunge letu linafuata taratibu za Commonwealth, mfumo wa utawala ni ule Marekani uchaguzi ni wa UK, ni vurugu tu. Habari ya akina Jaji Matungi kuleta utumbo mwingine, hapana! Tujiufnze kutokana na makosa
Katiba ya Tanzania ya 1977, tulipaswa tuelimishwe elimu ya uraia!. Matokeo yake waserikali ni mbumbumbu wa katiba ya JMT wanatunga miswada ya sheria inayokwenda kinyume cha katiba, Bunge ni la mambumbumbu wa sheria,linatunga sheria batili!, Mahakama ni mambumbumbu wanaliacha Bunge litunge sheria batili, na licha ya Mahakama kuzibatilisha, Mahakama mbumbumbu inalirudishia serikali mbumbumbu kupeleka kwenye Bunge mbumbumbu, ndio litengue sheria batili!.
Na ndiyo maana wanampa 'Matungi' kazi ya kuandika katiba tena. Hatujifunzi kutokana na makosa
Tuna wanasheria wabovu, vilaza na mbumbumbu wa katiba na sheria left, right and centre!, kuanzia kwenye mhimili wa serikalini, mhimili wa Bungeni hadi mhimili wa Mahakama!.
Tuna wanasheria wazuri , huwezi ku survive ukiwa na akili timamu ndani ya chama. kamata kamata , fungia mawakili, nyang'anya leseni inaeleza kitu.
Katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba, ni sheria batili!. Ubatilisho wa sheria batili, unabatilishwa na katiba yenyewe!, na sio Mahakama!. Kazi ya Mahakama Kuu ni kitafsiri katiba na sheria tuu, na kutangaza kubatilishwa kwa sheria batili, lakini kufuatia huo umbumbumbu wa katiba, mhimili wa Mahakama unaitangaza sheria fulani ni batili, halafu inawarudishia waliofanya ubatili huo ndio wairekebishe!, wakati ni katiba ndio imeitengua batili hiyo!. Huu kama sio umbumbumbu wa katiba na sheria ni nini?!.
Nilikueleza GPA na Utawala havina uhusiano. Tuna GPA Dodoma, utumbo. Nyingine Mahakamani ,aibu tu.
Tutakuwa tunawaonea bure Zanzibar!. Wakati tunaungana tulikuwa na mambo 11 ya muungano, tumekuwa tukiyaongeza kinyemela kinyume cha utaratibu mpaka yamefikia 26!. Karume akakomaa, gesi na mafuta
Ndiyo lakini mambo yaliyoongezwa kinyemela yanamnufaisha nani?

Mfano, elimu ya Juu ni kwa faida ya Zanzibar. Nafasi za vyuo vikuu ni za upendeleo siyo meritocracy. Unajua !
Nitajie jambo moja tu lililoongezwa kinyemela ambalo kwalo Tanganyika inanufaika. Nitajie moja tu

Nimewahi kuwauliza Wazanzibar wanitajie jambo moja tu, hakuna hata mmoja aliyewahi kunijibu.
Watanganyika wanasema ya kinyemela yaondolewe, wanahoji, Shaka Hamdu anakuwaje DC?
Tamisemi ni muungano? Watanganyika wanahojI, Mbarawa na Katibu mkuu wanakuwaje viongozi wa mambo ya Tanganyika. Huwezi kukataa ya kinyemela ukafanya unyemela. '' Nguruwe haramu mchuzi wake Halali''

Kwenye taasisi au wizara au idara ziszoi za muungano Wazanzibar waondolewe tusiingize mambo kinyemela. H
Hili lianze mara moja ili tuwatendee haki Wazanzibar. Ondoa katika eneo lisilo la muungano
Hili la katiba ya Zanzibar na katiba ya JMT ni tatizo!. Ni kweli marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010 yaliyounda GNU, ni marekebisho batili, ambayo sio tuu yameitambua Zanzibar kama ni nchi, huu ni uhaini!. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT!.
Tumekubaliana, Rais SSH anakoleza moto uvunjaji wa katiba ya JMT iliyomweka madarakani.
Kama Rais na ACT wanataka mamlaka kamili, atoe kura ya maoni kwa Wazanzibar waamue tu ! Waamue
Marebisho hayo yameipa katiba ya Zanzibar ukuu kuliko katiba ya JMT, na kusema sheria yoyote ya muungano itakayotungwa na Bunge la JMT, haitafanya kazi Zanzibar mpaka iridhiwe na BLW!. What is this!.
Ndiyo maana wana uwezo wa kutumia kodi zetu kwenda Dubai halafu wakirudi wanasema Bandari haiwahusu.
Ndiyo amaana wanaweza kusajili meli kwa njia haramu halafu sisi kama JMT tunabeba msala wao.
Ndiyo maana wana kiburi cha kutumia umeme bila kulipa ili walipiwe na mbeba mizigo wa Buguruni.
Rais SSH anaendeleza hayo , lakini kwanini asitoe kura ya maoni ili ACT na Wazanzibar waamue hatma yao?
Eti Rais wa Zanzibar naye ni Amiri Jeshi Mkuu wa JKU, KMKM na vikosi vya SMZ!.
Haaa! hii si ndiyo uniqueness ya Muungano.
Hakuna upacha wowote wa Zanzibar kimataifa, kimataifa nchi ni moja tuu, JMT, Zanzibar sio nchi, haiwezi kuingia mkataba wowote wa kimataifa au mkopo wowote wa kimataifa, ni lazima idhaminiwe na JMT!.
Sijui kama unaelewa nikikuambia Waziri wa fedha wa Zanzibar ame saini Mkopo siyo wa JMT.
Sijui kama unaelewa shirika la mafuta na gesi Zanzibar limeingia MoU tofauti na ile ya TPDC na nchi za uarabuni
Hivi Rais wa Zanzibar anaopingia mkataba na nchi kama Ujerumani ni kuifanya Zanzibar nchi kamili na si JMT
Zanzibar ina haki ya kupata mikopo ya kimaendeleo kwa udhakini wa JMT sio kuwalipia mkopo!. ikitokea waka default, wakashindwa kulipa, then mdhamini ndio anakuwa held responsible!.(Tanganyika)
Tunajua udhamini, lakini ikitokea default anayelipa ni Tanganyika. Ni default kama ya umeme waligoma na bili ya 60B analipa Mdhamini Mtanganyika wa Buguruni, Kagera, Chunya n.k. Lakini ikiwa Zanzibar wanalipa, Bajeti yao ya 2023/2024 ipo wazi. Naku challenge Pascal uonyeshe malipo ya mikopo kutoka bajeti ya Zbar
Kimataifa hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, hivyo hakuna bendera ya Zanzibar!, nchi ni moja tuu, JMT, kwenye issues za bahari Kuu, ni kama kwenye mikopo, Zanzibar inasajili meli lakini mdhamini ni JMT!, kukitokea timbwili, responsible ni mdhamini!.
Zanzibar wanafanya dili na Iran, wanachukua pesa kwa siritimbwili likitokea anayelipa ni Mtanganyika, this is rubbish and must end now. Wapewe mamlaka yao ikiwa ni pamoja na kubeba gharama za maamuzi yao
Hii ndio maana halisi ya udhamini!.

Japo katiba ya Zanzibar ni kwa mambo yao ya ndani kwenye mambo yote ya kimataifa, yanatuhusu!,r, it usually takes time huu udhamini wa serikali ya MT kwa Zanzibar, sio hisani, favour, ni wajibu, kwasababu Zanzibar ana haki ya kupata 4.5% ya mikopo na misaada yote ya kimataifa kwa Tanzania, hivyo Zanzibar ikikopa kwa udhamini wa JMT, ikashindwa kulipa, JMT itailipia, halafu huku sisi tunapiga panga ile 4.5% yao!.
Hakuna kitu kama hicho, Zbar wanapewa 1/3 ya mikopo na misaada, 4.5% ya pato la Tanganyika,.
Wanchangia 0% na matusi katika pato la JMT wakiwa juu ya mbeleko , wakilamba pipi na Juice mgongoni.
Sio kwa mujibu wa SSH, bali ndivyo katiba ya Zanzibar inavyosema!. Katiba ya JMT inasema Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye "sehemu mbili", Tanzania Bara na Zanzibar
Ikiwa kuna tatizo Rais wa JMT anapaswa kuliangalia si kulipapalia kama alivyofanya SSH
SSH kaagiza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya madini kuingia MoU na SMZ kupitia Wizara ya madini.
Ni kitu cha kushangaza kwamba Rais SSH anapalilia na kushadidia hoja akijua ita provoke upande mmoja.

Tanganyika wanakuwa provoked kwasababu SSH anasimama kama Rais wa Tanganyika ambayo Waziri wake wa madini ameingi Mkataba na Waziri wa madini wa Zanzibar, halafu SSH anasimama kama Rais wa JMT pale anapotaka masilahi ya Zanzibar. Hakuna tatizo kwa SSH kuipa mamlaka Zanzibar, lakini iwe kwa kura ya maoni.
Sii kweli!, japo ni kweli kuna Watanganyika ni wachache, wengi wetu ni Watanzania.
Muda ni mshiriki mzuri. Kama kuna wakati muungano upo njia panda ni huu wa SSH

SSH ana machaguo matatu tu , na kwa bahati mbaya hana back up kama ya Nyerere
1. Kurudisha Tanganyika iwe na mamlaka yake kwa mambo yake katika katiba mpya (Serikali 3)
2. Kuendeleza serikali 2, Watanganyika waje juu na siku moja tuwe na Mbeki au Zuma
3. Akatae mabadiliko ili aendelee kuwapa Wazanzibar mamlaka kamili kwa kuvunja muungano
Zanzibar kabla ya muungano alikuwa tajiri, muungano umeifanya kuwa masikini!. Zanzibar ndio nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na Colour TV, mwaka 1971!. Wakati tunaanzisha BOT ile 1966, Zanzibar ilikuwa na doleri za kufa mtu!. Kama sio muungano, Zanzibar ingekuwa mbali sana!, Dubai ingesubiri!.
Zanzibar ilikuwa tajiri kabla ya utumwa kwa kutumia rasilimali watu na vipusa wakati wa ukoloni
Zanzibar ikawa tajiri kwa kilimo cha karafuu ambacho sasa kinalimwa dunia nzima

Baada ya utumwa kufa na karafuu kufa, Zanzibar imebaki na uvuvi na utalii.
Ndivyo jiografia ilivyoipendelea na sasa inainyanyasa

Kuwa na TV ya rangi ni hoja za vijiweni baada ya kulewa kahawa na kashata.
TV ya Rangi aliangalia Sultani na Waarabu, Wazanzibar ambao hadi leo wanajisaidia baharini hawakuwa na TV.

Hioja ni za kizanzibar na naogopa kusema neno sensitive, kama ile hoja ya kipuuzi sana kwamba Kenyatta alikataa muungano. Ukiwauliza Wazanzibar lini alikataa hawana jibu, wamesikia fulani kasema!!

Ni hoja ya kizanzibar iya kusema kwanini nchi nyingine hazijaingia katika muungano bila kujua muungano unasababu zake ikiwemo zile za asili, tamudini , historia n.k. Ni ukosefu wa elimu tu na kusomewa vitabu

Ni vihoja vya kizanzibar kwamba Tanganyika yenye watu milioni 60 na uchumi wa 2 EA inaibia Zanzibar yenye watu milioni 1.5 tena nusu wakiishi Tanganyika.

Hivi kwa Bajeti ya 2.8 T sawa na ile ya Wizara ya ulinzi, unaiba nini hapo? NMB ina capital and assets za 11.Trilioni.

Sii kweli, it's a win win situation and lose lose situation, kila upande kuna vitu ime gain, kuna vitu ime loose.
Tanganyika ina win nini kwa Zanzibar? Hebu toa mfano mmoja tu na ina lose nini, toa mfano mmoja tu

Watu wengi wanakuuliza hili swali na wanasubiri jibu.
Ni kweli Zanzibar haichangii hata senti tano kugharimia uendeshaji wa muungano, kwasababu Tanzania bara imevaa koti la muungano!, hakuna gharama za muungano, ziko fused ndani ya budget ya JMT, anachotaka Zanzibar ni JMT iseme gharama, ndio wachangie.
Ahsante, Tanganyika imebeba mzigo wa muungano kwa kuvaa koti la Muungano.

Hoja hii ni nzuri na naomba uwe 'advocate' na Mentor' mzuri kwa lile kundi la Wapuuzi linalosema Tanganyika inanufaika kwa kuvaa koti la muungano. Koti la muungano ni zito limebeba mizigo, taka na vyoo!
Hiyo ni ajira halali yao, kosa ni letu, hatujui gharama za muungano!.
Awali umesema mambo 11 yameongezwa kinyemela. Sasa unasema ajira kwa mambo yasiyo ya muungano ni halali yao. Tukubaliane nawe, 21% kwanini Wazanzibar hawataki kulipia.

Nikueleze kitu, watumishi wa SMZ ni takribani 15,000. Zanzibar ikipewa 21% ya watumishi wa JMT. Kwa minajili ya mnakasha huu iwe 100,000, ina maana kwamba Zanzibar wanapewa 21,000.
Kati ya nafasi 21,000 nyingi ni za mambo yasiyo ya muungano zinazoporwa vijana wa Tanganyika.

Zinaporwa kwasababu Zanzibar wenyewe hawataki mambo zaidi ya 11 ambayo hayana ajira kiasi hicho.

Watanganyika wanasema ondoa mambo yote yalioongezwa kutoka 11, ondoa Wazanzibar katika mambo nje ya 11 ili Watanganyike wabaki na ajira zao kama ilivyo kwa Zanzibar.
Yote hayo ni matatizo ya koti la muungano.
Nimeorodhesha mambo umekubali ni matatizo ya Muungano na anayebeba matatizo ya muungano ni Tanganyika kwa gharama za rasilimali, kuwanyima watu wake fursa na kisha kupokea matusi kutoka kwa Jussa, Othman Masoud, Duni na ACT Wazalendo.

Hatuhitaji ugomvi na mtu, katiba mpya tuwe na Tanganyika na wabaki na Zanzibar yao njema, wakitaka tuwe na 3 ambako tutasimami mambo yetu hakuna MoU ya ajira, ardhi, au chochote kwasababu hatutanufaiki na chochote kutoka Zanzibar. Hatuna cha kupoteza
Naomba be a bit sensitive kwenye hizi issues za muungano, wenzetu damu imemwaika!, wana machungu na makovu!.
Mbona wao wanatumia lugha kali dhidi ya Tanganyika. Hakuna sensitivity ukweli ni ukweli na upuuzi tutaita hivyo.
Eti Tanganyika imevaa koti inafadika, hii elimu ya wapi! Huu ni upuuzi tu ukimsikia mtu anashadidia jiulize ..
No tukivunja muungano, we have everything to loose and nothing to gain, kwa kuulinda muungano, we have everything to gain and nothing to lose, hivyo tumeamua muungano wetu huu adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P.
Tuna lose nini? Hebu eleza kwa jamvi. Na sasa hivi tuna gain nini?
 
Bila huu Muungano usioeleweka kuvunjwa Waarabu koko watatuburuza sana.
Tatizo mlikremishwa kanisani kuwa Tanzania ni nchi ya kikristu ndio maana mbapaniki na kuona mnanyan'ganywa haki yenu kauli za kibaguzi za kidini zimejaa humu mara anatoka mvaa kobazi anaingia mvaa kobazi dah kweli tulikuwa hatujui mengi
 
Mbona Mtanganyika hawezi kufanya kazi kwenye taasisi za Zanzibar kama ZRA, ZPA, nk?
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ni Mtanganyika anaitwa Yusuf Mwenda alitokea TRA. Alishawahi kua MEYA wa Manispaa ya Kinondoni kama kumbukumbu zangu ziko vizuri.
 
Haya mambo Samia na dk Mwinyi wameyakuta. Wakati muungano unasainiwa kipindi hicho wao walikuwa watoto wadogo wakisoma shule ya msingi au pengine secondari.
Kama Kuna lawama katika kadhia ya muungano wakulaumiwa ni Nyerere na Karume na Siyo Samia na Dk Mwinyi.

Wakati wa kusainiwa Muungano Samia alikua ana umri wa miaka 4, Hussein alikua hajazaliwa.
 
Unelewa vizuri sana sema umeamua kujitia ujinga.

Zanzibar wana Bandari zao kwaajili ya Wazanzibari.

Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi kwaajili ya Wazanzibari.

TPA & TRA ni kwaajili ya watanganyika kutuletea Wazanzibari huko ni kuwadharau watanganyika million 61.

Kwakuwa hakuna mtanganyika ZPA & ZRA ni ujinga wa kiwango cha SGR kutuletea Wazanzibari kuongoza taasisi ambazo zipo Tanganyika.
Zanzibar hakuna Taasisi inayoitwa ZPA
 
Unelewa vizuri sana sema umeamua kujitia ujinga.

Zanzibar wana Bandari zao kwaajili ya Wazanzibari..
Kule Zanzibar asilimia 80 ya watu wana asili, damu, na makabila ya Tanzania Bara. Hii wengi hamjui.

Ukiacha upotoshaji ulioufanya, TRA ni chombo cha Muungano, kipo Zanzibar na kinakusanya kodi zote stahiki kutoka kwa Wazanzibari.

Aliyechaguliwa kuwa Kamishna wa kodi ni mfanyakazi mwandamuzi wa TRA aliefanya kazi Tanzania bara miaka mingi na anajua vyema mifumo yake.
 
Tatizo mlikremishwa kanisani kuwa Tanzania ni nchi ya kikristu ndio maana mbapaniki na kuona mnanyan'ganywa haki yenu kauli za kibaguzi za kidini zimejaa humu mara anatoka mvaa kobazi anaingia mvaa kobazi dah kweli tulikuwa hatujui mengi
Mimi binafsi huwezi kuona post yangu kuusema uislamu kwa sababu nami ni muislamu lakini sikubaliani na wale wanaofikiri uislamu ni Uarabu hivyo siku zote siwapendi waarabu hasa waarabu koko toka Zanzibar kwa sababu na wao hawatupendi jamii ya watu weusi iwe muislamu au mkristo wote wanatubagua.
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
kama mama anawapenda sana ndugu zake basi aivunje SMZ kuwe na unitary government, haiwezekani mtu ambaye siyo mtanganyika ashike madaraka katika taasisi ambayo siyo ya muungano, watanganyika tuamke, wakati ni sasa. Mtu kutoka Tanganyika hawezi hata kuajiriwa kwa ajira za kawaida kule zanzibar
 
Kamishna wa forodha Said Athuman Kiondo, ameondolewa nafasi yake na kuchukuliwa na Juma Bakari Hassan.

Kamishna Juma Bakari ndiye atahusika na ushuru wa Forodha TRA (customs) ndani ya ofisi ya meneja wa Bandari.

Idara ya Ushuru na Forodha inasimamia kodi zote zinazohusu biashara ya kimataifa. Kodi hizo ni pamoja na Kodi ya Uingizaji Bidhaa, Ushuru na Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa bidhaa ziingizwazo nchini. Kodi ya uingizaji bidhaa ni kodi inayotozwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini.
20230802_184411.jpg
20230802_184414.jpg
 
Kamishna wa forodha Said Athuman Kiondo (Tanganyika), ameondolewa nafasi yake na kuchukuliwa na Juma Bakari Hassan (Zanzibar)

Kamishna Juma Bakari ndiye atahusika na ushuru wa Forodha TRA (customs) ndani ya ofisi ya meneja wa Bandari wakati Bandari zetu zikiwa mateka wa DP WORLD

Idara ya Ushuru na Forodha inasimamia kodi zote zinazohusu biashara ya kimataifa. Kodi hizo ni pamoja na Kodi ya Uingizaji Bidhaa, Ushuru na Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa bidhaa ziingizwazo nchini. Kodi ya uingizaji bidhaa ni kodi inayotozwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini.
View attachment 2706440View attachment 2706442View attachment 2706447
Tanganyika ishakua koloni tena la nchi ndogo kabisa
 
Back
Top Bottom