Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Unelewa vizuri sana sema umeamua kujitia ujinga.

Zanzibar wana Bandari zao kwaajili ya Wazanzibari.

Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi kwaajili ya Wazanzibari.

TPA & TRA ni kwaajili ya watanganyika kutuletea Wazanzibari huko ni kuwadharau watanganyika million 61.

Kwakuwa hakuna mtanganyika ZPA & ZRA ni ujinga wa kiwango cha SGR kutuletea Wazanzibari kuongoza taasisi ambazo zipo Tanganyika.
😆😆😆😆
 
Njaa tu itawaua kule hakuna kitu. Mishahara ya watumishi wa Zanzibar inaashiria hivyo
Sasa imekuwa ni njaa na sio kubaguliwa Watanganyika kwenye ajira? Nimesema tukinyamaza sio kwamba hatuwezi kusema ni ustaarabu tu tulionao. Usimpe bubu kusema.

Sasa semeni tuvunje muungano kwasababu Watanganyika hawaajiriwi Zanzibar, Watanganyika hawapati ardhi na mingine ili tukuonesheni uongo wenu.

Mukitaka kuvunja muungano vunjeni tu musilete visingizio.
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
Watanganyika mna wanyanyasa Sana wazanzibari..
 
Na hapa ndipo tunaona umuhimu wa katiba mpya kumaliza kila upumbavu unaoanzishwa na wana ccm hapa bara.
 
Ndiyo kusema Zanzibar ni nchi huru, lakini Tanganyika ipo kwenye mabano hiv

Ndiyo kusema Zanzibar ni nchi huru, lakini Tanganyika ipo kwenye mabano hivi!!!
Kwenye Ramani ya Dunia hakuna nchi inaitwa Tanganyika.
Hakuna rais wa Tanganyika, bunge la Tanganyika, mahakama ya Tanganyika Wala jeshi la Tanganyika.
Hivyo vyote vilikuwa vya Tanganyika kabla ya muungano baada ya muungano Tanganyika na kila ilichokuwa nacho vilizikwa kwa ajili ya maslahi ya muungano.
Nyerere alosema 1 + 1 = 2 na jibi haliwezi kuwa 3.
 
Huu muungano gani unaotoa haki ya upande mmoja tu.

Wazanzibari chao ni chao tu ila vya tanganyika ni vya wote.

Wizara hata zisizo za muungano wazanzibari wamejazwa humo.

Hakuna mtanganyika hata mmoja anayeruhusiwa kumiliki kipande cha ardhi huko Zenj, wazenj wanawapangia bajeti watanganyika, mbaya zaidi wazenj wanawaamulia mambo makubwa watanganyika huko bungeni na nje ya bunge. Rejea bandari.
Haya mambo Samia na dk Mwinyi wameyakuta. Wakati muungano unasainiwa kipindi hicho wao walikuwa watoto wadogo wakisoma shule ya msingi au pengine secondari.
Kama Kuna lawama katika kadhia ya muungano wakulaumiwa ni Nyerere na Karume na Siyo Samia na Dk Mwinyi.
Kinachofanyika sasa ndicho ambacho Nyerere na Karume walikubaliana kwamba mambo ya muungano ni ya watanzania wote na Yale ambayo siyo ya muungano ni ya wazanzibari.
 
Huu muungano gani unaotoa haki ya upande mmoja tu.

Wazanzibari chao ni chao tu ila vya tanganyika ni vya wote.

Wizara hata zisizo za muungano wazanzibari wamejazwa humo.

Hakuna mtanganyika hata mmoja anayeruhusiwa kumiliki kipande cha ardhi huko Zenj, wazenj wanawapangia bajeti watanganyika, mbaya zaidi wazenj wanawaamulia mambo makubwa watanganyika huko bungeni na nje ya bunge. Rejea bandari.
Haya mambo Samia na dk Mwanyi wameyakuta. Wakati muungano unasainiwa kipindi hicho wao walikuwa watoto wakisoma shuke ya msingi au pengine secondari.
Kama Kuna lawama katika kadhia ya muungano wakulaumiwa ni Nyerere na Karume na Siyo Samia na Dk Mwinyi.
Kinachofanyika sasa ndicho ambacho Nyerere na Karume walikubaliana kwamba mambo ya muungano ni ya watanzania wote na Yale ambayo siyo ya muungano ni ya wazanzibari
 
Hilo la mtu wa bara kuteuliwa kufanya kazi Zanzibar haliwezi kutokea kwa sababu ofisi za Zanzibar siyo za muungano. Wazanzibari wanateuliwa kufanya kazi Tanzania bara kwa sababu ofisi za Tanzania bara kuanzia ikulu, mahakama, Baraza la mawaziri,bunge na majeshi yote ni ya muungano.
Hapo ndipo penye mjadara sasa and not otherwise.
 
Kwenye Ramani ya Dunia hakuna nchi inaitwa Tanganyika.
Hakuna rais wa Tanganyika, bunge la Tanganyika, mahakama ya Tanganyika Wala jeshi la Tanganyika.
Hivyo vyote vilikuwa vya Tanganyika kabla ya muungano baada ya muungano Tanganyika na kila ilichokuwa nacho vilizikwa kwa ajili ya maslahi ya muungano.
Nyerere alosema 1 + 1 = 2 na jibi haliwezi kuwa 3.
Ilikuwepo kwenye ramani ya mwaka 1963. Tunataka iwepo kwenye ramani ya sasa.
 
Back
Top Bottom